22 Oct 2014 in National Assembly:
Nauli za Shirika la Ndege la Kenya zinakera. Pia, zinapatia watu wengi masaibu. Kwanza ni ghali. Utaketi kiti na mwenzako vile nilivyokaa hapa na Mhe. Omar Mwinyi na utakuta umelipa nauli tofauti kabisa na mwenzako ambaye ameketi nawe. Kisa na maana ni nini? Ni kwa sababu wewe aidha ulikata tiketi yako mapema na mwenzako amekata tiketi yake baadaye. Nimeona mambo haya katika Shirika letu la Ndege.
view
22 Oct 2014 in National Assembly:
Pili, ukisema unabadilisha masaa yakusafiri; labda ulikuwa usafiri jioni na useme unataka kuongeza masaa, mara nyingi utaambiwa kwamba nauli imebadilika. Kwa nini nauli ibadilike? Ninaposafiri kwenda Mombasa kwa basi, nikisema ninaenda huko nikitumia basi ya saa tatu na nibadilishe nisafiri na basi ya saa tano nauli haibadiliki. Lakini katika Shirika la Ndege la Kenya, utakuta kwamba unalipishwa ada.
view
22 Oct 2014 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukipatikana na mkosi na uamue unabadilisha safari yako, labda ulikuwa umetafuta nafasi ya kusafiri kutoka Nairobi kwenda Mombasa nakurudi, ikiwa hukuchukua safari ya kwanza yakuenda na unatumia nauli yakurudi, pia utalipishwa kwa kutosafiri. Ni mara ngapi tumesafiri na ndege ya shirika hili na unakuta viti viko bure? Ndege inapaa juu na inaenda bure lakini watu wameachwa chini na wanaambiwa kwamba ndege imejaa.
view
22 Oct 2014 in National Assembly:
Tunaomba kwamba Shirika la Ndege la Kenya lipatiwe changamoto, na njia yakulipatia changamoto ili liamke ni kuruhusu mashirika mengine ya ndege kutumia anga yetu ya Kenya.
view
22 Oct 2014 in National Assembly:
Tuko na Mkenya mmoja anayeitwa Rubani Musa Bulhan. Huyu alikuwa ni mmoja wa Wakenya wa kwanza kununua ndege kubwa lakini amenyimwa nafasi ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
22 Oct 2014 in National Assembly:
kutumia hizi ndege kutoka Nairobi hadi Kisumu ama Nairobi hadi Mombasa. Ameamua ndege zake zitoke Nairobi ziende Jeddah na kama si Jeddah ziende Somalia. Je, hili anga ni la Kenya Airways peke yake? Tukiwapatia changamoto, wafanyikazi wa shirika la Kenya Airways watageuza mienendo yao na tabia zao na kuanza kuwajibika. Mara nyingi, wafanyikazi wa shirika hilo ni wazembe, wafidhuli na mahanithi. Siwezi kusema mengine, lakini wafanyikazi wa Kenya Airways wamekuwa wajeuri kiasi kwa sababu wanajua kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kupatiwa nafasi ya kuleta ndege zake humu nchini.
view
22 Oct 2014 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, mara nyingi, unapoenda kwenu kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Eldoret, hutumia ndege gani? Utaona kwamba ni shirika moja tu ambalo limepewa nafasi – Kenya Airways. Kampuni nyingine inayoruhusiwa kupeleka ndege huko ni Flight 540. Mimi na mhe. Mwinyi tukichukua mkopo kutoka kwa benki na kununua ndege hatuwezi kuruhusiwa kutumia anga ya nchi hii kwa sababu imetengewa Kenya Airways. Kwa hivyo, ninatoa changamoto kwa Serikali iweke anga yetu wazi kwa wale watu ambao wangependa kushiriki katika biashara ya usafiri wa ndege ili nauli za ndege zishuke.
view
22 Oct 2014 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninatoa ombi langu kwa mara nyingine na kumshukuru ndugu yangu, Alhaj Omar Mwinyi, kwa kuuleta Muswada huu Bungeni.
view
21 Oct 2014 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Naomba nami nichukue nafasi hii kupeana rambirambi zangu kwa familia ya kaka yetu, ndugu yetu mpendwa, Prof. Ali Mazrui. Wengi wetu tulimfahamu Prof. Ali Mazrui tukiwa chuoni kama wanafunzi wakati alikuja kupeana mijadala kadha wa kadha, ijapokua wakati huo ilikua vigumu sana kwa mtu msomi mwenye fikira tofauti na za uongozi, kukubaliwa kuendelea kupeana mijadaala. Ilibidi mara nyingi Prof. Ali Mazrui awe nje ya nchi kwa kueneza na kufunza watu ambao walikua wanahitaji elimu yake na ufasaha wake. Tutakubali kuwa Prof. Ali Mazrui alikua amesifika. Alikua ana sifa za hali ya juu. Prof. Mazrui alikua ametukuzwa na ...
view
21 Oct 2014 in National Assembly:
wote kwa ujumla, Mwanakenya shupavu; shujaa. Nina imani atawekwa katika kumbukumbu zetu nchini kuwa mmoja wa watu wa Kenya ambao wamejibidisha iwezekanavyo katika mrengo wa elimu. La mwisho, naomba wenzetu ambao pia nao wamesoma, wajaribu wawezavyo kuiga mfano wa Prof. Ali Mazrui. Si mtu ambaye alikuwa anataka kujilimbikiza mali ya ulimwengu. Sote tunajua tunaiacha, bali aliishi kama mtu mnyenyekevu, mpole mwenye hekima na busara, na mstaarabu. Yote haya ni maadili ambayo yalikua na Prof. Ali Mazrui. Kwa hayo machache, naomba kutoa pole zangu kwa familia na nchi nzima kwa ujumla. Ahsante Mhe. Spika.
view