Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 91 to 100 of 424.

  • 15 Oct 2024 in Senate: Asante sana, Mstahiki Spika wa Muda, kwa kunipa hii nafasi. Kwanza kabisa, ni jambo la aibu kwa sababu aliye gavana wa Kaunti ya Isiolo, mhe. Abdi Guyo alikuwa Mwakilishi Wadi ya Matopeni. Wakati huo nilikuwa Mwakilishi Wadi wa Kerugoya. Mhe. Guyo, pia alikuwa Kiongozi wa Wengi kama mimi. Nilipokuja Seneti, yeye naye alifanikiwa kuwa gavana wa Kaunti ya Isiolo. Tunaamini kwamba ukifanikiwa kupanda ngazi kutoka Mbunge wa Bunge la Kaunti hadi kuwa gavana, huwa umesoma mambo mengi. Ni vibaya na aibu kuona wanaofanikiwa kupanda cheo kutoka kuwa waakilishi wadi hadi kuwa magavana, ndio wanavunja sheria. Hiyo ni kutuharibia sifa hata ... view
  • 14 Oct 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ninakushukuru kwa kusikiilza ombi la Kiongozi wa Seneti wa Walio Wengi, Sen. Cheruiyot, na kuruhusu Wawakilishi wa Wadi kusikiliza kesi hii. Mimi pia nilikuwa Mwakilishi wa Wadi na ni vizuri kuhudhuria kikao kama hiki na kushuhudia kwa sababu kesho wataweza kuwa hapa pia. Katika Kanuni zetu za Kudumu, Nyongeza ya Tatu ambayo inatoa masharti ya utaratibu wa kusikiliza na kuamua mashtaka ya kumwondoa gavana mamlakani; Kanuni ya Kudumu namba 80(12) inasema masharti ambayo yamepeanwa yakizingatiwa, gavana atasikilizwa na ushahidi utakapoanza, utaendelea hadi Seneti itakapohitimisha kusikiliza swala hilo. Bw. Spika, tumeanza kusikiliza jambo hili na Kanuni zetu za ... view
  • 25 Sep 2024 in Senate: Bw. Spika, kwanza nampa kongole kwa kuwa Waziri katika Serikali ya Kenya Kwanza. Kuna upungufu wa wafanyakazi, haswa katika Huduma Centres nyingi. Unafanya au unakusudia kufanya nini kuhakikisha kwamba kuna wafanyakazi wa kutosha ili kuhakikisha hakuna foleni za kupata huduma zinazotafutwa sana na Wakenya katika Huduma centres? view
  • 25 Sep 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada ambao unafaa kurekebisha sheria ambayo inahusika na vyama vya ushirika, Mimi ni Seneta wa Kenya kutoka Kaunti ya Kirinyaga. Kirinyaga kuna vyama vya ushirika 14 ambavyo vinashughulika na kahawa iliyo kwenye viwanda 75. Kuna chama kimoja kikubwa cha ushirika ambacho kinashikanisha vyama vingine vidogo; chama hiki kinaitwa Kirinyaga District Cooperative Union. Chama hiki kiliundwa baada ya Kenya kupata Uhuru. Vyama vya ushirika ni muhimu. Wakulima wanaouza mazao yao kupitia vyama vya ushirika, wanaweza kusaidika kupata bei nafuu. Mswahili husema umoja ni nguvu. Kwenye ukuzaji wa mchele katika eneo la ... view
  • 25 Sep 2024 in Senate: kupenyea na kuanza kuwafinya wakulima. Ndio maana nataka kumshukuru Sen. Mariam Omar kwa sababu Mswada huu ukiwa sheria, itarekebisha shida tulizonazo kwenye sekta hii. Niruhusu niongee kuhusu vyama vya ushirika ambavyo vinahusika na ukuzaji na uuzaji wa kahawa nchini. Shida za wakulima wa kahawa zinafanana katika kila sehemu ya nchi ambapo kahawa inalimwa. Mkulima wa kahawa kutoka Kirinyaga, Tongaren, Mt. Elgon na kwingineko hupitia shida zinazofanana. Sheria ya marekembisho ambayo imeletwa na Sen. Mariam Omar itatibu shida hizi. Kaunti ya Kirinyaga kuna vyama vya ushirika vya Mutira na Kibirigwi ambavyo vilikuwa na mgomo na kubandua mwenyekiti wa chama. Iwapo mtu ... view
  • 25 Sep 2024 in Senate: Unapata kwamba mwenyekiti wa chama cha ushirika kama kile anaeza omba shilingi milioni 3. Katika kuomba zile pesa, mali ya dhamana ni ya wakulima. Ni vizuri tutakapoangalia marekembisho ya vyama vya ushirika tupitishe sheria ambayo itazuia viongozi hawa kukopa pesa ya wakulima bila kuhusisha zaidi ya wakulima theluthi mbili ambao ni wanachama kwenye chama cha ushirika. Jambo la pili ni kwamba vyama vingi vya ushirika vimeunda SACCO. Kaunti ya Kirinyaga bado tuko na shida. Kuna chama cha ushirika ambacho kinaitwa Rwama ambacho kilikuwa na Rwama SACCO. Tayari chama hiki kimefunga milango na pesa za wakulima. Kuna chama kingine kinachoitwa Mwireri ... view
  • 25 Sep 2024 in Senate: kupelekea wale wakiritimba na kahawa ya wakulima inapotea. Nasema hivyo nikijua mfano mzuri ni Chama cha Ushirika cha Kibirigi. Kwa hivyo, hii sheria tuliyo nayo sasa, tukiibana ili wakora wasipate mahali pa kupenya, tutaweza kusaidia mkulima. Vile vile, kuna utepetevu. Nawashukuru wale wanaohusika na vyama vya ushirika katika Kaunti ya Kirinyaga. Kuna jamaa mzuri sana pale anayeitwa Haliam, anayefanya kazi nzuri katika vyama vya ushirika. Ndio pia naunga mkono Hoja ya Sen. Omogeni ya kugatua mambo mengi katika vyama vya ushirika ili tusaidie wakazi. Ni lazima tuhakikishe kuna wafanyikazi wa kutosha wanao shughulikia mambo na sheria inafuatwa na wale waliochaguliwa ... view
  • 25 Sep 2024 in Senate: On a point of information, Mr. Temporary Speaker, Sir. view
  • 25 Sep 2024 in Senate: Thank you very much, the Deputy Party Leader of the Orange Democratic Movement (ODM). It is a privilege to inform you. The Bill on cooperatives is already in the Second Reading in the National Assembly. It has already reached there. Thank you. view
  • 24 Sep 2024 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. I rise pursuant to Standing Order 56 (1)(b) of the Senate Standing Orders to make a statement relating to activities of the Standing Committee of Agriculture, Livestock and Fisheries during the second part of that session covering the period between April to August 2024. During the period under review, the committee held a total of 19 sitting, during which it considered one legislative agenda, three Bills, six Statements, two Petitions and one inquiry. In the reporting period, pursuant to Standing Order No.131(1), the committee considered the Legislative Proposal; the Agricultural Produce Minimum Guarantee The electronic ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus