Naomi Shaban

Parties & Coalitions

Full name

Naomi Namsi Shaban

Born

9th September 1963

Post

P.O. Box 73855 - 00200 Nairobi

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

namsi-ns@yahoo.com

Telephone

0722814412

Telephone

0202215245

All parliamentary appearances

Entries 111 to 120 of 1513.

  • 24 Jul 2019 in National Assembly: Ukweli ni kwamba sioni kama Ripoti hii iko kikamilifu hapa mbele ya Bunge la Kitaifa. Mwenye Kiti na Wabunge wa Kamati wamejaribu sana kuangalia jambo hili. Ninajua wanaangalia kuwa Wizara inayosimamia masuala ya wanajeshi inataka kufanya hii shughuli na hivyo basi wana hiyo haraka. Wahenga wanasema, “Haraka haraka haina baraka.” Hivyo basi, ninapendekeza warudi wahusishe wahusika na washika dau wote na bila shaka, watapata mwelekeo bora. view
  • 24 Jul 2019 in National Assembly: Ninapendekeza kuwa suala hili lirudishwe kwa Kamati na wahusishe watu hao ili waweze kupata mwelekeo ambao utafurahisha kila mtu. view
  • 24 Jul 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 27 Jun 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kwanza kutoa shukrani kwa Kamati ya kusimamia masuala ya afya hapa Bungeni ambayo inasimamiwa na Mhe. Sabina Chege kama mwenyekiti kwa kuleta Ripoti hii ambayo ni ya muhimu sana. Tangu Kenya ipate Uhuru mwaka wa 1963, hadi kufikia mwaka wa 2010 wakati tulipata Katiba mpya, masuala ya afya yalipatiwa kipaombele kwenye Katiba yetu na ndani ya Katiba kulitajwa umuhimu wa kila Mkenya kuwa na haki ya kupata huduma ya afya kiwango cha kumwezesha kuishi vile anavyostahili. Ripoti hii ambayo imetengenezwa na Kamati ya Afya ni muhimu sana maana inagusia hospitali za kitaifa ... view
  • 24 Apr 2019 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nami nijiunge na wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa Hotuba yake aliyotoa hivi jusi. view
  • 24 Apr 2019 in National Assembly: Ufisadi ni ugonjwa mgumu sana na mbovu kushinda saratani, kwa maana ni ugonjwa ambao utamaliza nchi yetu kama hatutasikiza vile Mheshimiwa Rais amesema. Amezungumzia sana kuwa kuna umuhimu wa kupigana na ufisadi maanake ni janga ambalo linatumaliza sisi sote na pia mwananchi. view
  • 24 Apr 2019 in National Assembly: Janga hili la ufisadi ni janga ambalo linahitaji Wakenya wote waungane na Mheshimiwa Rais tuwe kama jeshi lake kuweza kupigana na huu ufisadi. Kina mama wakienda kujifungua hospitalini wanakosa dawa, ama vifaa vya kuwasaidia na mama anapata dhiki ya kupata mtoto afariki au yeye apate matatizo na kufariki. view
  • 24 Apr 2019 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, ufisadi unatumalizia wananchi wetu, na kutuletea balaa hapa nchini. Sio wote kule mashinani wanaweza kwenda kwa hospitali ambazo ni za kibinafsi. Watu wengi huenda hospitali za umma ili kuweza kuwezeshwa. Hata Mhe. Rais aliposema anazungumzia ajenda zake nne, moja ni kuhusu habari za kuwawezesha Wakenya kupata huduma ya afya kwa njia inayofaa na mwafaka. view
  • 24 Apr 2019 in National Assembly: Kule mashinani watu hutembea kilomita nyingi kutafuta maji. Pesa zinazofujwa kwenye ufisadi, zinafanya wananchi kuteseka, na kukosa maji ya kutumia. Kama inavyosemekana maji ni uhai. Maswala mengi na haswa sakata kubwa zilizoko ni kuhusu maswala ya kuhusiana na maji. Ufisadi hauwezi kuendeleza nchi na itakuwa sababu kubwa ya nchi hii kudidimia chini, kama hatutamsikiliza Mhe. Rais anavyosema. view
  • 24 Apr 2019 in National Assembly: Ningependa sana kumpongeza Raisi haswa kwenye maswala ya kimaendeleo, reli ya kisasa inavyotutoa Mombasa ikitufikisha hapa, sasa hivi inaelekea kumalizika kuelekea Naivasha halafu kuendelea mbele. Tunajua kwamba ameenda nchi ya Uchina kuhakikisha ya kwamba ameweza kumalizia maswala ya kupata fedha za kumalizia kazi hii. Wakenya wengi wana kilio, lakini dawa ya kilio chenyewe ni moja tu, kuhakikisha kuwa ajenda hizo nne za Raisi zinaweza kutimizwa na yeye kabla hajafika kustaafu mwaka wa 2022. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus