20 Jun 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Hoja hii. Haya ni mambo muhimu sana, hasa kule kwetu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Lamu. Lamu kuna shule ambazo zimefungwa kwa sababu ya mambo ya kutokuwa na usalama. Wanafunzi wanapata shida kwa sababu wakiamka asubuhi, wanalazimika kuenda kutafuta maji walete kwa nyumba zao ili hayo maji yatumike kutengeneza chakula cha mchana na chakula cha usiku. Kwa hivyo, mpango huu utasaidia sana. Nikitoa ushuhuda, mimi ni mmoja wa waliofaidika na Maziwa ya Nyayo na tuliyafurahia sana. Matokeo yake yalionekana. Mpango huu ukifanyika utasaidia sana wanafunzi. Wabunge wakisema kila Mkenya anafaa kuwa sawa na Mkenya mwingine, bado tuna sehemu kama Lamu ambapo hatujakuwa sawa na wengine. Wale wanasema hivi labda wanaangalia Nairobi na kaunti zingine. Wanafaa ...
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi niweze kuchangia Hoja hii. Naiunga mkono Hoja hii. Huyu mheshimiwa ambaye ameleta Hoja hii amefikiria sana. Hili ni jambo la maana kwa sababu vijana wetu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
wanarandaranda mitaani. Kila kaunti ina matatizo yake. Katika Kaunti ya Lamu, jambo hili litasaidia pakubwa.
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Mwanzo kabisa, tutaona mabadiliko katika magereza. Idadi ya vijana magerezani itapungua sana kwa sababu watakuwa wamepata jambo la kufanya. Lamu ni tofauti na kaunti nyingine kwa sababu kuna upande wa visiwa na ardhi, na matatizo yao ni tofauti. Katika Faza Ward, ambayo ni kisiwa kikubwa, vijana hupigana wakilipiza kisasi kwa sababu hawana kazi ya kufanya. Shule za michezo zikijengwa katika maeneo bunge, zitawasaidia pakubwa sana kwa sababu ni vijana ambao wanapenda kazi hiyo. Zitawafanya wawe na umoja na uwiano. Pia ikiwa hizo shule zitahusisha kaunti nzima, itabidi upande wa Lamu Mashariki na Lamu Magharibi waletwe pamoja ili wawe na uwiano.
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Ndugu yangu, Woman Representative wa Isiolo, amesema kwamba kuna kaunti ambazo zina matatizo ya vijana kuvuka kwenda Somalia. Shule za michezo zitapunguza hilo tatizo pakubwa. Kumekuwa na matatizo mpaka akina mama wanalia kwa sababu hawajui ni nini kinachoendelea. Akina mama ambao wako nyumbani hawajui ukweli wakati watoto wao wanafuatwa na polisi. Haya matatizo yatakwisha vijana wakishiriki katika michezo. Pia, kuna tatizo la kuonea watu wengine wivu wakati wamekaa pamoja. Kuna wengine wamepata zaidi na wengine hawajapata. Wivu huchangia kuwepo kwa matatizo fulani katika Kaunti ya Lamu. Hali hiyo itapungua shule za michezo zikijengwa katika maeneo bunge. Watu wakiketi pamoja watapendana ...
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Lisianzishwe kwingine na Lamu iwe ya mwisho. Sisi watu wa Lamu husahaulika wakati miradi mingi inaanza tunakuwa wa mwisho. Naomba lianzishwe kwenye kaunti zote ili sote tusaidike. Matatizo mengi yatapungua especially upande wa akina mama. Tuna kipato kidogo cha kusaidia youth na tuko tayari kujitolea na kushirikiana na jambo kama hili ili youth wetu wasaidike. Kama mwenzangu ambaye alinitangulia amesema, hili jambo litaleta upendo na kusaidia watu kufanya exercise . Tunajua magonjwa mengine husababishwa na watu kutofanya
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
au walizoea kufanya wakiwa shuleni…
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, nimepotelewa na ulimi na kukosea. Asante kwa kunirekebisha. Nimechagua Kiswahili. Msinitoe mbali na hii Hoja kwa sababu ni nzuri. Ni vizuri sote tukichangia tujiangalie ili tusipelekane kwa mambo madogo. Hili ni jambo la maana na tunaomba litiwe mkazo. Vijana wetu wanatuangalia na kutamani sana. Wengine wanatuma message kwa simu kwamba tuchangie hii Hoja kwa sababu wamegonjea, na ilikuwa ije hapo awali. Saa hizi walikuwa wanatarajia iwe imefika mashinani. Kwa hivyo, tuharakishe ili ifike mashinani wanangojea kwa hamu sana.
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view