14 Feb 2023 in Senate:
On a point of order Mr. Speaker, Sir.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Bw. Spika, hoja yangu ya nidhamu ni kwamba kuambatana na sheria za hapa ndani yaani Standing Orders zetu na pia zile sheria ambazo ni za Spika, tunatambua ya kwamba ni lazima mtu awe amevaa kisawasawa. Hatuwezi kuingilia katika maisha ya mtu vile anavyotaka kuvaa, lakini hapa Seneti---
view
14 Feb 2023 in Senate:
Bw. Spika, Kiswahili safi ni kwamba, mwanamke akiwa vile, huwa anamwaga damu na hatakikani hata kidogo kuonyesha umati wa watu ama ndugu zangu hawa wanaume wako na wake zao na madada zao wa heshima. Saa hizi, mke wa (Dr.) Khalwale, anatutazama na anaona vile mheshimiwa ameingia hapa akiwa anavuja damu kutoka sehemu zake za siri. Je, hii ni haki ndani ya Bunge hili la Seneti?
view
14 Feb 2023 in Senate:
Bw. Spika, hatupingi uamuzi uliotoa kwamba Sen. Sifuna atoke nje kwa sababu amejibizana nawe. Ningependa kusema kitu kimoja. Aliyeanzisha fujo hakutolewa licha yake kufanya hivyo mara mbili akiwa hapa ndani. Alitoka pale alipokuwa ameketi akaja hapa na kusema alivyosema na ukamwambia aketi lakini hakukaa. Ulipoendelea kuongea, alirudi hapa mara ya pili na akaendelea kujibizana nawe. Amejibizana na upande huu kwa mara ya tatu kwa sababu alikuwa anamwambia asikilize amri ya Spika. Kama wangekuwa wachezaji wa mpira, basi wote wawili walifanya makosa. Ukipeana kadi nyekundu huku, unafaa kupeana kule pia ili wote wawili watoke nje. Hiyo itaonyesha kuwa haki imetendeka. Sipingi ...
view
14 Feb 2023 in Senate:
Tafadhali, Seneta kiongozi mwenzangu, siwezi kujibizana nawe ukiwa umepewa nafasi kuongea. Nitanyamaza mpaka wakati wangu ufike. Bw. Spika, kwa hisani yako, na ninajua sheria inauma pande zote mbili, kwanza, yule amefanya makosa makubwa. Alipojibizana nawe mara ya kwanza, ulifaa kumtolea kadi nyekundu na kuamuru aende nje. Inaonekana kwamba umelemea upande huu na kupendelea upande ule mwingine. Aliyeanzisha fujo ni Seneta wa Embu. Hata Wakenya wote wameona. Nakuomba, Bw. Spika, adhabu uliyotoa kwa upande wa walio wachache inafaa kutolewa pia kwa upande wa walio wengi. Asante sana.
view
14 Feb 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika. Naunga mkono yote yaliyosemwa na ndugu yangu kiongozi wa walio wengi, Sen. Cheruiyot. Kwanza, nawashukuru maseneta ambao wako hapa sasa hivi. Wale saba ambao wako kwenye list hii ni maseneta ambao wamechaguliwa na upande ule mwingine na upande huu wa walio wachache pia. Nikiangalia hii list ya hawa maseneta saba, ni watu waliojukumika, walio na taaluma tofauti tofauti ambazo wataleta katika Senate Business Committee (SBC). Nataka kuwapatia kongole kwamba ni watu ambao wamekamilika kisawa sawa. Kuna Sen. Ali Roba, aliyekua gavana. Dadangu Sen. Veronica Maina ni wakili mkubwa. Ndugu yangu Sen. Wakili Segei ni wakili mkubwa. Dadangu ...
view
14 Feb 2023 in Senate:
La, tena kubwa sana. La.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Bw. Spika nataka pia kuwahimiza ndugu zangu maseneta ya kwamba majukumu tulionayo ni ya wakenya. Litakua jambo jema ikiwa hivi sasa, muhula huu wa pili ambao
view