Naomi Shaban

Parties & Coalitions

Full name

Naomi Namsi Shaban

Born

9th September 1963

Post

P.O. Box 73855 - 00200 Nairobi

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

namsi-ns@yahoo.com

Telephone

0722814412

Telephone

0202215245

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 1513.

  • 18 Feb 2021 in National Assembly: mimea ambayo mazao yake hayawezi kukaa kwa muda mrefu. Kwa mfano, nataka kuzungumzia ndizi ambazo zinatoka kule kwetu. Utakuta kuwa ndizi hazikai kwa muda mrefu. Ni kati ya ile mimea ambayo tunajua itakuwa na matatizo. Tunajua mahindi yanaweza kukaa kwa muda lakini juu ya hiyo, mahindi pia lazima yapatiwe bei inayostahili. Vilevile, Serikali inafaa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa taaluma ya kilimo wanaweza kuwasaidia wakulima kupata haki yao. Ukienda nchi za nje, utakuta kuwa kahawa na chai nzuri zaidi zinazotumika kule ni zile za kutoka Kenya. Saa zingine wanachanganya kahawa yetu na zingine, lakini zaidi sana kahawa ya Kenya inasifika kila ... view
  • 26 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii pia nami niweze kuchangia suala hili la kurekebisha Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Dennitah Ghati. Kwanza, ni muhimu tufahamu kuwa binadamu haishi kuumbika… The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 26 Nov 2020 in National Assembly: Yes, I am getting there. Bi. Naibu Spika wa Muda, nimeanza kwa kutaja kuwa aliyeleta Hoja hii amefanya jambo muhimu sana. Ningetaka kuunga mkono Mhe. Daktari James Nyikal ambaye tuliweza kufanya kazi pamoja na walemavu hapa nchini. Sioni aibu kusema kuwa alikuwa Katibu wangu wa Kudumu na alipigania swala la walemavu vilivyo. Ukweli ni kwamba walemavu wanateseka hapa nchini. Na katika hali ya mateso yale, kuna umuhimu wa sisi kujua kuwa Kipengele cha 27 cha Katiba ya Kenya kinasema tusibaguane. Tusibague mtu kwa misingi ya ulemavu, dini, kabila au rangi. Haya yote yametajwa katika Katiba yetu. Hivyo basi, ninakubaliana na ... view
  • 26 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii nami pia nizungumzie swala hili nyeti. Hii ni Hoja inayoleta taarifa kuhusu makadirio ya pesa iliyopeanwa kutoka wizara tofauti tofauti. Vile vile, Kamati ya Bunge itueleze kuhusika kwenye makadirio ya kuhakikisha kuwa zile pesa tulizokuwa tumekadiria tuliweza kuzibadilisha zitumike kwenye janga hili. Sio siri kwamba kuna utukutu mwingi katika nchi hii. Wafanyibiashara wasiokuwa na nia nzuri walitumia janga hili kujinufaisha. Kamati ya Bunge inayosimamia masuala ya afya imezungumza kinaganaga juu ya matatizo yaliyoko, haswa, zile pesa zilizofujwa badala ya kutumika vile ilivyotakikana. Ni dhahiri kwamba wale waliofanya biashara na KEMSA ... view
  • 26 Nov 2020 in National Assembly: akija hospitali akose kivuta pumzi, hata kama haugui Coronavirus, hawezi kusaidika maanake hawawezi kupata njia ya kupata hewa ya haraka ili atibiwe. Wakenya wako na shida kubwa sana. Ninashangaa kuwa mtu anaweza kulala usingizi akijua amechukua pesa amezifuja kwa ufisadi na kuweka mfukoni na kulala akifikiri ametajirika ama akitarajia kuwa wanawe wanatakikana kuishi vizuri kuliko Wakenya wengine. Ni jambo la aibu na la kusikitisha. Ninatumai kufikia sasa watu waliohusika wangekuwa wakichezea jela, kama kweli kuna vita dhidi ya ufisadi humu nchini. Ni laana na dhambi. Nilimuona aliyekuwa Katibu wa Kudumu tuliyefanya kazi naye, Dr. Nyikal, na ambaye pia ni daktari, ... view
  • 24 Sep 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuongea juu ya mwandishi mkuu wa vyama vya kisiasa hapa nchini. Kwanza, nimefurahi kwa sababu Mhe. Rais ametuletea majina hapa. Alikuwa ameleta majina mawili ya wanawake na mawili ya wamaume. Hivyo, nampongeza sana Mhe. Rais kwa kuwa aliona kuwe na usawa katika ugawaji wa kazi hii ambayo iko katika afisi ya watu wanne. view
  • 24 Sep 2020 in National Assembly: Mhe. Spika tuko katikati ya maswala ya jinsia na nataka kumpogeza Rais kwa kufanya huo uamuzi. Kwa ufupi, ningependa kusema katika hao wote wane, Ann Nderitu na Florence Birya ni akina dada ambao nawafahamu. Nafahamu kazi zao na kwa muda mrefu, niko na imani kuwa wataweza kazi hii. view
  • 24 Sep 2020 in National Assembly: Kulingana na kubobea kwa kazi ya Ann Nderitu ni sawa amepatiwa kuwa mwandishi mkuu wa kusimamia vyama vya kisiasa hapa nchini. Florence Birya pia namfahamu na najua anaweza kazi na bila shaka atafanya kazi nzuri. Kwa uchache tu, ningependa kuzungumzia juu ya kijana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 24 Sep 2020 in National Assembly: huyu. Kusema kweli, nafikiria Mhe. Rais alikuwa ameamua kupeana kazi kwa mlemavu na pia awe kijana. view
  • 24 Sep 2020 in National Assembly: Ningependa kusema kuwa kijana huyu ambaye ni mlemavu, Mhe. Rais alimchagua kwa nia safi. Isipokua ukiangalia sheria vile ilivyo ni kuwa hakutoshea na hakubobea kuwa kwenye nafasi hiyo. Kuna umuhimu kuwa kijana huanza kwa kutambaa ndio aweze kukimbia. Mimi ningependelea kama walemavu na jamii ndogo kama Wakuria pia wangepatiwa nafasi. Hii ni kwa sababu ni haki yao kupatiwa nafasi. Lakini isiwe mtu anapewa kazi kama hajafanya kazi kwa muda unaofaa ama mrefu. Pia, kwa umri wake, kazi kama hii ni nzito si nyepesi. Nakubaliana na taarifa hii iliyotolewa na kamati hii kuwa hawa watatu wapatiwe kazi na huyu mmoja anzishwe ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus