Rashid Juma Bedzimba

Parties & Coalitions

Email

bedzimbar@yahoo.com

Telephone

0720679612

Telephone

0733679612

All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 62.

  • 1 Oct 2015 in National Assembly: Ukiangalia viongozi wa upinzani katika mataifa hayo, wanaishi jela na wengine kupoteza maisha yao. Hapa kwetu tuna demokrasia. Ni vyema tuungane na wao kiuchumi lakini tusiungane nao kiusalama. Kwa hivyo, mimi nimesimama hapa kupinga Hoja hii kwa sababu taifa letu lina demokrasia. Sitaki kuona mataifa mengine yakiingilia kwetu ili tufuate mfumo wao. Je ikiwa tumeungana nao katika usalama na kuwe na matatizo hapa wakati wa uchaguzi, hilo jeshi ambalo litakuwako litatumika kuja kuharibu kabisa taifa letu ambalo ni zuri, huru na liko na amani? Kwa hivyo, nimesimama kupinga Hoja hili. Naomba Wabunge wenzangu watafakari kwa makini jambo hili kabla ya ... view
  • 30 Sep 2015 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ya kuzungumzia suala hili la ardhi ambalo ndilo lenye utata kwa taifa nzima. Nimeona ni vyema sana nipenyeze sauti yangu katika suala hilo. Kwanza, ninakubaliana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi kwamba ni lazima tuheshimu hati miliki. Ni vyema sana kuziheshimu. Lakini vilevile tuangalie uzito ulioko kuhusu watu wetu kwa sababu hao maskwota walioingia katika shamba hilo, ni watu ambao hawana makao na ndiyo sababu wakaingia katika lile shamba kujiwekea makao. Ikiwa waliingia kuuza, hapo ni makosa. Lakini kama walienda kwa makao yao, ni kwamba walikuwa na utata. Vile vile ... view
  • 30 Sep 2015 in National Assembly: hizo huwa lile shamba limekaa wazi, halilimwi na hakuna shughuli inafanyika. Inavutia mtu mwingine ambaye anapata shida na pale pako wazi, panakaa nyoka na wanyama. Hii ndiyo sababu wanaenda pale. Kwa upande wangu, ningeomba Kamati ya Ardhi ishughulikie suala hili. Inafaa Serikali inunue lile shamba ili wale walio pale wasiondolewe. Tatizo hili lipo katika upande wa Kisauni. Wengi wameingia katika mashamba ambayo yako wazi. Kama wale watu wangekuwa wameyatumia mashamba yale hata kwa kulima na kuleta mapato, hakuna mtu angeingia. Lakini kwa sababu shamba halina mtu, lipo wazi na panaishi nyoka ambao wanakaribia zile nyumba, wananchi wanaingia pale kujisaidia wenyewe. ... view
  • 30 Sep 2015 in National Assembly: Naiunga mkono lakini hilo ndio suala ambalo ninalitilia uzito. Asante. view
  • 25 Mar 2015 in National Assembly: Hoja ya nidhamu, mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 25 Mar 2015 in National Assembly: Ahsante, mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kwa Hoja ya nidhamu, nikijua kwamba una uwezo wa kuamua ni nani anafaa kuongea. Ninaona kwamba kuna upendeleo humu ndani. Nimekuja Bungeni mbele ya mhe. Ramadhani lakini amepewa nafasi nami bado sijaongea. Kwa hivyo, ninaomba kwamba iwapo kuna Waheshimiwa wengine ambao hawaruhusiwi kuzungumza tuambiwe tujue ndiyo tukae mpaka muda uishe twende zetu. Ninaomba majina ya wanaongojea kuzungumzwa yawekwe mahali ambapo tutayaona ndiyo kila mtu ajue ni nani anafuata mwingine. view
  • 25 Mar 2015 in National Assembly: Ahsante. view
  • 25 Mar 2015 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nashukuru kupata fursa hii. Waswahili wanasema “chelewa ufike”. Nimefika sasa. Lugha ya Kiswahili si lugha tu ya taifa, ni lugha rasmi ya taifa la Kenya. Kiswahili kimeangaziwa sana kama ni lugha ya watu maskini ingawa si kweli bali ni unyanyasaji kwa wale wanaotumia Kiswahili. Kutafsiri sheria za Kenya kwa lugha ya Kiswahili kutawawezesha wengi kuelewa ikiwa waliosoma na hata ambao hawakusoma. Ile lugha inayotumika ya Kiingereza ni ya ndani sana ambayo si rahisi mtu kuielewa. Kwa hivyo, ni vyema sana sheria hii itafsiriwe kwa Kiswahili. Viongozi wote ambao wako hapa, karibu asilimia 90, ... view
  • 25 Mar 2015 in National Assembly: Kwa hivyo, mimi naunga mkono Hoja hii na kumpongeza mheshimiwa Joyce Lay kwa kuileta wakati huu unaofaa. Ahsante sana. view
  • 19 Nov 2014 in National Assembly: Nashukuru, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii kutoa rambirambi zangu. Kwa niaba ya watu wa Kisauni nasema pole ndugu, jamaa na familia ya Senator Kajwang’. Vilevile, nitachukua fursa hii kusema pole kwa familia nne zilizouawa juzi katika eneo Bunge la Kisauni kupitia mikono ya majambazi. Tunawaombea roho zao zilale mahali pema peponi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus