Danson Mwashako Mwakuwona

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 197.

  • 4 Mar 2020 in National Assembly: Asante, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nzuri ya kuchangia mjadala huu ambao umeletwa na mwenzangu wa Mwatate. Ningependa kumpongeza Mheshimiwa Mwadime kwa kutuletea Mswada mzuri kuhusu huduma za umma au public service kwa Kimombo. Itaangalia wananchi wote katika maeneo yote ya nchi na kuhakikisha kwamba kila mmoja anajihisi kuwa ana nafasi sawa ya uajiri katika nchi yetu. Katika Kenya hii Mungu alitubariki na makabila 43. Imekuwa jambo la kustaajabisha kuwa uajiri katika nchi yetu haujatilia maanani kila mmoja apate nafasi ya sawa. Naunga mkono Mswada huu. Kamati ya Uwiano na Utangamano huchapisha kila mwaka ripoti kuhusu jinsi idara ... view
  • 4 Mar 2020 in National Assembly: Nilikuwa ninazungumza na Mhe. Mwadime nikimweleza kuwa nitaleta mapendekezo ya marekebisho. Hoja hii haijataja vitengo vya usalama. Kwa kweli, jeshi na polisi huajiri vijana kutoka kila eneo bunge. Lakini, baada ya vijana hawa kuchukuliwa, wawe wawili ama watatu kutoka kwenye kata, bado huwa kuna watu ambao hujiunga na kikosi cha polisi ama jeshi kupitia milango ambayo imefunguliwa na wale wanaoshikilia nyadhifa za juu. Nitaleta mapendekezo ili jeshi na vitengo vinginevyo vya usalama navyo vituletee ripoti hizi. view
  • 4 Mar 2020 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda nitokako, najua Wabunge wengi wanakumbana na shida hii, vijana wanakosa tamaa. Wao huenda kwa wingi, mamia na maelfu, kupambana ili kujaribu kujiunga na vikosi vya jeshi ama polisi. Ni aibu kwa kuwa ni wawili ama watatu tu wanaochukuliwa kati ya vijana elfu mbili wanaojitokeza. Vijana hao huja kwetu sisi Wabunge kuomba wafanyiwe mipango. Zamani, Wabunge walikuwa wanapewa nafasi mbili au tatu kuwaingiza watu katika vitengo vya usalama—leo hii tunajua hali si hiyo. Maanake Wabunge tuko wengi, hatuwezi pewa nafasi hata moja kwa kuwa tutachukua watu bila hata kuenda kwa wananchi. view
  • 4 Mar 2020 in National Assembly: Kwa hivo, jeshi na vitengo vingine vya usalama lazima viwe hapa. Wakati wanapoajiri watu, wacha tujue ni watu wangapi wamechukuliwa katika kila kata. Hivyo tutaweza kutoa ripoti kwa wananchi waliotuchagua. Tutawaambia waliochukuliwa. view
  • 4 Mar 2020 in National Assembly: Mwisho, kwa sababu ya muda, inasitikisha sana maana idara kama Kenya Ports Authority (KPA) zamani, kazi zilikuwa zinagawanywa kulingana na usawa wa Kenya. Lakini leo wanaongoza kule juu… Ningependekeza kwamba Bunge hili lingeamuru tufanyiwe audit for thelast five years ya watu ambao wameajiriwa katika bandari ya Mombasa. Mhe. Naibu Spika wa Muda, utashangaa kuwa kwa wale walioajiriwa, asilimia 90… Niko na statistics. Hata kazi za kufagia, kazi ambazo ni za chini kabisa, watu wanatolewa bara kuja kukomboa nyumba Mombasa ili waweze kupata ajira bandarini. view
  • 4 Mar 2020 in National Assembly: Katika kitengo cha Inland Container Depot hapo Mombasa vilevile, utakuta mambo yale yale. Kenya yetu, nashukuru kwa ajili ya handshake, BBI itaweza kutusaidia. Nikisikia mtu akisema hatuhitaji BBI, nashangaa maanake, suala hili tunazungumzia leo ni baadhi ya maswala ambayo yameangaziwa sana katika BBI. Kuna masuala ya kujihisi kuwa Wakenya; kupambana na ukabila; ukosefu wa kazi na shared prosperity . Wacha Mtaita wa Wundanyi aliyehitimu na shahada awe na nafasi sawa na yule Mkenya anayetoka Kisumu, Nyeri, Nakuru au Giriama ili Kenya iwe bora. Mtu anapoenda interview, wacha bidii yake na uzoefu wake wa kujieleza uwe ndio nguzo yake ya kumpatia ... view
  • 10 Feb 2020 in National Assembly: Asante Mhe. Spika. Nasimama kutoa rambirambi zangu binafsi, za familia yangu na za watu wa Wundanyi na Taita/Taveta kwa jumla kwa kumpoteza aliyekuwa Rais wa nchi hii, hayati Daniel Toroitich arap Moi. Nilifaidika sana na Maziwa ya Nyayo. Kwenda shule Jumatatu, Jumatano na Ijumaa wakati ule ilikuwa ni lazima kwa sababu tulipewa maziwa siku hizo. Mpaka nilipokuwa mtu mzima, sijaona maziwa yaliyo na kile kwa Kiingereza kinaita ‘cream’. Ilikuwa unapasua lile boksi ukimaliza kunywa maziwa unapata ‘cream’ nzuri sana. Naomba mwenyezi Mungu alaze roho yake mahali pema peponi. view
  • 26 Nov 2019 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika. Wakati Mhe. Millie Odhiambo alipokuwa akiitisha hoja ya nidhamu, tulingoja tusikie ni gani. Leo ametaja chura kwamba wengine ni wanadamu lakini wengine ni chura. Sikuelewa ilitokea wapi lakini tunamuelewa maana yeye ni gwiji katika mambo ya Bunge. Ninasimama kuunga mkono mjadala huu ambao umeletwa ndani ya Bunge kuongea masuala ambayo yamekumba nchi yetu haswa masuala ambayo yanafungamana na lile janga ambalo limetokea kule West Pokot, kaunti ambayo Mhe. Moroto anatoka. Nampongeza sana. Kama mzee na mheshimiwa wa Bunge hili, ameleta jambo hili ambalo limeangaziwa sana katika vyombo vya habari. Bunge la Taifa limepata nafasi nzuri ya ... view
  • 26 Nov 2019 in National Assembly: Mimi ambaye ninatoka maeneo yale ya miinuko kama kule Taita na Wundanyi, tumepata taabu kubwa. Kule kwangu, juzi tulipoteza mtoto mdogo ambaye nyumba yao ilisukumwa na maporomoko ya ardhi. Leo hii, tunavyoongea hapa, mchana wa leo, kulikuwa na kamati ya kushughulikia majanga kule kwangu Wundanyi ikiongozwa na mkuu wa kata ndogo ya Wundanyi, Taita, wakitathmini hasara iliyoletwa na maporomoko yale. Mhe. Naibu Spika, naomba kukujuza. Asilimia 60 ya Eneo Bunge langu la Wundanyi ni miinuko ambayo wakati mvua ilipoanza kunyesha, leo hii nina familia 170 ambazo zimeathirika sana na masuala haya. Nashukuru juzi niliongea na Waziri Matiangi na kumjulisha kwamba ... view
  • 6 Nov 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. I rise to ask Question No. 476 of 2019 to the Teachers Service Commission: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus