Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 424.

  • 13 Nov 2024 in Senate: Bw. Naibu Spika, kusiwe na mazoea ya Mawaziri kukataa kuja hapa baada ya kualikwa. Waswahili pia husema kuti la mazoea humwangusha mgema. Mawaziri hawa wataanguka kwa sababu ya kuzoea kukosa kuja hapa. Asante. view
  • 12 Nov 2024 in Senate: Asante sana Bw. Spika. Kulingana na Kanuni ya Kudumu ya 159(1) ya Bunge la Seneti, naomba kuondoa katika Ratiba, The Rice Bill (Senate Bills No.19 of 2023). Sababu kuu ni ili tushauriane na wahusika wakuu wakiwemo wakulima na wote wanaohusika ili kuwasilisa huu Mswada katika Seneti kwa safari moja. Asante sana. view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa hii nafasi. Kwanza, ninashukuru kamati iliyokaa chini na kuhakikisha wamefanikisha maelewano kati ya fedha ambazo zinaenda kaunti zetu. Kazi inayofanywa na Maseneta ni muhimu sana. Shida ambazo wanapitia kuhakikisha kwamba pesa zinazoenda kwa gatuzi zetu zimefika ni kazi ngumu, ni kazi msalagambo. Ni kazi inayohitaji Maseneta kumakinika na kutetea gatuzi zetu. Bw. Naibu Spika, jambo la ajabu ni kwamba hizi fedha zinapofika katika kaunti zetu, magavana wengi wanajifanya kama miungu na hawawezi kulizwa maswali. Ni kama Seneti tumekuwa tingatinga; kazi yetu ni kuchukuliwa kubomoa milima na tunapomaliza kutengeneza barabara na fedha kufika kaunti ... view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati ni vizuri niseme ya kwamba, miradi mingi ambayo inafanyika katika gatuzi zetu ni kama magavana wengi wamesahau kuna ukulima na uvuvi. Katika nyanja ya uchumi samawati, shida iliyoko ni kwamba, ukiangalia zile bajeti zinatengenezwa na kupelekwa bunge zetu za kaunti, huwezi pata hata moja imewekwa pesa za kutosha kwenda kwa uchumi samawati. Tumetembea sehemu mbalimbali kule uvuvi unafanyika na cha kushangaza ni kwamba, wavuvi bado wanahangaika na bado kuna fedha zinafaa ziende kusaidia wale wavuvi. Bw. Naibu Spika, mkulima ni mtu wa maana na nitaregea ... view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Mwea. Hii inagharimu wakulima shilingi 1,200 katika kila gunia. Kama mkulima atapoteza shilingi 1,200 kwa sababu ya miundo msingi ambayo inafaa itengenezwe na gatuzi ya Kirinyaga, inamaanisha kuwa ile faida yote inapatikana kwa sababu ya kupata mbolea ya ruzuku na pembejeo za bei ya rahisi inapotea. Ningependa kumwambia gavana wangu kuwa mghala muue na haki yake umpe. Tuhakikishe kwamba huduma za barabara na miundo msingi imeboreshwa ili wakulima waweze kufaidika. Sio haya tu ambayo nilikuwa nataka kusema siku ya leo. Najua kwamba kamati nyingi zimekuwa na matatizo kubwa wakati tunawaita magavana hapa kuja kujibu maswali. Mswahili husema Mrina haogopi nyuki. ... view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Ninaomba kwamba, Mswada kuhusu ustawishaji wa pamba, marekebisho yaliyotoka Bunga la Taifa Mswada Nambari 5 wa 23--- view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. I beg to move that the National Assembly amendments to the Cotton Industry Development Bill (Senate Bills No. 5 of 2023) be now considered. view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika, Mswada wa pamba ambao uko mbele yetu ulimaliziwa katika Bunge la Seneti na ukaenda Bunge la Taifa ili uweze kuzingatiwa baada ya kufanya misururu ya mikutano na uhamasishaji wa umma katika sehemu tofauti na Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati ya Seneti kuleta ripoti katika Seneti. Ilipoenda kule, kuna marekebisho ambayo Bunge laTaifa limeomba yafanywe na ukarudishwa tena kwa Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati. Tulikaa chini na tukavalia njuga swala hilo na tukaangalia mambo yote ambayo yanafaa kuangaliwa, na tukakubaliana kwamba, marekebisho yote yaliyotoka Bunge la Taifa yanafaa kuzingatiwa. Kwa hivyo, hakuna Seneta aliyekuja ... view
  • 27 Oct 2024 in Senate: nchi, Bonda la Ufa, maeneo ya Kati, Ukambani na uende mpaka Lamu katika eneo la Pwani, pamba kwa sababu inastahimili ukame, inaweza kukuzwa katika sehemu nyingi. Ni kitega uchumi kizuri na kama tutawekesha na kuhakikisha kwamba kuna mtaji wa kukuza pamba, pembejeo zinapatikana na mbegu zinaitwa za BT, ambazo kilo moja ni zaidi ya Shilingi 7,000 lakini ni pamba nzuri sana ikipewa wakulima. Tulionelea ikiwa wakulima watapewa nafasi na pembejeo, watanufaika pakubwa na pamba. Bw. Spika wa Muda, pamba ni mmea ambao una maana sana kwa sababu, ukitoa ile pembe kwa kimombo inaitwa lint, itatengeneza nguo. Ukitoa mbegu ya ndani ... view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Samahani, Bw. Spika wa Muda. Nitahakikisha nitafuatilia maagizo hayo. Nilikuwa namalizia kwa kusema ya kwamba, mmea wa pamba ni mojawapo ya mimea ambayo inasawasisha jamiii nyingi nchini. Wakati kuna watu ambao wanasamehewa mikopo, kuna watu wanaopewa mitaji, iwe kwamba kila Mkenya ana mmea unaompatia pesa za kujikimu. Ukiangalia takwimu ya mahali ambapo pamba inapandwa, pamba ni mmea unaoweza kustahimili ukame. Sehemu nyingi nchini zinaweza kukuzwa pamba. Pia, katika Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuna miswada ambayo tutawasilisha kuhusu jamii za wafugaji ili kuhakikisha kwamba wananufaika na kilimo biashara. Mswada huu utakapotiwa sahihi na Rais wa Jamuhuri ya Kenya utakuwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus