4 Mar 2014 in Senate:
Wakati wa kulala usiku, alikuwa analala katika hali hiyo, nusu ya mwili wake ukiwa ndani ya maji. Kwa sababu ya jambo kama hili, ilibidi niende kortini kuielezea hali yake. Ninamshukuru sana Justice Ang’awa ingawa sasa ni hakimu kwa sababu aliamuru aachiliwe mara moja.
view
4 Mar 2014 in Senate:
Jambo lingine ambalo ningependa kugusia ni juu ya Wakili Rumba Kinuthia. Yeye ni wakili maarufu sana. Lakini ukiona hali yake ya kiafya hivi sasa, ni ya kusikitisha. Yeye ni wakili ambaye nimeangalia hata katika ule uamuzi uliotolewa alipokuwa ameenda kortini, ya kuambiwa kwamba yeye hawezi kupewa ridhaa kwa sababu hakuweza kutoa kithibitisho kuwa aliumia alipokuwa mfungwa korokoroni; kufungwa bila haki na kukosa kuwa na jinsia ya familia yake, kukosa kuwa na mkewe ndani ya nyumba na kwa miaka isiyojulikana kufungiwa korokoroni, hiyo ni haki kweli? Tunasema watu kama hao ambao judgement zao zilikuwa kutupiliwa mbali waweze kuangaliwa. Watu kama Kenneth ...
view
26 Feb 2014 in Senate:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. I have restrained myself from standing on a point of order, because the debate is going on very well in this House. But I think that we are also taking an extremely difficult position when we allow ourselves to go outside the ambit of our Standing Orders. I am referring to Standing Order No.78 which reads:- “(1) All proceedings of the Senate shall be conducted in Kiswahili, English or in Kenyan Sign Language. (2) A Senator who begins a speech in any of the languages provided for under paragraph (1) shall ...
view
26 Feb 2014 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza, nataka kumpatia mkono wa heko ndugu yangu, Sen. Moses Masika Wetangula, kwa ushindi wake mkubwa ijapokuwa mimi sikuenda kule kwa sababu nilikuwa mgonjwa. Lakini sio hoja; ushindi wake ulithibitisha kabisa kwamba watu wa Bungoma wanampenda zaidi. Bw. Naibu Spika, Sen. Wetangula amekuwa wakili mkubwa katika nchi hii. Mimi nikiwa kama jaji nimemwangalia katika mikakati zake zote za uwanasheria na pia akiwa Waziri wa Mambo ya Nje. Nafikiri kuwa uamuzi wa ndugu yangu, Sen. Boni Khalwale na Sen. Kennedy Okong’o kujiweka kando na kumpisha ndugu yetu, Sen. Wetangula, kuchukua nafasi hiyo, ni jambo la heko. ...
view
14 Feb 2014 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, Kilifi votes “yes” to all the counts.
view
14 Feb 2014 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, Kilifi votes “yes” to all the counts.
view
5 Dec 2013 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Ningependa kusema kwamba huu ni Mswada muhimu sana kwa Wakenya. Kulingana na mambo yoyote yanayohusu habari, hiki ni kiungo cha kati baina ya mwananchi na viongozi wake. Katiba inasema kwamba katika jambo lolote ambalo linahusu wananchi au kaunti, Seneti itahusishwa wakati wowote ikiwa kutakuwa na Mswada. Habari ni kiungo cha kati ambacho kinahusu mambo ya wananchi. Itakuwa na upungufu kuona ya kwamba Mswada kama huo unapitishwa na upande mmoja wa Bunge.
view
22 Oct 2013 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii iliyoletwa na Sen. Elachi. Jambo la kwanza ambalo ningependelea kuunga mkono ni kwa sababu ni haki ya mfanyikazi kuona ya kwamba wakati wa ugatuzi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
15 Oct 2013 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Spika. Je, ni haki kwa ndugu yangu, Sen. (Dr.) Machage, kutumia neno “hasara” badala ya jina Sarah? Tunajua neno “hasara” linamaanisha jambo mbaya. Je, ni jina lipi lilo sawa ni Bi Sarah au hasara?
view