Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 424.

  • 14 Nov 2024 in Senate: Najua hakuna atakayetusumbua na mambo ya kutoa fedha katika harambee. Waswahili husema, “Kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.” Hakuna anayelazimishwa kwenda kutoa. Mtu hutoa kwa hiari yake. Swali nauliza, mzigo ulio kichwani, kwapa lakutokeani jasho? Kama sijalazimishwa mimi kutoa fedha, kwa nini nianze kutengeneza sheria ya pesa ambayo inatolewa na mtu anayetoa kwa hiari? view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Matatizo ambayo yako hapa yanamkumba sana mwananchi wa kawaida. Na siku ambayo mbwa anatua katika sehemu nyeti, hiyo ndio siku mtu hujua sio kila tatizo huwa linatatuliwa kwa fimbo au nyundo. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Shida tuliyonayo saa hii sio lazima itatuliwe kwa sheria. Ni tatizo ambalo linafaa kutatuliwa kwa kuweka miundo msingi mbele ili wananchi waweze kuendelea. Sheria kama hizi ndio wakati mwingine hufanya wananchi wajiulize kama waliweka chui zizini. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Wakati tunapoomba viti, wanaotushikilia ngazi ni wale wananchi wa kawaida. Unajua, mtu anayehusika kupandisha wengine ngazi hupigwa teke kwa meno kwa sababu anayemshikilia anaenda juu ilhali miguu iko chini. Kwa hivyo, ni rahisi sana kumpiga teke kwa meno. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Hivyo basi nasema ya kwamba, mimi kama Seneta wa Kirinyaga, nikikaa katika baraza, wale wanaokalia kumbi na vigogo, vile wanavyoongea kuhusu shida walizonazo, mimi nitakuwa kama mtu wa kuwapiga teke kwa meno nikisema huu Mswada unafaa kwa wakati tulionao kwa sasa. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Mambo ambayo mimi nimeyapitia, na wengi wanaokaa katika Seneti, naweza kudhihirisha ya kwamba wanaoketi hapa wengi walipita na kusoma kwa sababu watu walikuja pamoja kwa harambee wakawachangia pesa. Kwa hivyo, ile njia iliyowapitisha kuwafanya walivyo siku ya leo, mimi naomba tusije tukaifunga. Kwa nini? Angalia mtu aliyefiwa kwa sababu ya kukosa matibabu. Mwili unafungiwa makafani kwa sababu familia haina pesa ya kuutoa. Labda mwendazake alikufa kwa sababu ya ukosefu wa matibabu. Kama tungelainisha maneno na kuhakikisha kuwa matibabu yanapatikana, pengine tungezuia vifo na hakuna mtu angeitishwa pesa. view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Najua kuwa mnachangia sana kulipa karo za wanafunzi kwa kupeana bursary . Tumeongea sana kuhusu jambo hilo. Kuna Mswada unaonuia kufanya elimu kutoka kiwango cha chekechea hadi chuo kikuu bila malipo. Mswada huo ukiwa sheria, hakuna mtu atatuita kwenda kuchangisha pesa ya watoto kwenda shuleni. Kwa nini tusianze na kutengeneza sheria ambazo nimetaja? Kule kwetu, kuna msemo kuwa anayekula kwa kijiko huwa hajui kuchomeka kwa anayekula kwa mikono. Kama sisi tuna bima, hatuna matatizo na hatutaki kuchangiwa, tusisahau kwamba wanaoitisha msaada wana shida na wanafaa kusaidiwa. Bw. Spika wa Muda, kwa kumalizia, nilipokuwa nimeketi hapa, nilipata jumbe kadhaa za watu ... view
  • 14 Nov 2024 in Senate: Mimi kama Seneta wa Kirinyaga, kwa sababu ya watu wa Kirinyaga na Kenya nzima, kwa wale wote ambao nimeongea nao na wale wanaoketi katika mabaraza kuongea shida zao na kutualika sisi kwenda kuwapa msaada, kwa ajili ya akina mama na wale ambao wamejiunga katika vikundi kule Kirinyaga ili kuchangisha pesa kusaidia waliofiwa, sitaunga mkono Mswada ulio mbele yetu. view
  • 13 Nov 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Ili nifike hapa mapema nilitoka nyumbani kumi asubuhi. ndio nipate nafasi ya kujadili kuhusu mengi hususan yanayohusu Wizara ya Afya ambayo ni muhimu sana katika nchi hii. Tunaweza jenga barabara na mambo mengi lakini hatuwezi yatekeleza majukumu haya kwa wafu. Wanaotumia hizo huduma ni waliohai. Namwombea Daktari Hon. Barasa apone haraka na apate nafasi ya kuja kujibu maswali. Waswahili husema kiserema hulima kuliko jembe jipya. Yeye ni daktari, kwa hivyo ni mzoefu wa mambo yanayolingana na hospitali na basi majibu ambayo tungepata saa hii yanafaa kusuluhisha maswali yote yaliyoulizwa. La kutatanisha sana ni majibu ya Waziri ... view
  • 13 Nov 2024 in Senate: Hon. Rebecca Miano. Samahani nimepewa taarifa isiyo ya kweli na rafiki yangu hapa. Bw. Naibu Spika, Hon. Miano hakuwa mgonjwa lakini ameamua kuenda kuweka vifaru, vifaa vya ufuatiliaji katika hifadhi ya wanyama pori. Katika taratibu ya wanaombeba na uzito, anatuchukulia kwa bei rahisi kama bei ya chumvi. Ameweka vifaru kwanza halafu Bunge la Seneti linafuata. Kwa nini hangempa mwengine jukumu hilo? Nina uhakika kuwa sio yeye anaweka vifaa hivyo. Tumepoteza nafasi ya kuongea kuhusu kinachoendelea katika serikali. Waswahili husema ukikalia kuti kavu kuanguka sio ajali na--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus