27 Oct 2024 in Senate:
Wakati Rais alisema kuwa Mswada wa Sukari uko hapa uzingatiwe, tulichoma mafuta usiku kucha na mchana kutwa. Mimi kama Mwenyekiti mwenza Mheshimiwa Emanuel Wangwe tukakaa chini na kuhakikisha kuwa tumemaliza kushughulikia Mswada huo. Tunapoongea, kuna matumaini katika wakulima wa miwa, kahawa na majani chai. Kwani kama Seneta wa Bomet umeleta Mswada kujaribu kulainisha mambo ya kilimo cha chai. Matumaini ya wakulima wa ndengu yako wapi? Matumaini ya wakulima wa pamba yako wapi? Kutakuwa na matumaini kama tutakuja na kuhakikisha kwamba Miswada kama hii inapita bila siasa ambazo hazina maana. Nikimalizia, Waswahili husema wavuvi wa pweza hukutana mwambani. Sisi kama Maseneta ...
view
27 Oct 2024 in Senate:
Samahani, Bw. Spika wa Muda. Nitamuita Seneta wa Kitui, Sen. Wambua, kuunga mkono Mswada huu.
view
27 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Naomba unipe dakika tatu ili nishukuru wale Maseneta ambao wameunga mabadiliko ambayo yameletwa katika Mswada huu wa pamba. Pili, ni kuwa pamba ni mmea muhimu sana kwa sababu inakuwa malighafi ya chakula cha wanyama na mafuta. Sen. M. Kajwang' ambaye pia ni mmoja wa walio The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
27 Oct 2024 in Senate:
katika Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi tulipata kuzuru Kaunti ya Kitui na kupata ya kwamba mafuta yanayotolewa katika mbegu za pamba yanatumika kutengeneza nguvu za umeme ya kutumia kwa generator zao na pia yanatumika kwenye gari zao. Sen. M. Kajwang' ndiye mwenyekiti wa Kamati inayohusika na mabadiliko ya tabia nchini. Kwa hivyo, hilo ni jambo nzuri sana tukiweza kuipata. Pamba sio nguo pekee ila ni malighafi ya vitu vingine vingi. Bw. Spika wa Muda, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Seneti No.66(3), naomba swali la Mswada huu liahirishwe hadi siku nyingi. Asante.
view
17 Oct 2024 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Kwanza ningetaka kumuombea afueni haraka Naibu wa Rais. Ningependa kusema hivi, fisi anapotaka kula mwanawe, husema kwamba ananuka kama mbuzi. Ni dhahiri shairi kuwa, mashtaka iliyo mbele yetu leo ni fisi anayetaka kumla mwanawe. Wakati Sen. Thang’wa alikuwa anaongeo hapa, leo ulimwambia uombe msamaha. Alikuwa amemwambia Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Jinai kwamba anapojibu, ajibu na wanao. Mashtaka ambayo imekuwa na kampuni zote zilizokuwa hapa, mingi zilikuwa za watoto wake Rigathi Gachagua. Ama kweli, chambilecho, mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu. Kwa sababu hakuwezi kuwa na ubaguzi wa wanawe Naibu Rais, lakini kusiwe wale wengine ...
view
17 Oct 2024 in Senate:
Mimi nimetoka Kirinyaga na ninajua mashtaka yote 11 ambayo yako hapa. Kuna jambo moja ambalo mpaka ufanye kama utadhihirisha hayo mashtaka na ni ushiriki wa umma ambao tuko na ushahidi mbele yetu. Katika ushirika wa umma ambao tuko nao mbele yetu, isipokuwa picha za maofisi za National Government – Constituency Development Fund (NG –CDF) na takwimu ambazo zimetoka katika Bunge la Kitaifa. Hii ni kwamba wale wote ambao walikuwa wametia sahihi kumuondoa Naibu wa Rais ndio walio ongoza katika ushiriki wa umma. Bw. Spika, ningeuliza itakuwaaje na itawezekanaje mtu ambaye ametia sahihi kumuondoa Naibu wa Rais anaongoza katika ushiriki wa ...
view
17 Oct 2024 in Senate:
kuzingatia ushahidi na kuangalia kila jambo na maombi ambayo tuko nayo katika Seneti kuwa wenye haki na uaminifu. Asante sana.
view
17 Oct 2024 in Senate:
Asante, Mhe Spika. Swali langu litaeenda kwa Bw. Abdi. Kwa sababu anayehukumiwa hapa ni Naibu wa Rais, tungetaka kujua ya kwamba kwa sababu mlifanya uchunguzi, ni kesi ngapi ama kuna kesi yeyote ambayo EACC imepeleka mahakami ili Naibu wa Rais ahukumiwe? Jambo la pili, wakati Naibu wa Rais alikua anachunguzwa katika Bunge la Kitaifa, kuna ushaidi wowote ambao wewe uliwasilisha? Kama hukuwasilisha, kwa nini umeamua kuwasilisha hapa Bunge la Seneti na sio Bunge la Kitaifa? Swali la mwisho, katita zabuni ambayo ilikuwa ni ya vyandarua vya mbu ambayo inasemekana Naibu wa Rais alihusika nayo, ile zabuni ilikuwa imeghairiwa na KEMSA,
view
17 Oct 2024 in Senate:
kwa lugha ya kingereza na ilifaa kurudushwa. Je, hio dhamana ya zabuni ilirudishwa ama iliitishwa? Ingekuwa inasiadia Naibu wa Raisi na nini ama kungekuwa na manufaa gani ya kurudisha thamana ya zabuni kama ulivyorudisha zingine 17? Ningependa kujua hayo. Asante.
view
16 Oct 2024 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Ningetaka kumuuliza Mhe. Mutuse swali kwa sababu kampuni nyingi ambazo ameorodhesha pale kama ushahidi ni kwamba ni za watoto wake Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua. Kwa sababu umesema umefanya kazi kama wakili, lazima ulikuwa unafanya kazi kupitia kampuni. Je, ilikuwa ni kwa ajili ya ulaghai ukiwa na baba yako na kwamba wale watoto ambao umewaorodhesha pale, wote walitengeneza kampuni ili kulaghai pesa kupitia zile kampuni? Swali langu la pili ni kwamba, katika stakabadhi ambazo zimewekwa pale, zinaonyesha kwamba waliokuwa wanafaa kupata mgao wa shares katika kampuni, kuna wale walikuwa wanafaa kupata asilimia 30 na ile miradi ...
view