Ruweida Mohamed Obo

Parties & Coalitions

Born

1978

Telephone

0722222784

All parliamentary appearances

Entries 421 to 430 of 439.

  • 14 Feb 2018 in National Assembly: Tuheshimiane. Mimi niko na bwana. Sikuja hapa kutafuta wanaume. view
  • 14 Feb 2018 in National Assembly: . Sikuja hapa kupendwa. Unaniambia umependa nini? Tuheshimiane. Nimetumwa hapa na kaunti ya Lamu. Namhurumia sana mama na watoto wa marubani wawili walioshikwa South Sudan. Hii siku ya leo watu wanafurahia Valentine’s Day ilhali wao wanahuzunika. Ningependa muda uongezwe. Waziri wa masuala za nje na wengine wafuatilie. Waharakishe ili wale marubani wawili walioshikwa kule na waasi baada ya ndege yao kuanguka waachiliwe huru. Marubani wamezuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Nahurumia sana bibi yake na watoto, ambao hawana habari ni lini wataachiliwa. Ningependa pia kuwaeleza Mawaziri waharakishe kwa sababu watu wakisherehekea mambo mengine, nimesikia mwenzangu akisema watu huko Lamu ... view
  • 14 Feb 2018 in National Assembly: barabara ilifuata nyumba. Hakukuwa na ramani ya barabara. Kwa hivyo haki za wale watakaoathirika zifuatiliwe. Asanteni. view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami nichangie Hoja hii. Kwanza, ningependa kumpongeza Rais wetu mpendwa kwa ukakamavu wake na busara yake aliyotumia mpaka jana tukafikia kwamba Wakenya wenyewe wanasema sasa watarudi kazini. Leo tukitoka nyumbani, tumewaona Wakenya wamejitokeza kwenda kazini. Ni kama sasa tumepata nafasi ya kufanya kazi. Tulikuwa tunashikiliwa sana. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ni muhimu sana barabara za kando zitengenezwe. Utafahamu zaidi kama umewahi kuwa katika ambyulensi. Mimi nimewahi kuwa ndani ya ambyulensi na mgonjwa. Wakati upo hapo ndani na mgonjwa unatamani uweke mabawa na uruke hasa ukiona hali ya ... view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: hapa, zitapunguza kupoteza uhai wa binadamu na pia zikiwekwa zitawasaidia maafisa wa polisi wa trafiki kuwashika wale wanaovunja sheria. Jana tuliwapoteza maafisa wawili wa usalama barabarani. Sababu kubwa ni kwamba barabara ni mbaya. Najua mjenzi amepewa kandarasi ya kujenga. Tunamhimiza afanye bidii maana ikiwa barabara za Lamu zitajengwa vizuri, wahalifu na wakora hawatapata nafasi rahisi kwa sababu gari zitakuwa zikienda kwa kasi. Hawatapata nafasi ya kuwaua maafisa wetu wa usalama. Natoa rambirambi kwa familia za maafisa hao wawili ambao wameuawa wakiwa kazini wakichunga usalama Lamu. Jambo lingine nataka kusema ni kwamba watu wengine wameanza kupinga ujenzi wa barabara hizi kwa ... view
  • 29 Nov 2017 in National Assembly: yake aliyoisema kuwa Lamu pia ipate waziri safari hii. view
  • 8 Nov 2017 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika. Ninashukuru umenipatia nafasi hii nami nichangie. Nina- support Hoja hii. Kama utaniruhusu, ningependa nami kutoa rambirambi zangu kwa--- view
  • 8 Nov 2017 in National Assembly: Ninaunga mkono. view
  • 8 Nov 2017 in National Assembly: Kama utaniruhusu, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa jamaa na marafiki wa Gavana wa Nyeri. Mimi na watu wa Kaunti ya Lamu tunasema pole. Pia Lamu tumekuwa na mkasa mdogo na ningependa kutoa rambirambi zangu. Kuna mgonjwa wa akili aliyekuwa anatembea msituni. Maafisa wa KDF walimpiga risasi kisha wakaandika wameua gaidi wa Al-Shaabab . Tunatoa pole na tunaomba wahusika waombe msamaha kwa sababu familia ina uchungu sana na sisi kama viongozi wa Lamu tunajaribu kuweka jamii na maafisa wa usalama wawe karibu na wasiwe mbali sana ili wakiona mtu anapita ambaye hawamjui wapeleke habari. Hata hivyo mambo haya yakiendelea kwamba watu ... view
  • 8 Nov 2017 in National Assembly: Mhe. Spika wa Muda, nakushukuru sana kwa kunipatia hii nafasi nichangie Hoja hii na kuiunga mkono. Ni vizuri kuwa na mpangilio ili tufaidike kutokana na lile tunalotafuata. Mwanzo, ningependa kuishukuru ile kampuni ya Zarara ambayo iko Lamu. Wamejitahidi sana. Wanakwenda mashinani kuzungumza na jamii. Kwa hivyo, jamii katika Lamu Magharibi, na haswa katika Wadi ya Faza, wanajua kile kinachoendelea. Naomba pia kampuni zote zinazokuja Lamu kwa chochote wahusishe jamii vizuri. Pia, kile kinachopatikana kutokana na kuchimbwa kwa madini kiwe kinafaida jamii maana vitu vingine kama ule mradi wa makaa Lamu umeleta shida sana. Viongozi waliokuweko labda waliwaonyesha manufaa; lakini sisi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus