9 May 2017 in National Assembly:
He wants to make noise.
view
9 May 2017 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. Nashukuru. Imeeleweka na inajulikana ni hivyo. Lakini ninakubaliana na vile ulivyomesema. I respect the Chair. Ukishatoa mwelekeo, ni lazima tuufuate. Ndiyo ninamshauri mwenzangu awache kuzungumzia siasa za Bahati. Tuzungumzie mambo ambayo yako mbele yetu. Ndugu yangu, tuheshimiane. Tuangalie tutafanya nini ili tuweze kuiendeleza nchi hii tukiwa pamoja. Ahsante sana.
view
22 Feb 2017 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nashukuru kwa kupatiwa nafasi hii ili niunge mkono huu Mswada. Naungana na Wabunge wenzangu ambao wanauunga mkono. Wakati umefika tuweze kuzungumza mambo ambayo yataweza kusaidia wale waliotuchagua. Wauguzi ndiyo wanaohudumia watu sasa katika hospitali nyingi kwa sababu hakuna madaktari. Huko kwetu mashambani, utapata wauguzi wanahudumia wagonjwa. Hao watu ni muhimu sana na wanafanya kazi nzuri sana. Kwa hivyo, naunga wengine mkono na kusema kwamba jambo hili linahitaji Bunge hili, kabla hatujaondoka, tuwe tumelitatua ili watu wetu waweze kuhudumiwa kwa njia ambayo inatakikana. Nimewasikia Wabunge wengi wakiongea. Nawaunga mkono kwamba kuna mambo nyeti na ...
view
22 Feb 2017 in National Assembly:
kwa NG-CDF, ikatupatia nafasi ya kujenga nyumba za wauuguzi ili waweze kuwahudumia wagonjwa wakiwa karibu. Mpaka sasa, kuna shida na nyumba ambazo tuliwajengea wauguzi na madaktari. Huu ndio wakati wa kuangalia ni watu wapi watakuwa wakiishi karibu na wananchi ili kuwahudumia. Wauguzi ndio wanaweza kuwahudumia watu wetu hata kwa kuwatembelea manyumbani na mitaani. Kwa hivyo, litakuwa jambo muhimu sana ikiwa Mswada huu utapitishwa haraka iwezekanavyo kwa sababu naona Wabunge wote wanakubaliana nao. Ni jambo ambalo litabadilisha nchi yetu. Watu wetu ni wagonjwa na wana shida nyingi. Juzi nilifanya medicalcamp na niliona watu wana shida nyingi sana. Kwa hivyo, lazima tuhakikishe ...
view
22 Feb 2017 in National Assembly:
Yes, Hon. Temporary Deputy Speaker. I wanted to alert you that I do not see the Opposition in this House today. I do not know what is happening. They are very important. I cannot see anyone of them. Does that mean that they are not interested in this Bill?
view
7 Feb 2017 in National Assembly:
Ninashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Pili, ningetaka kumpongeza Mhe. Okoth kwa kuuleta Mswada huu wakati ufaao. Haswa, kwa ujuzi ninao, kwa mambo nimepitia, Mswada huu unahitajika sana na ni muhimu sana sisi kama Wabunge tuuangalie kwa makini. Mara nyingi, Miswada huja hapa Bungeni na tunaikimbiza bila kuangalia matokeo yake. Njia za kuwaadhibu washukiwa kama wameshikwa na polisi zimezidi kila mahali. Polisi wanatumia njia nyingi sana. Matusi ambayo wananchi ambao tunaongoza wanatusiwa ni adhabu kubwa sana kabla hawajafikishwa kortini. Wanatusiwa vibaya sana. Polisi wanawatukana wananchi kwa majina ya waheshimiwa na watu wengine ...
view
7 Feb 2017 in National Assembly:
kwa mtu ambaye anaheshimika. Kama Mheshimiwa ataadhibiwa na matusi kama hayo, mwananchi wa kawaida, wale tunaongoza, hali yao itakuwa namna gani? Pia, kunyang’anya watu mali yao baada ya kushikwa na kuingizwa seli ni kuadhibu mtu kabla hajafika kortini. Unakuta hata njia ya kupea hawa watu chakula, wengi wanaadhibiwa kwa majina ambayo hata siwezi kutaja hapa kwa sababu lugha hiyo ni mbaya kwa Mbunge kutaja. Lakini unakuta wanaadhibiwa vibaya sana. Hata rumande zingine ukiingia hali ni mbaya sana. Kwa hivyo, lazima tuangaliie mikakati. Nafasi imekuja ya sisi tuangalie huu mjadala na tuangalie ni kitu gani tutaweka kisheria ili kulainisha vifungo ambavyo ...
view
2 Feb 2017 in National Assembly:
Nashukuru, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu lakini pia tunayo mambo nyeti ambayo tunahitaji kuangalia, sisi kama Wabunge. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
2 Feb 2017 in National Assembly:
Kwanza, tunajadiliana mambo ambayo hatuna uwezo kuyahusu. Kila mara tunalaumu Serikali ilhali sisi ndio Serikali.Tukiwa hapa, tuna mikakati ya kisheria ya kumwita Waziri yeyote ili kuchunguza mambo ambayo tunataka yawe ni kuhusu fedha ama mabadiliko ambayo tunataka. Lakini ninaona tunalia tu bila kuona tuna uwezo wa kufanya hilo jambo. Nakubali kuna mambo nyeti ambayo tunayazungumzia hasa kuhusu serikali za kaunti. Kuna kaunti zimefanya vizuri sana na kuna nyingine ambazo zina shida. Hata hivyo, tuna uwezo wa sheria kuchunguza ni nani amekosa kufanya kazi yake. Ndugu zetu katika Seneti, mimi naona wana shida. Hii ni kwa sababu wakipendekeza na kupitisha kwamba ...
view
2 Feb 2017 in National Assembly:
Kwa sababu nazungumzia jambo nyeti. Itakuwa bora tukipitisha sheria kuwa pesa zote zinazokusanywa katika makaunti ziwe zikiwekwa na Serikali mahali fulani. Hizo pesa zitakuwa ni zao tu lakini tujue zile wataongezewa na zile wamekusanya ni ngapi. Bila kufanya hivyo, tutazungumza mengi na tutaendelea kuwa na shida kubwa. Kwa hivyo, ninaunga mkono huu Mswada lakini tuweke mikakati ya kutosha ili tuweze kujua pesa ambazo zinatozwa ushuru ni ngapi. Tunasikia kwamba hata zingine haziwekwi kwenye akaunti ya kaunti. Hizo pesa zinapatiwa mawakala ambao wanakusanya hizo pesa. Baadaye hizo pesa hazirudi kwa wananchi hata kidogo. Hayo ndiyo maoni yangu na ninashukuru kwa kuniongezea ...
view