15 Oct 2014 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Spika. Naomba tuu uniruhusu kwa heshima yako nimpatie mwenzangu, Mheshimiwa Wamalwa aendelee na huu mjadala.
view
15 Oct 2014 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii nami nitoe mchango wangu kuhusu sekta hii ya boda boda. Kama uelewavyo, shughuli za boda boda zimeenea kila pembe ya nchi yetu. Huwezi kwenda pahali popote na kukosa vijana wakifanya biashara, ama shughuli za boda boda. Kwa hivyo tunakubaliana sote kuwa ni biashara, ni sekta ambayo inakua na inahitaji kupatiwa msaada, ama kutiwa shime ili ipate kukua zaidi. Imeongeza uchumi wa nchi, imetoa ajira; vijana wanafanya kazi wao wenyewe bila kung’ang’ana, au kuzozana, na watu wakitafuta ajira. Kitu kinachohitajika ni kuboresha sekta hii ili hao vijana wawe wanaweza kutoa huduma kwa The ...
view
15 Oct 2014 in National Assembly:
umma, huduma ambayo ni nzuri, huduma ambayo haitaumiza watu, huduma ambayo ni rahisi na itarahisisha usafiri. Vijana ambao wanashughulika na kazi ya boda boda mara nyingi wana shida. Moja ya shida wanazokumbana nazo ni ukosefu wa mafunzo ya kutosha. Kama wangekuwa wamefunzwa uwajibikaji, na kujua sheria za barabarani kulingana na sheria za usafiri, bila shaka, ajali tunazoziona nchini mwetu zingekuwa zimepungua. Jambo lingine ni kuhusu vifaa. Utakubaliana nami kuwa mara nyingi hawa vijana wanabebana bila kuvaa kofia ambazo zinaweza kuwasaidia wakati wa ajali. Abiria ambao pia wanabebwa nao hawawezi kuvaa hizo kofia. Hawana nguo ambazo zinaweza kuonyesha mtu usiku kuwa ...
view
15 Oct 2014 in National Assembly:
Kwa haya machache, naunga mkono Hoja hii ili ipate kuwasaidie vijana wetu huko mashinani.
view
14 Oct 2014 in National Assembly:
Mhe. Spika, naomba nitoe mchango wangu kuhusu Hoja hii. Kitu cha kwanza, hata huenda ikawa wengi wa Wabunge ambao wako hapa, walisoma kupitia michango ya harambee. Ninajua kwamba ndugu yangu, Chris Wamalwa, alisomeshwa kwa Harambee. Hata ndani ya hili Bunge leo, tuna wageni ambao ni wanafunzi. Nimewaona huko juu kwa gallery ; wengi wao wanasomeshwa na fedha za Harambee. Wabunge wamejitoa muhanga ili kusomesha ndugu zao, watoto wa dada zao ama kaka zao. Kwa hivyo, kusema kuwa kuweko kwa Harambee kunaua ule moyo wa kutoa wa wananchi wetu si sawa; ninakubaliana na msemaji wa hapo awali. Alisema hata juu ya ...
view
14 Oct 2014 in National Assembly:
zangu, nina nia ya kumsaidia mtu fulani, nani hapa nchini anaweza kunizuia kumsaidia mtu fulani? Hata Jumapili ijayo, Rais atakuwa katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni, na atakuwa anachangisha pesa. Mnataka kuniambia nisiende nikachangie shule? Mimi naye tutapelekwa kortini? Kama vile mwenzangu amesema, ni kweli kuwa hiyo barua ina ubaguzi. Imelenga Wabunge peke yao; imeacha watu wengine. Naomba tuangalie hilo jambo vizuri; ikiwa Wabunge wamejitolea kutoa mchango wao kusaidia wagonjwa, shule na kadhalika wasiwekewe vikwazo na mtu yeyote. Naomba ndugu yetu wakati huu aanze kufikiria mwenzake. Alianza kuzozana na Wabunge katika Bunge la Kumi na kilichompata kilikuwa ni kuondolewa kutoka ...
view
14 Oct 2014 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, wacha nione kama ninaweza kufanya vizuri zaidi kuliko Mheshimiwa ambaye ametangulia. Ningependa kutoa maoni yangu kuhusu maswala haya ambayo yametokea kuhusu Makatibu wa Wizara kuja mbele ya Kamati ya Bunge – Kamati ambayo imeteuliwa ili kujihuzisha ama kuwahuzisha Wabunge wote ili waje waelezwe waziwazi yanayojiri katika Wizara zao.
view
14 Oct 2014 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kabla zijaenda mbali naomba kuchukua nafasi hii kwa heshima yako nitoe rambirambi zangu kwa mwanakenya Professa Ali Mazrui ambaye ametuacha akiwa ni mtu mwenye sifa ambaye ameheshimika ulimwengu wote mzima na amepatia nchi hii sifa. Naomba mwenyezi Mungu aiweke roho yake pahali pema peponi.
view
14 Oct 2014 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, Spika ameeleza wazi kuwa kukutana na Makatibu Wakuu hapa hakumaanishi kuwa wanaingia Bungeni. Ni sababu tumekosa sebule kubwa ambapo tunaweza kukutana na wao vile wanavyokutana na kamati kila wakati. Tungekuwa tuko na nafasi kubwa hatungekutana hapa. Tungekutana pahali pengine lakini kwa sababu hiyo, imebidi waje hapa. Swala la kushangaza ni huu uoga umetokea wapi?
view
14 Oct 2014 in National Assembly:
Kama Katibu wa Wizara, Mhesimiwa Charity Ngilu amekuja hapa akajieleza na wenzake wawili walionekana hapa basi kilichowafanya watoweke ni nini? Ni uoga ama nikutuheshimu Bunge ama nini kimetokea? Ndio maana nilikuwa naomba Kiranja wa Walio Wengi Bungeni na Walio Wachache--- Naomba nifafanue, sisi mrengo wetu mnatuita wachache hapa Bungeni lakini uko nje ndio tulio wengi. Kwa hivyo, Kiranja wa Walio Wengi ndani ya Bunge ningeomba afafanulie Bunge ni nini kimewafanya hawa wenzetu Makatibu wakaondoka bila kuja kufafanulia Bunge yale ambayo walikuwa wameitiwa. Hata kama walikuwa wanaondoka wangeomba radhi. Wangeeleza, “mna mambo yametokea dharura na inatubidi tuondoke na tunaomba msamaha ili ...
view