Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 361 to 370 of 604.

  • 14 Oct 2014 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ni ombi langu kuwa hawa waje tena wajieleze na wachukuliwe sheria za kinidhamu. Mwenzangu Mheshimiwa Nyokabi alisema kuwa Serikali hii ya Jubilee iko katika nguzo za uwajibikaji na uwazi. Nashukuru na ni vizuri. Kama iko katika nguzo za uwajibikaji na uwazi mbona watu wao hivi leo asubuhi wakaogopa kuja mbele ya kamati ya Bunge? Walikuwa wamepata wakati unaofaa waje wajieleze na waonyeshe kuwa Serikali ya Jubilee imefanya hili na inataka kutekeleza haya na hatufichi chochote lakini huu uoga umetokea wapi? Ni nini wanachoficha? view
  • 14 Oct 2014 in National Assembly: Nakubaliana na Mheshimiwa ambaye amesema hata hizi kamati za Bunge ambazo tumeziunda, wakati mwingine lazima ziwe zenyewe zina sifa. Wale ambao wamepelekwa kamati fulani, kama ni kamati ya sheria je tuko na wanasheria wangapi pale ili waweze kuingia kina cha kisheria na waweze kuwauliza hao maswali? Mara nyingi unakuta tumepeana kamati na yule ambaye amepelekwa kwa kamati fulani hana ufahamu, uwezo na majukumu. Anaenda tuu pale kujionyesha kisha anaondoka. Naomba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 14 Oct 2014 in National Assembly: tuchukue nafasi hii hata hizi kamati nazo tuziangalia upya na tuone ni wapi watu wanaweza kuwajibika. view
  • 14 Oct 2014 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, nashukuru Mheshimiwa Ngilu kwa kuja hapa lakini wakati huo alipokuwa anajibu, yale yalikuwa yanakuja kwangu ni “Karen kuna utata”. Wao wenyewe wamesema hii ardhi ni ya mtu mwingine. National Land Commission imesema hii ardhi ni ya mtu mwingine. Ukweli uko wapi? view
  • 14 Oct 2014 in National Assembly: Wakati kama huu, vile Mheshimiwa amesema, ni mchache mno wakuweza kutoa maswala kama haya bayana yakabainika waziwazi kuwa yanaweza kujibiwa. Kwa hivyo, tunaomba, ijapokuwa muda huu umetolewa kamati pia ziendelee na kazi zao ambazo zinahitajika kufanya. view
  • 14 Oct 2014 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, tulikuwa na kikao hapa Jumatatu iliyopita ambacho kiliandaliwa na Mheshimiwa Spika. Makatibu wa Wizara wakaja wote na wakaelezwa kwa nini tumebadilisha sheria zetu za Bunge. Wanakuja kwa kamati andalizi ya Wabunge wote ili wajieleze. Wakafafanuliwa kila kitu. Jana na leo katika magazeti tunasoma kuwa mmoja wa Makatibu ambaye ni kinara wa Jubilee anawaomba hawa Makatibu wa Wizara wasije Bungeni. Yeye mwenyewe kwa nini awaelekeze? Kwa hivyo, kuna utata mkubwa ambao tungeomba Bunge iutatue. Inafaa wafahamu kuwa wakija hapa ni kujibu maswala ambayo Wabunge wangependa yafafanuliwe. Kwa haya mengi Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, naomba kuweka ... view
  • 10 Sep 2014 in National Assembly: Jambo la nidhamu, mhe. Spika. ingawa wamenipatia wadhifa wa Kiranja hapa Bungeni, siwezi kuwa Kiranja na nikubali matamshi ambayo hayawezi kuthibitishwa. Wataita wameonewa hata wakati huu. Siwezi kuunga mkono hata mtu mmoja kwa sababu hakuna Mtaita hata mmoja ambaye amepewa wadhifa. Kwa hivyo, siwezi kuunga mkono, na hamna--- view
  • 12 Aug 2014 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe mchango wangu kwa Mswada huu wa Mapato. Huu ni Mswada muhimu sana kwa nchi yetu na unafaa uangaliwe kwa makini sana. Kila Mbunge anahitajika na anatakiwa atafakari ni wapi Mswada huu unatupeleka na matokeo yake yatakuwa yapi. Nikitoa maoni yangu kuhusu Mswada huu, naomba nichukue nafasi hii kwanza, kukishukuru chama changu cha Orange Democratic Movement (ODM) na muungano wa CORD kwa ujumla kwa kunitunukia nafasi ya kuwa kiranja wa walio wachache Bungeni na walio wengi nchini. Hii ni kwa sababu sisi ndio tulio wengi nchini lakini hapa Bungeni, tuko wachache. ... view
  • 12 Aug 2014 in National Assembly: Na tuliongeza mmoja jana, ijapokwa sikuwa hapa nchini. Tumeongeza moja kutoka eneo la Uwakilishi Bungeni la Mathare. Nashukuru kila mmoja aliyehusika na shughuli hiyo. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimshukuru aliyekuwa kiranja wa walio wachache Bungeni, Mhe. Mung’aro kwa kazi alizozifanya wakati alikuwa katika kiti cha kiranja wa walio wachache Bungeni. Namshukuru kwa kazi zake na namtakia kila la heri. Naomba wenzangu wa muungano wa CORD tushirikiane na tuangalie hawa ndugu zetu wa Muungano wa Jubilee. Tunaenda nao kwa safu moja kwa moja. Pale ambapo hawatekelezi wajibu wao, tunawakosoa yakutosha kwa sababu ni wajibu wao. Mara nyingi, kuna utelezi na utetezi. ... view
  • 12 Aug 2014 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika, tukiangalia Mswada huu katika kipengele cha pili hadi cha 24, vipengele hivi vyote vimependekeza mageuzo fulani ya kutafuta ushuru. Mbinu hizi ni muhimu. Hizi mbinu zilingane na mahitaji ya nchi. Hizi mbinu za kutatufa hela ni muhimu. Lazima tuzingatie vile tutakavyoweza kuinua kiwango cha maisha cha watu wetu. Tukiangalia nchi nzima, utakuta kwamba, mara nyingi, usambazaji wa miradi umegemea upande fulani. Tungependa kurekebisha hayo na ndio maana tukaomba ugatuzi katika Kenya. Ijapokuwa ugatuzi umeingia, bado kuna changamoto za vile hela zinavyotumiwa mashinani, hasa tukiangalia vile magavana wengine wanavyotumia pesa. Hawataki kujibu vile fedha zinavyotumiwa.. Mhe. Naibu Spika, ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus