Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 2001 to 2010 of 2263.

  • 10 Feb 2016 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono dada yangu, Sen. Wangari, kwa kuleta Mswada huu wa kuleta marekebisho katika sekta ya utendakazi. Ukweli ni kwamba sio sisi sote kama binadamu tunauwezo wa kupata watoto na kuwalea. Kuna wale walio katika ndoa na wale ambao hawamo. Katika maisha, kila binadamu aliyehai kuwa na hamu ya kupata mtoto. Wasiokuwa na uwezo wa kupata watoto, wamepewa nafasi katika sheria kuweza kupata watoto kisheria; katika lugha ya Kingereza inajulikana kama “ adoption” . Bw. Naibu Spika, kuna umuhimu kwa Bunge la Seneti kuzingatia binadamu wenzetu wasio na uwezo wa kupata ... view
  • 10 Feb 2016 in Senate: Bw. Naibu Spika, kunradhi kama matamshi niliyosema hayafai. view
  • 10 Feb 2016 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika kwa kufafanua. Kunradhi dada yangu kama nimesema jambo ambalo pengine limekuumiza moyo. Ninakotoka, tukisema “Vipofu”, ni wengi. Tukisema “Kipofu”, ni mmoja. Katika hali ya utendakazi wa kuzaa, sio watu wengi wanaofanya pamoja. Ni mtu mmoja pekee ndiye anayefanya kitendo kile. Ndiyo sababu nikasema ya kwamba, “Ki” na ni yule mmoja anayefanya namna hiyo. Kwa hivyo pole--- view
  • 10 Feb 2016 in Senate: Kunradhi dada yangu basi kama nimeongea jambo ambalo limekuguza moyo, sio sinto fahamu zangu. Utanisamehe. Bw. Naibu Spika, nilikuwa nasema ya kwamba katika Mswada huu ambao umeletwa na dada yetu Sen. Wangari, pia vilevile tumezingatia ya kwamba tumetangulia hapo awali kusema kuzaa sio hoja lakini kufuga ndio msemo ya kwamba ikiwa uko na uwezo wa kuzaa, basi uwe na uwezo wa kufuga. Ikiwa hauna uwezo wa kufuga, basi afadhali umpishe mwenzako ambaye ana uwezo wa kufuga. Kuna msemo usemao: “Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo”. Ule muda ambao mzazi anapewa kama ni miezi mitatu, uwe na mama awe na mtoto wake ndani ... view
  • 10 Feb 2016 in Senate: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. Is the distinguished Senator in order to say that men are irresponsible and do not spend time with children when they are born, when in fact, some of us are responsible from the day the child is born? view
  • 9 Feb 2016 in Senate: Asante Bw. Spika, kwanza, kwa makaribisho yako ya mwaka wa 2016, na pongezi kwa kazi ambayo sisi Maseneta tulifanya. Vile vile, nakushukuru kwa kuwakaribisha wananchi kutoka Kilifi ili wajifunze hali na taratibu za utendakazi. Nina imani kwamba wakirudi kwao watatumia elimu watakayoipata katika Seneti kuendeleza Kaunti ya Kilifi. Nakuunga mkono katika kuwapongeza sana Maseneta wenzangu kwa kazi tuliofanya. Tumepitisha Miswada mbalimbali na itakuwa jambo la muhimu ikiwa sheria tulizopitisha zitalisaidia taifa letu la Kenya. Asante, Bw. Spika. view
  • 2 Dec 2015 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Tumeambiwa kwamba hatimaye Bw. Madaga alilazwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Kenyatta. Je, ni daktari wangapi ambao walimhudumia marehemu Madaga? Hakuna hata mmoja ambaye ametajwa kwenye hii Ripoti. Ni kina nani ambao walimhudumia marehemu Madaga akiwa hali mahututi? view
  • 1 Dec 2015 in Senate: Bw. Spika wa Muda, mpaka sasa sijapata taarifa mwafaka inayoweza kujibu swali ambalo ndugu yangu, Sen. Omar, aliuliza. Naomba nipewe muda kidogo ili niweze kukamilisha mawasiliano yangu. Nina uhakika kwamba siku ya Alhamisi nitakuwa tayari kutoa taarifa hiyo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 1 Dec 2015 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nataka kuhakikishia Seneti kwamba nitakuwa na jibu mwafaka siku ya Alhamisi. view
  • 1 Dec 2015 in Senate: Bw. Spika wa Muda, sina jibu wakati huu, lakini--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus