Zuleikha Juma Hassan

Parties & Coalitions

Born

10th August 1979

Post

P. O. Box 169 - 80133 Mariakani

Email

akinatanga@yahoo.co.uk

Telephone

0705403237

Telephone

0721400882

Zuleikha Juma Hassan

Zuleikha is grateful that her father’s postings abroad exposed her to a myriad of opportunities, which impacted on her life positively. While studying in South Africa, she recalls that she went through the stages of anger over apartheid. The realization of Zuleikha that one needed to be in politics to influence policy formulation prompted her to join politics. Initially, Zuleikha sought the Kaloleni parliamentary seat but was dissuaded. In parliament she has pushed the government to fund the National Youth Council.

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 309.

  • 17 Jun 2021 in National Assembly: (Kwale (CWR), ODM): Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I want more time to prepare to contribute in a few minutes. Maybe you can give another Member and then I will contribute later. Thank you. view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii ya kuchangia Mswada kuhusu fedha zitakazopewa serikali za kaunti katika mwaka wa 2021/2022. Mwanzo, naunga mkono Mswada huu kwa sababu pesa sahihi zinakwenda mashinani tangu tupitishe Katiba mpya mwaka wa 2010. Ninasema hivyo kwa sababu sa hii Wapwani hatuna haja tena ya kusema kuwa Pwani si Kenya. Sa hii tunapata mabillioni ya pesa kila mwaka na tunachagua viongozi miongoni mwetu ambao wanasimamia miradi muhimu ya msingi. Hatuna haja tena ya kumngoja Mtukufu Rais aje mashinani ili tumuombe vitu vidogo vidogo kama miradi ya maji, shule za chekechea na pia hospitali ... view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Naomba magavana pia wawe wabunifu. Mumeskia Wabunge wengine wamesema kuwa view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: za kitambo zilikuwa zinakusanya fedha zaidi kuliko serikali za kaunti ilhali serikali za kaunti zina nguvu na mamlaka zaidi kuliko kamati za councils za hapo awali kabla hatujabadilisha Katiba. Wawe wabunifu na waangalie mifano ya magavana wengine humu humu Kenya ambao wametengeneza mitambo ambayo imeongeza thamani ya bidhaa zao, kwa mfano, maembe, maziwa na kadhalika. Bidhaa na mimea za wananchi katika hizo kaunti zimepata soko na zimeleta bei nzuri. Hiyo imeweka pesa nzuri katika mifuko ya wananchi ili waweze kujikimu kimaisha na gharama zao ndogo ndogo za maisha. Viwanda pia vinazalisha kazi. Tunajua ajira ni changamoto kubwa sana nchini mwetu ... view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Kwa hivyo, magavana wawache hii tabia ya kudanganya wananchi kuhusu majukumu yao na vile serikali inavyofanya na kuzidi kuwatatiza. Pia, nawasihi magavana mwaka huu na miaka ijayo wawekeze zaidi kwa vile vitu ambavyo ni muhimu kwa wananchi kama maji. Wamepewa jukumu hili. Mvua imechelewa hivi sasa. Kuna sehemu nchini ambapo watu wanakunywa maji ya chumvi. Unasikia hadithi kuwa watoto wanakunywa maji ya chumvi mpaka wanatapika, kwa sababu hakuna maji masafi. Tumekuwa na ugatuzi karibu miaka kumi. Hili ni jambo la kusikitisha. Magavana wanasikia habari hizi lakini hawapeleki maji ya kusaidia kwa dharura. Wamekaa tu kimya wananchi wakipata taabu na hilo ... view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Magavana wawekeze katika masuala ya afya kwa sababu mengi yamegatuliwa. Hakuna dawa katika hospitali. Madaktari hawatoshi. Shida ya magavana wengi ni kujenga zahanati na hospitali kila pembe za kaunti. Wanaongeza zahanati lakini zile ambazo ziko hazina dawa na madaktari wa kutosha. Nashangaa kwa nini wanataka kuweka mijengo mingi bila kupeana huduma katika sehemu hizo. view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu pesa ambazo zitapelekwa mashinani zimeongezwa. Zitasaidia sana. Kuna baadhi ya viongozi ambao wamesema pesa zisigatuliwe kwa sababu kuna ufisadi sana katika serikali za ugatuzi. Pesa zigatuliwe. Iwe jukumu la wananchi kuhakikisha kuwa wanapigia kura gavana na serikali ya kaunti ambayo inafaa, inajali wananchi na ambayo haitakuwa na ufisadi. Pesa iwe pale kwa kaunti ili ifanye masuala mazuri, iwapo tutapata viongozi wazuri. view
  • 16 Jun 2021 in National Assembly: Asante. view
  • 13 May 2021 in National Assembly: Kisiwa. view
  • 13 May 2021 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alisema kwamba uongozi ni kuoyesha njia na sio kufunga njia. Nafikiri ni somo kubwa sote viongozi. Pili, sasa nimekuwa na moyo kuwa shida za biashara kubwa na ndogo ndogo kama za boda boda katika mpaka wetu wa Horo Horo ulioko Kaunti ya Kwale zitaisha. Alisema tushikane na tuungane naye ili tuweze kupitisha yale maswala aliyotuambia ya kusaidia nchi zetu mbili katika biashara na utalii. Asante sana. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus