Ruweida Mohamed Obo

Parties & Coalitions

Born

1978

Telephone

0722222784

All parliamentary appearances

Entries 361 to 370 of 439.

  • 4 Oct 2018 in National Assembly: which is 297 kilometers. This leaves a vast stretch along the border that is unmanned and no record of activities happening in the various border crossings. The Committee recommended the removal of a barrier erected at the entrance of the Isibania Border Post Facility by the Migori County Government. The one-stop border point authorities should ensure multi-stakeholder collaboration and partnership amongst border communities and other relevant agencies. The Ministry of EAC and Northern Corridor Development should fast-track efforts of harmonised policies in order to facilitate cross border trade within the region. The governments of Kenya and United Republic of Tanzania ... view
  • 4 Oct 2018 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mwanzo, ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenye Kiti wa hii Kamati. Mimi ni naibu wake. Pia, ningependa kuchukua nafasi hii kushukuru Kamati kwa jumla kwa kazi nzuri tuliyoifanya. Pia, ningependa kuwashukuru Waheshimiwa wote waliochangia. Sisi tumesoma kutoka kwa vile wamechangia. view
  • 4 Oct 2018 in National Assembly: Katika upande wa wafanyikazi, ni kweli tuliona kulikuwa na hiyo changamoto Isibania. Wenyeji hawajapewa hizo nafasi. Tuliita shirika ambalo linahusika na tukapeana mwelekeo wetu kwamba njia ambayo wanatumia wakiweka matangazo haifiki kule mashinani. Kwa hivyo, tukasema ni vizuri waweke hayo matangazo hata pale kwa border . Pia, ni vizuri katika zile kandarasi zao wakipeana, waweke kama maagizo kwamba ni vizuri wawapatie wale wenyeji hizo nafasi. view
  • 4 Oct 2018 in National Assembly: Pia, Waheshimiwa wamezungumza kuhusu zile border post zingine ambazo hatujazifikia au hazijafungulia. Kama Kamati tutakaa tuziangazie zaidi. view
  • 4 Oct 2018 in National Assembly: Lamu, tuna changamoto kule Kiunga. Tulijaribu kwenda huko lakini hatukuruhusiwa kufika. Tulifika Lamu na ikabidi tufanyie mikutano yetu huko. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 4 Oct 2018 in National Assembly: Naomba na nasisitiza kwa Waheshimiwa Wabunge tuwe na moyo wa kuleta majirani wetu pamoja. Hiyo haimaanishi tuwe wakarimu sana. Lakini nawahakikishia kuwa ukarimu wetu unatufaidi. Wenzetu wataendelea kuona ukarimu wetu na faida tunayopata na wao watakuwa wakarimu kama sisi. Lau kama hawatakuwa wakarimu, hawatafaidika. view
  • 4 Oct 2018 in National Assembly: Asante sana. Shukrani. view
  • 3 Oct 2018 in National Assembly: Ahsante, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Ningependa mwanzo kuchukua nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Oluoch The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 3 Oct 2018 in National Assembly: kwa Hoja hii. Ni kweli vijana wetu wengi hawajaajiriwa. Kulingana na utafiti wa United Nations Development Programme (UNDP), asilimia 39 ya vijana wa Kenya hawajaajiriwa. Ukipima, hicho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na majirani wetu kama Tanzania, Uganda na wengine. Nawakilisha Kaunti ya Lamu. Kenya National Bureau of Statistics walisema asilimia 68 ya vijana wetu hawajaajiriwa. Ni kiwango kikubwa sana. Kutoajiriwa huleta uhalifu. Kwa mfano, utaona ya kwamba kaunti nyingi ambazo watu hawajaajiriwa, uhalifu uko juu zaidi. Mfano ni Lamu ambapo uhalifu uko juu zaidi. Vijana wetu wameingia kwenye mihadarati sana. Hii inachangia matatizo zaidi. Kwa mfano, ugonjwa wa ukimwi umekuwa ... view
  • 3 Oct 2018 in National Assembly: Serikali pia kwa mipango yake saa zingine husababisha watu kukosa kazi zaidi. Kwa mfano, katika Kaunti ya Lamu, wakati Lamu Port -South Sudan-Ethiopia Transport (LAPSSET) Corridor Project ilipoanza, wavuvi wengi hawangeweza kwenda baharini. Kwa hivyo, imechangia ukosefu wa ajira. Kuna kiwanda ambacho kinataka kuwekwa cha makaa. Sehemu hiyo ilikuwa na wakulima ambao walikuwa wamekaa hapo miaka mitatu wakingojea walipwe. Hawalimi sasa. Hii imeleta ukosefu wa ajira na wengi ni vijana. Pia kuna mpangilio wa Serikali uliyowekwa wa kutokata mikoko. Hii imechangia pakubwa ukosefu wa ajira kwa familia 3,000 katika Kaunti ya Lamu. Mipango hii ambayo iko katika Hoja hii itasaidia ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus