14 Feb 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
14 Feb 2023 in Senate:
tuko, tukitia bidii. Tulienda induction ama kufunzwa na kupata taaluma za juu zaidi ili tukija hapa, tuchape kazi vyema. Ndugu yangu Sen. Cherargei ana taaluma ya juu, ili hawa wengine wawe na taaluma kama Sen. Cherargei, lazima tuelimishane. Hii kamati italeta mambo mazuri ndani ya Bunge la Seneti. Sisi tunatakikana kuiga mfano mwema. Mifano ya kusikitisha ni ile tumefanya leo ambayo Bw. Spika ametoa uamuzi wake na tumekubaliana. Nidhamu ni kitu muhimu. Sisi kama maseneta katika ‘nyumba ya juu’, nataka tubaki hapo juu kuliko Bunge la Taifa.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Nakumbuka ule muhula wa kwanza ambao tulikuwa na wale wengine ambao walikua maseneta pia. Kulikua na ndugu zangu Sen. (Dr.) Khalwale na Sen. Cheruiyot. Seneti hilo lilikuwa la hali ya juu sana na liliheshimiwa Kenya nzima. Sisi pia twaweza kuwa hivyo na tukaheshimika. Ukiangalia hapa alipoketi ndugu yangu Sen. (Dr.) Khalwale, GG Kariuki alikua anaketi pale.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Pale pengine alikua anaketi Kiraitu Murungi. Kule kwingine kulikua kunaketi Mutahi Kagwe. Upande huu wa walio wengi ilikua kuna misingi ya watu ambao waliongoza Kenya na walileta mafanikio mpaka hivi leo tumejikuta hapa.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Bw. Spika ukiangalia kwa upande mwingine tulipoanza, tulikuwa katika garage ingine ya Kenya International Convention Centre (KICC), mahali pengine kama tundu. Ilikuwa hatuwezi kuketi mahali kama hapa. Lakini kwa nguvu na juhudu ya wale waliokuweko tumefika hapa. Ni jambo la kujivunia kama Senate .
view
14 Feb 2023 in Senate:
Kwa hivyo, mimi nataka kuwaambia ndugu zangu, tuko hapa kuleta mageuzi ndani ya Kenya, ili Wakenya wapate vitu muhimu au maisha yao iwaletee afueni.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Kwa hivyo, ninaunga haya majina yaliyoletwa hapa kuwa kwa Senate Business
view
14 Feb 2023 in Senate:
(SBC) ili tuweze kupata mafanikio kama Maseneta na pia tuweze kuwafanyia Wakenya kazi.
view
19 Jan 2023 in Senate:
Bw. Spika, tuko na mwenzetu, Seneta aliyechaguliwa ameingia na kuapishwa. Kama ilivyo kawaida yetu, nafikiri ingekuwa muhimu kwetu kwanza tuweze kumkaribisha na kumpa kongole yake kubwa kwa sababu alishiriki katika
view