1 Nov 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, Serikali hii inasikitisha. Inalia tu vile inavyolia inapofika wakati wa kupambana na ufisadi, ingawa hakuna chochote kinachotendeka. Waziri Msaidizi amesema wazi kwamba anajua viwanja vya shule vimenyakuliwa na watu binafsi na analia na Serikali. Ni lini Serikali itakuwa na meno?
view
1 Nov 2006 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nitaanza kuzungumza nikimpongeza Mbunge wa Bahari kwa kutambua umuhimu wa kulishughulikia swala la maskwota nchini, na haswa kuzingatia shida tuliyo nayo mkoani Pwani ya watu wetu walionyanganywa ardhi yao na kugandamizwa kuanzia nyakati za ukoloni wa Mwarabu na ukoloni wa Mzungu, hadi wakati huu ambapo ukoloni mambo leo unaendelea. Hii ni Hoja muhimu sana. Ninashukuru kwamba Hoja hii imeletwa Bungeni wakati ambao Serikali pia imependekeza Sera mwafaka kuhusu ardhi ambayo inaendelea kutayarishwa na Wizara ya Ardhi. Sera hiyo inaambatana na Hoja hii. Ningependa kusema kwamba wale tunaoiunga mkono Hoja hii tutaendelea kuiunga mkono ...
view
26 Oct 2006 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Spika. Imekuwa kawaida kwa Mawaziri kuja hapa na kusoma majibu ambayo yameandikwa na maofisa wa Serikali bila ya kuhakikisha kama ni ya kweli. Hata pesa nyingi za umma zimepotelea Wundanyi. Wakati Wabunge wanapowaeleza Mawaziri kuwa miradi hii haipo, wanabishana, ni kama wameiona. Bunge hili litasaidiaje kulinda hela za umma ambazo zinapotea namna hiyo?
view
26 Oct 2006 in National Assembly:
Bw. Spika, ningetaka kujua kama Serikali inazingatia masharti ya wafadhili ya kuwafuta wafanyakazi. Je, sera za Serikali juu ya wafanyakazi ni zile za wafadhili? Hii ndio maana Serikali inapunguza idadi ya wafanyakazi kila siku.
view
26 Oct 2006 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Spika. Umesema kwamba wachache pia wapewe nafasi wazungumze. Mimi nilikuja hapa kupitia chama cha FORD(P). Wenzangu wakaniacha wakaenda upande ule wa Serikali. Jambo ambalo naomba kusema---
view
26 Oct 2006 in National Assembly:
Bw. Spika, kazi tunayoifanya sasa, ya kuchagua Wabunge watakaotuwakilisha katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni nzito mno. Naijua kwa sababu niko katika Kamati ya Mashauri ya Nchi za Nje na Ulinzi. Tumeshughulikia sana mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mimi sitazungumza mengi. Lakini jambo ambalo naomba kusema ni kwamba, pamoja na sheria zote, ziwe za kidemokrasia au la, Serikali ina jukumu muhimu la kuhakikisha kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki inalindwa na kwamba, Wabunge wanaoenda huko wana baraka za watu wote wa Afrika Mashariki. Tukiangalia vyama vyote, hasa chetu cha FORD(P), watu wote wanatoka sehemu moja. Hiyo haionyeshi haki ...
view
26 Oct 2006 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Spika. Naomba viongozi wote wa vyama wafikirie zaidi kuhusu nchi yetu. Tusifikirie maslahi ya muda mfupi ambayo yanaweza kuvunja nchi yetu kupitia ukabila. Hilo ni jambo muhimu kwa wananchi wote wa Afrika Mashariki.
view
25 Oct 2006 in National Assembly:
aliuliza Waziri wa Elimu ni lini walimu wa Wundanyi na Taveta wataanza kulipwa marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu kama wenzao wa Voi na Mwatate.
view
25 Oct 2006 in National Assembly:
alimuuliza Waziri wa Elimu ni lini walimu wa Wundanyi na Taveta wataanza kulipwa marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu kama wenzao wa Voi na Mwatate.
view
25 Oct 2006 in National Assembly:
Bw. Spika, hilo jibu ni la kusikitisha kabisa, hasa kwa walimu wa Wilaya ya Taita-Taveta. Ni jibu ambalo lina lengo la kuendeleza vurugu na kuvunja motisha wa kufundisha kwa walimu wa Taita-Taveta. Waziri Msaidizi amesema kuwa tume ya kuwaajiri walimu ilifanya utafiti na ikatoa ripoti yake. Tarafa ya Taveta ndiyo yenye hali ngumu zaidi katika Wilaya ya Taita Taveta. Tarafa ya Wundanyi inapakana na tarafa za Mbololo, Mwatate na Voi, ambako walimu wanapata pesa za kufanya kazi katika mazingira magumu. Shule kama Kishushe, Ngongodinyi, Sagenyi, Sirienyi na Mwoloko ziko katika mazingira magumu zaidi. Je, ni vigezo gani vilitumiwa na Wizara ...
view