Andrew Mwadime

Parties & Coalitions

Email

achawia@yahoo.com

Telephone

0722867598

All parliamentary appearances

Entries 121 to 130 of 443.

  • 13 Mar 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I rise to ask the Cabinet Secretary for Water and Sanitation the following Question: What plans has the Ministry put in place to construct dams and pans in Mwatate Constituency for provision of water for livestock and for household use? view
  • 13 Mar 2019 in National Assembly: I thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker view
  • 6 Mar 2019 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Spika kwa hii fursa. Nimesimama kuunga mkono malalamishi haya ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu. Ni leo tu asubuhi mkazi mmoja wa eneo Bunge langu amenitumia barua kwa njia ya nukishi akilalamika kwamba yeye ni mgonjwa na hali yake ni mbaya. Kwa wale ambao hawaelewi, nukishi ni fax . Ni kweli kwamba wengi wao ambao walistaafu mwaka wa 1997 walikuwa ni wazee na hela hii imechelewa. Ninaomba Kamati ambayo inashughulikia suala hili iharakishe. Mwaka jana mwezi wa tano, tulikutana na wale waliostaafu 1997. Wengi wao wamekomaa na ni wazee. Wanadai hela yao ambayo ni haki yao. Ingekuwa ni vyema ... view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Mwanzo kabisa, naunga mkono Hoja hii. Sura ya nchi ni lishe bora, mazingira bora na matibabu bora. Vilevile, kabla sijasahau, ni vyema Bunge hili lifikirie sana sheria za nidhamu kwa sababu kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza iko kila mahali. Ndio maana Bunge la Tanzania limechangamka kuliko hili letu kwa sababu Wabunge wengi hawawezi kuongea Kiingereza moja kwa moja na pia hawawezi kuongea Kiswahili moja kwa moja. Hiyo ni changamoto. Kando na changamoto za lishe bora na mazingira bora, matibabu nchini yamekuwa kizaazaa kikubwa mno. Sasa hivi, Wabunge wengi wanatumia ... view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: kwa sababu hakuna mpangilio sawasawa. Kungekuwa na mpangilio sawasawa na ufujaji usiwepo, Serikali ingekuwa inaweza kutibu watu wake bila hata kuomba hela za madawa au za matibabu na hata kama unahifadhi mwili mtu anapofariki. Sisi tumelegea katika upande huo. Hela inayohitajika kutibu Wakenya wote haiwezi kuzidi Sh500 bilioni. Haya ni mahitaji ya kila mwananchi. Sasa hivi ukiangalia hospitali zote nchini, sio za rufaa tu bali hata zile za umma kule mashinani, taabu ni hizo hizo. Kwangu nyumbani niko karibu na zahanati nyingine hapo. Ni kizaazaa. Hamna hata kutulia. Hili ni suala ambalo watu wanafaa kulichukulia kwa undani na walifikirie sawasawa. ... view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Mwanzo kabisa, nasimama kuunga mkono marekebisho haya. Kilimo ni miongoni mwa sekta ambazo ziko rohoni mwa majimbo yote ya Kenya. Ugatuzi ni kitu ambacho Wakenya walipigania na tumeona maendeleo ya ugatuzi. Ingawaje kuna madoadoa hapa na pale kwa sababu ya rushwa, ugatuzi bado umewasaidia Wakenya wengi isipokuwa mfumo wa ugavi wa huu mgao ambao tunatumia sasa hivi kidogo uko na dosari. Nikiangalia, kuna majimbo kutoka tangu tupate Uhuru mwaka wa 1963 ambayo bado hayana maji na ukiangalia katika majimbo mengine, wana maji yakutosha yakunywa na yakufanya unyunyizaji mashambani mwao. Wengine ... view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Sasa hivi nilikuwa na angalia rununu yangu. Ukiniruhusu nitadokeza kuhusu niliyoona katika WhatsApp . Mmoja amesema: “Usifananishe maendeleo ya Taita Taveta na Kaunti ya Kitui. Usitofautishe maendeleo ya Taita Taveta na Kaunti ya Kwale.” Lakini ukiangalia ugavi wa Kwale na ule wa Kitui ni mkubwa kuliko ule wa Taita Taveta. Kwa hivyo, huwezi kufananisha maendeleo ya majimbo haya na majimbo mengine ambayo yanapata hela kidogo, haswa Taita Taveta maana jimbo ni kubwa na linataka hela nyingi. Mfumo ungetengenezwa ikawa kwamba kama ni dawa, mahali kuna watu wengi basi Seneti ingetengeneza kwamba jimbo ambalo lina watu wengi lipelekewe pesa nyingi za ... view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Sasa hivi utakuta kwamba majimbo ambayo yanapata hela nyingi za barabara bado hela nyingi zinazidi kupelekwa kwao na zile zinapata mgao mdogo ndio zinazidi kuumia. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono marekebisho haya lakini Seneti ijaribu kufikira njia mwafaka ambayo inaweza kusaidia majimbo yote ya Kenya yawe sawa. Nashukuru kwa kunipa fursa hii. view
  • 5 Dec 2018 in National Assembly: I would like to ask the Cabinet Secretary for Water and Sanitation the following Question: a) Could the Cabinet Secretary provide a list and details of water projects, including cost of each project in Mwatate Constituency? b) What is the status of funds set aside for water projects in Mwatate Constituency in the Financial Years 2013/2014, 2014/2015, 2015/2016 and 2016/2017? c) Could the Cabinet Secretary consider providing water for irrigation to the people of Mwatate Constituency? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus