Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 2191 to 2202 of 2202.

  • 15 Oct 2013 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, nataka kumpongeza dada yangu, Sen. Elachi, kwa kuleta Hoja hii. Kitu ambacho nataka kufafanua zaidi ni upande wa Katiba. Mimi kama mwanasheria, nahisi kuwa kuna umuhimu wa kuthibitisha sheria za Katiba. Kulingana na Kipengele cha 96, kinasema kuwa jukumu letu si kuwakilisha peke yake, bali ni kulinda na kutetea rasilmali za kaunti na serikali zake. Hiyo, kisheria, haina haja ya kufafanua zaidi. Kazi ya Seneti hapa ni kulinda na kutetea serikali za kaunti. Kwa hivyo, ni makosa kuona ya kwamba shirika linaloangalia suala la mishahara ya wafanyikazi wa Serikali halizingatii ... view
  • 15 Oct 2013 in Senate: wakati wa mama huyu kujificha kama mbuni umekwisha. Kunao umuhimu wake kukaa na kufahamu ya kwamba ikiwa yeye anapata mshahara wa mamilioni, basi kunao waheshimiwa katika bunge za kaunti ambao wanapata mshahara wa Ksh79,000 kwa mwezi; na kunao umuhimu kuona ya kwamba zile pesa wanazopata zimeongezwa. Tunajua kabisa kuwa sheria za leba za wafanyikazi zinazosema ya kwamba mfanyikazi anayelipwa vizuri huwa pia anayo bidii ya kufanya kazi. Lakini mfanyakazi ambaye humlipi vizuri hana budi kukuibia wewe mwenyewe kama tajiri. Tunaanza mfumo ambao ni wa kusikitisha kwa sababu ikiwa hawa tumewapatia jukumu kama waheshimiwa katika bunge za kaunti, na mapato yao ... view
  • 18 Sep 2013 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza, ningependa kumpongeza wakili Seneta Mutula Kilonzo Junior kwa ushindi wake katika uchaguzi mdogo. Ushindi wake ulikuwa wa kukamilika na kuthibitisha ya kwamba ni wakili na mtetezi ambaye watu wa Kaunti ya Makueni walikuwa wamejitolea kumpa nafasi ili aweze kuwahudumia. Bw. Spika, namfahamu Sen. Mutula Kilonzo Junior kama wakili mwenzangu ijapokuwa nimepita viwango kadha nikwa jaji na hatimaye kuweza kustaafu. Kama wakili, kuna nyakati amekuwa mbele yangu nikiwa jaji na nimeona kwamba amekamilika kiwakili. view
  • 18 Sep 2013 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kumpongeza Sen. (Prof.) Lonyangapuo kwa Hoja hii. Mtu anayeitwa KPR ni askari ambaye amepewa kifaa cha kujitetea, kulinda amani na kuweza kuona ya kwamba watu wanaishi kwa amani. Lakini tunajiuliza ni kwa sababu gani watu hawa wanaopewa vifaa kama hivi hawalipwi mishahara. Ni mpango gani Serikali iko nayo kuona ya kwamba watu hawa wamelipwa mishahara? Kutolipwa mishahara inamaanisha kwamba watu hawa wanafanya kazi bure ilhali hii si kazi ya kanisa, bali ni kazi ya kulinda amani. Amani haiwezi kupatikana kule pwani ikiwa mashamba ya watu wa pwani yamechukuliwa na ... view
  • 24 Jul 2013 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, is it in order for my colleague to refer to the Temporary Speaker as “Mr. Chairman?” view
  • 23 Jul 2013 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Nataka kuunga mkono Mswada huu wa ugawanyaji pesa. Kama tunavyoelewa, kulingana na kipengele cha 96 cha Katiba, sisi kama Seneti kazi yetu ni kulinda na kutetea rasilmali za zile kaunti tunazotoka. Ya pili ni kuhakikisha kwamba ugawanyaji wa pesa zitakazotoka katika Serikali kuu zimefika mashinani na zimefanya kazi inayohitajika kufanyika huko. Wakati ule Mswada wa pesa ulipokuja hapa, tuliona kwamba pesa zile zilikuwa hazitoshi, ndio sababu tukasema ziongezwe kutoka Ksh210 bilioni hadi Ksh258 bilioni. Lakini kwa ukosefu wa nidhamu ama kutozingatia masilahi ya serikali za kaunti, zile pesa zilipunguzwa ama zilibaki pale ... view
  • 23 Jul 2013 in Senate: Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, nataka kuunga mkono na kusema kwamba Mswada huu ni mzuri na utaweza kuleta maendeleo, hasa tukihakikisha kwamba wale magavana ambao wako katika utawala wa serikali za kaunti wasitusiwe. Tumeona hivi majuzi kwamba wanaitwa sijui “maraisi.” Ukiitwa “his Excellency,” wewe sio raisi; unaitwa “ his Excellency the Governor ;” haukuitwa “ his Excellency the President .” Lakini tukiangalia watu wengine – kwa sababu wanajaribu kuharibu majina ya hawa watu walio pale – wanaanza kutumia lugha isiyofaa. Mimi nasema ya kwamba magavana wetu wanafanya kazi nzuri, na kulingana na utawala wao mpaka sasa, naona ya kwamba wanafanya ... view
  • 11 Jul 2013 in Senate: Bi. Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasi hii. Pia mimi ningependa kujumuika na Maseneta wenzangu na Wakenya wengine kuomboleza vifo vya wanafunzi vilivyotokea kule Kisii. Hawa ni baadhi ya wanafunzi ambao wamechaguliwa na wana akili sana. Kama tunavyojua, ukisomesha mwanafunzi umesomesha taifa nzima. Maisha yao yamekatizwa kwa wakati ambao haujafika. Mimi, familia yangu na watu wote wa Kilifi County ningependa kuwapatia pole sana wazazi wa watoto hawa, familia na jamii zote za watu wa Kisii haswa nikizingatia sana Gavana ambaye ni rafiki yangu, Gavana Ongwae. Ninajua ana wakati mgumu sana wakati huu. Pia ningependa kumwambia kwamba aweke juhudi ... view
  • 3 Jul 2013 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi nichangia Hoja hii. Pia ningetaka kuchukua nafasi hii kumshukuru Sen. Obure kwa kuleta Hoja hii inayowahusu wafanyakazi. Kama sote tunavyojua, mfanyakazi ni mtu muhimu sana katika uendelezaji wa uchumi wa nchi yetu. Lakini ni jambo la kusikitisha tukiona kwamba baada ya mfanyakazi kustaafu anapatikana barabarani, ofisini na nyumbani za marafiki akiomba omba ili apate namna ya kuweza kujikimu kimaisha. Ningetaka kuhimiza mapato ambayo yanapewa na mahakama yalipwe mara moja kwa sababu ni haki ya mfanyikazi. Mfanyakazi aliyefanya kazi au kwa bahati mbaya amepoteza kazi yake, ni sharti alipwe ikiwa mahakama imeamua ... view
  • 3 Jul 2013 in Senate: On a point of information, Madam Temporary Speaker. His Excellency the President referred to children joining class one and not those that are one year old. view
  • 24 Apr 2013 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuwashukuru watu wa Kilifi Kaunti kwa kunichagua kama Seneta wao wa kwanza. La pili, pia vile vile ningependa kukupongeza kwa kuchaguliwa kama Spika wa Seneti. Pia, ningependa kuwapongeza Maseneta wenzangu kwa kuchaguliwa kuwa Maseneta. Katika Hotuba ya Rais, alizungumzia kuhusu kutofautiana kwa maoni na kuheshimiana. Ningependa kuongea juu ya mambo ya utalii. Ile Kaunti ambayo ninawakilisha hapa Seneti ina hoteli nyingi kuanzia Mtwapa mpaka Tana River. Hoteli hizo hutembelewa na watalii wanaotoka katika sehemu nyingi sana za nchi za ng’ambo. Watalii wanaokuja katika nchi yetu, baadhi ya wale wanaotembelea mbuga za ... view
  • 24 Apr 2013 in Senate: Asante, Bw. Spika. Naunga mkono. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus