Rashid Juma Bedzimba

Parties & Coalitions

Email

bedzimbar@yahoo.com

Telephone

0720679612

Telephone

0733679612

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 62.

  • 14 Apr 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuchangia Hotuba ya Rais lakini nashukuru umenipatia nafasi. Nasema shukrani. view
  • 14 Apr 2016 in National Assembly: Kwanza natoa shukrani zangu kwa Mhe. Rais kwa kusema tusimame ndani ya Bunge kama heshima kwa wale wanajeshi wetu waliopoteza maisha yao huko Somalia. Hilo jambo lilinitia nguvu. Niliona kwamba Mhe. Rais aliguzwa na ana imani na wanajeshi wetu. view
  • 14 Apr 2016 in National Assembly: Kwa sababu yeye ni Amiri Mkuu wa Majeshi, tulitarajia kuwa katika Hotuba yake kuhusu suala la wanajeshi wetu, atatangaza wazi idadi ya wanajeshi waliopoteza maisha yao nchini Somalia, idadi ya miili iliyorudi nchini na kuzikwa na wangapi hawajulikani waliko, lakini hakulitaja jambo hilo. Kama Amiri Mkuu wa Majeshi, tungetaka atueleze maana ya wanajeshi wetu kukaa huko Somalia, na ikiwa watakaa kule, watarudi lini. Ikiwa wataishi huko The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 14 Apr 2016 in National Assembly: muda mrefu basi angetueleza. Angetupa kiwango cha siku watakazo kuwa kule. Kwa maoni yangu, naona kuwa tunahatarisha wanajeshi wetu kwa sababu wanapambana na adui wasiemjua. Wanajeshi wetu ni hodari, wana silaha, uwezo na mafunzo mazuri lakini shida ni kuwa hawajui adui wanaepambana naye. Ikiwa tutaendelea kuwaacha wanajeshi wetu Somalia basi wataendelea kupoteza maisha yao. Pendekezo letu ni kuwa Rais angesema kuwa wanajeshi wetu watoke huko tuje tulinde taifa na mipaka yetu kuhakikisha kuwa adui hatatuingilia tena. Ni sawa kwenda kwa mara ya kwanza, kwenda kuweka sawa nchi jirani lakini kwa sasa ni vyema warudi. Si vibaya kwa sababu hata Jeshi ... view
  • 23 Mar 2016 in National Assembly: Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ili pia nipenyeze sauti yangu kwenye Hoja hii. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii. Karibuni, kulikuwa na matokeo yaliyoonyesha kuwa Wakenya wengi wanatumia pesa nyingi kwa matibabu ya saratani ng’ambo. Ni vyema Serikali itilie maanani jambo hili ili iweze kujenga sehemu ambazo saratani itatibiwa katika sehemu zote za ugatuzi. Hata tukiwaelimisha watu kwamba wapimwe mapema wajue kama wana saratani ili watibiwe, wengi wanaogopa kupimwa kwa sababu wana hakika kwamba hakuna pahali watapata matibabu. Ni vyema Serikali itenge fedha na ihakikishe kwamba kila eneo la ugatuzi lina vifaa maalum vya saratani ili ... view
  • 23 Mar 2016 in National Assembly: Nakushukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda na kila anayesimama kuunga mkono Hoja hii. Naunga mkono Hoja hii kwa dhati ili Serikali iwe tayari kutenga fedha ili wagonjwa wanaogua saratani watibiwe hapa kwetu na kwa njia rahisi. view
  • 23 Mar 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 16 Mar 2016 in National Assembly: Sioni kama vile hii mambo inavyoendelea ni sawa. Sisi tumefinya tukitaka kuzungumza--- view
  • 28 Oct 2015 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Ninakushukuru sana kwani unapokuja ninapata fursa ya kuzungumza. Mara nyingine huwa nabofya mpaka nasinzia. Ninasimama hapa kuunga mkono Kamati ya Usalama wa Taifa kwa Ripoti ambayo imeleta. Ni kweli kwamba inakuwa vigumu kwa vikao vya tume kuendelea kwa sababu ya idadi ya wanachama wao. Ninachukua fursa hii kusema kwamba ndugu yetu Maj. (Rtd.) Shadrack Muiu alikuwa mzalendo aliyejitolea kwa taifa hili. Juzi, tulisherehekea siku ya Mashujaa. Siku zijazo hata yeye atakuja kusherehekewa kama shujaa kwa sababu alijitolea mhanga kwa taifa ambalo lilikuwa linakwenda kwenye mapinduzi. Kwa sasa, inakuwa vigumu ... view
  • 1 Oct 2015 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Hoja hii muhimu. Nimesimama kupinga Hoja hii kwa sababu ukiangalia mataifa jirani kama Uganda na Rwanda hayana muda maalum wa viongozi wa mataifa hayo kuhudumu. Sisi tuna miaka mitano maalum lakini wao hawana. Ni hatari sana kuungana nao kijeshi ama kiusalama. Wanaweza kutuambukiza ugonjwa huo huku kwetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus