Zuleikha Juma Hassan

Parties & Coalitions

Born

10th August 1979

Post

P. O. Box 169 - 80133 Mariakani

Email

akinatanga@yahoo.co.uk

Telephone

0705403237

Telephone

0721400882

Zuleikha Juma Hassan

Zuleikha is grateful that her father’s postings abroad exposed her to a myriad of opportunities, which impacted on her life positively. While studying in South Africa, she recalls that she went through the stages of anger over apartheid. The realization of Zuleikha that one needed to be in politics to influence policy formulation prompted her to join politics. Initially, Zuleikha sought the Kaloleni parliamentary seat but was dissuaded. In parliament she has pushed the government to fund the National Youth Council.

All parliamentary appearances

Entries 121 to 130 of 309.

  • 9 Mar 2016 in National Assembly: Asante, Bwana Spika kwa nafasi hii ya kuzungumzia Mswada huu. Ninauunga mkono. Ninaomba upitishwe kwa sababu tumekuwa tukipata shida sana tangu enzi za Uhuru hadi sasa hapa nchini, hususan sehemu nyingi za Mkoa wa Pwani. Uenezaji wa umeme umekuwa ukifuata sanasana barabara za lami. Watu ambao wanaishi karibu na hapo ndio wamekuwa wakipata sitima. Wananchi wengine wamekuwa wakiachwa kwa giza kwa siku nyingi licha ya kuwa na huo mpango wa kuleta stima katika sehemu ambazo ziko ndanindani na ni za mashambani. Bado kuna watu wengi ambao wako nyuma kiuchumi kwa sababu hakuna stima ya kutosha. Pia, inaonekana kama sehemu nyingine ... view
  • 9 Mar 2016 in National Assembly: Hon. Temporary Deputy Chairman, please repeat your question about creation and science. view
  • 9 Mar 2016 in National Assembly: That is straightforward. According to Islamic religion, creation is by God. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia kuhusu hii sheria ambayo itaweza kuwasaidia maskini kupata msaada wa mawakili wa Serikali. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Hii sheria ingepitishwa kama juzi. Kwa hakika, ni miaka 50 tangu tupate Uhuru. Pia, ni vizuri kuwa tumeweza kufungua macho yetu kwa wakati huu kuweza kuleta sheria kama hii humu chini. Kwa mfano, hata leo, nimepigiwa simu na mama mmoja kutoka Kaunti ya Kwale The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: ambaye mtoto wake amebakwa. Kijana mshukiwa alishikwa kisha akawachiliwa. Kesi ni kesho na haelewi atafanya nini ama ataenda vipi kumsaidia mtoto wake na yeye mwenyewe waweze kupata haki. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Kwa hivyo, tukiwa na mawakili ambao wanalipwa na Serikali itawasaidia sana wale walalahoi nchini kwetu ili kupata msaada, hususan wale ambao wanadhulumiwa kiasi kama hicho na zaidi. Kwa mfano, pia, kuna wanawake wengi Kwale ambao mara kwa mara wanakuja kwa sisi viongozi wakitaka msaada kuwatoa vijana wao ambao wameshikwa na wamefungwa gerezani na hawajui vipi watawatetea watoto wao. Wengi ambao wanashikwa huwa ni vijana wa kiume kwa bahati mbaya na afisa wetu wa polisi kwa maswala ambayo hayaeleweki mara nyingi, katika mambo ambayo tunayaita misako. Maafisa wa polisi wakimpata kijana anatembea tu, wanamshika. Wakati mwingine wanamua kwa muda kushika watu ... view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Kitu ambacho nitaomba kibadilishwe, na pamoja na wenzangu tutaleta mabadilisho, ni Ibara 9(a) ambayo inasema kuwa Rais aweze kuandika mkurugezi wa bodi ambayo itasimamia sheria hii. Tunaona ni afadhali Jaji Mkuu aweze kumchagua atakayesimamia bodi kama hii. Pia, tunaona kuwa Wakili Mkuu wa Serikali amewekwa hapa pamoja na Wizara ya Haki, ambayo hivi sasa hatuna. Kwa hivyo, pengine angewachwa mmoja peke yake. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Kuna jambo lingine ambalo limenifurahisha sana. Huko Kwale, tuna kabila linaloitwa Makonde. Makonde ni watu ambao wanatoka Mozambique ambao walikuwa hapo miaka na mikaka. Wamezaliwa hapo na wanaishi hapo. Jambo la kusikitisha ni kuwa Serikali ya Kenya bado haijaamua kuwatambua watu hawa ijapokuwa hivi sasa tuko kwenye harakati za kuwasaidia watambulike kama Wakenya. Karibu wote hawajui vile watarudi. Hawana mtu wanaomjua huko na nchi yao ni Kenya. Hivi sasa, hawana vitambulisho na hawatambuliki kabisa. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Jambo nzuri katika sheria hii ni kuwa watu ambao hawana nchi ama kwa Kiingereza “stateless persons”, wataweza kupata msaada wa mawakili ili kusaidika katika kesi zao tofauti tofauti. Pia, ingekuwa vizuri kama wangeweza kupata msaada ili kuwatetea pia wao waweze kutambulika kama Wakenya. Makonde hapa nchini wako kama 10,000, watu wengi sana ambao wanaumia na wameoana na Wakenya hapa nchini. Watoto wao wanapata shida wakitaka kuandika karatasi za usajili wa kuzaliwa, kupata vitambulisho au hati za kusafiria kwa sababu pengine mzazi wao mmoja hatambuliki kama Mkenya. Kabla sijaketi, ningetaka kuiomba, kwa sababu nina hakika hii sheria itapita katika muda usio ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus