18 Apr 2018 in National Assembly:
Maafisa wengine wa Serikali wanaohitaji ushauri nasaha ni wale wanaofanya kazi katika Huduma Centre. Lamu inastahili kuwa ya kwanza kupata huduma hizi. Tunazihitaji sana kwa sababu watu wengi hupigana wao kwa wao. Hata wenyenji wa Lamu East wanakatana kwa mapanga kwa sababu ya kukosa ajira. Imewaharibu akili. Wengine wanaenda sehemu ambazo hazifai. Wengi wao wamevuka mpaka na kwenda hadi Somalia kwa sababu wana shahada lakini hawana kazi. Wakipata ushauri nasaha utawasaidia sana. Wengine wanaingilia mambo ya kusikitisha. Tumefanya assessement ya vijana na tukapata hivi: katika wadi ya Faza, asilimia 20 ya vijana wana maradhi ambayo wao hawajasema wako nayo. Hawajawambia ...
view
18 Apr 2018 in National Assembly:
imewaingia watu na hawana la kufanya. Kwa hiyo wameingilia matumizi ya mihadarati sana. Vijana wetu Lamu wameisha. Hatuna vijana Lamu. Vijana ambao wameingilia matumizi ya mihadarati na kwa mambo mabaya ni asilimia 57 kwa makadirio ya daktari. Haya yote yametokea kwa sababu wamekosa huduma za ushauri nasaha. Wangeitwa, wakalishwe chini na waelezwe hali ilivyo wangekuwa faida kwa Serikali, Lamu na Kenya nzima.
view
18 Apr 2018 in National Assembly:
Nakubaliana na haya na mwenzangu aliyependekeza Mswada huu. Ingekuwa vizuri utiliwe mkazo utusaide sote. Akina mama wanaona vibaya watoto wao wakipotea.
view
21 Mar 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ambayo nimeitafuta kwa muda mrefu. Ningependa Wabunge wajue kwamba ukitetea askari wa eneo Bunge lako au jimbo lako, yule askari kesho atakuwa Lamu. Huwezi mlipa sawa askari aliye Nairobi na askari aliye Lamu katika Boni Forest. Huwezi ukamlipa sawa askari ambaye ako Gamba Police Station au Kiangwi na askari ambaye ako Nairobi. Tusitetee kwamba hao askari watabaki pale pale. Hawa askari kawaida wanahamishwa. Itakuwa si sawa. Itafika wakati askari watakataa kwenda kule. Kuna wengine wanakataa hata wako tayari kuacha kazi kwa sababu ya kupelekwa sehemu kama Lamu. Lazima wapewe posho---
view
21 Feb 2018 in National Assembly:
Asante Bwana Spika. Ninashukuru umenipatia nafasi hii nami niweze kuchangia hii sera ya makazi. Kwa ruhusa yako, naomba nisome jinsi Katiba inavyosema kwa lugha ya Kiingereza. The Constitution states that every person has a right to access adequate housing and a reasonable standard of sanitation. Further, Article 21(2) states: “The State shall take legislative, policy and other measures including the setting of standards, to achieve the progress realisation of the rights guaranteed under Article 43.” Hii Sera ni muhimu sana. Saa hii katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki kuna barabara inayojengwa. Barabara hiyo inatoka Mtangawanda ikielekea Kizingitini. Ni maendeleo mazuri ...
view
20 Feb 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa pia kuunga mkono Hoja hii. Kuwa na mazingira masafi ni muhimu sana. Wenzangu waliozungumza mbele yangu wameongea kuhusu ajenda nne za Serikali Kuu. Sisi tunajua kuna Rais mtawala kulingana na Katiba. Hao wengine hatuwajui. Hizo ajenda zake nne alizosema haziwezi kutimizwa ikiwa kuna mabadiliko ya tabianchi. Pia, kuna umuhimu wa Serikali Kuu na kaunti kutenga fedha ambazo zitasaidia kuzuia haya mabadiliko ya tabianchi.
view
20 Feb 2018 in National Assembly:
Ni bora watu wajue kwamba haya mabadiliko ni ya ukweli. Tumeyaona na yanasababisha shida nyingi kwa kila kaunti. Mbunge mwenzangu amesema kwamba kaunti tano The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
20 Feb 2018 in National Assembly:
zimejaribu kurekebisha haya mambo na wanajitolea mhanga kusaidia. Mimi pia nitachukua jukumu huko kwetu na kuongea na gavana wangu ndio Lamu iwe kaunti ya sita kwa kusadia kurekebisha haya mabadiliko. Nimeshuhudia Mlima Kilimanjaro kutoka mwaka wa 2004 nilipoanza kazi. Nimekuwa nikipitia juu ya mlima huo nikiwa ndani ya ndege. Siku hizi, nikipitia hapo naona mabadiliko makubwa ya barafu iliyokuwa hapo awali na ile iko sasa. Nilisoma kwa kitabu kimoja kwamba barafu hiyo ikiyeyuka watu wa Lamu wanaathirika zaidi kwa sababu wanaishi baharini. Yale maji yanakuwa mengi na wanapata shida nyingi. Nimeona ni muhimu nichangie ili tuweze kuajibika pamoja. Huko Lamu ...
view
14 Feb 2018 in National Assembly:
Asante sana,Naibu Spika wa Muda. Mimi pia ninaunga mkono kuongezwa kwa muda kwa sababu tunawahitaji sana hawa Mawaziri. Kuna kazi nyingi ambazo tunatarajia watazifanya na kuzikamilisha, baada ya kuapishwa. Watu wamezungumzia siku ya kupendana, kwa umaarafu Valentine’s Day .
view