All parliamentary appearances
Entries 51 to 60 of 973.
-
18 Feb 2025 in Senate:
Mhe. Malulu ulisomea chuo kikuu nilichosomea. Uliweza kuwa mwenye kiti almashauri na bodi za shule nikiwa mwalimu. Ulipigania watu wako, ujenzi wa miundo mbinu shule na barabara. Ulikuwa mkatoliki wa imani. Tulitunga sheria za ufugaji na upanzi wa miwa na usagaji wa sukari tukitaraji kuwa wakulima wako wa Malava watanufaika. Tulikuwa kwako na Mhe. Rais. Tukapeana shule ya nua ya Chanderema. Wewe ulikuwa unajua ya kwamba watoto wetu wakinufaika katika masomo, siku zao za usoni zitakuwa salama. Mhe. Malulu, tembea salama. Luwere luwere mwana wa mama, tutakutana Mungu akipenda. Asante sana na Mungu awalinde.
view
-
13 Feb 2025 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ningependa kusisitiza kuhusu Taarifa ambayo Sen. Faki ameleta hapa kuhusiana na hali ya afya katika Kaunti ya Mombasa. Coast General Teaching and Referral Hospital ina mapacha katika kaunti tofauti ambao wanafanana kabisa. Tulizungumzia masuala ya matabibu wanaojitolea ambao hali yao ni ya kusononesha sana. Kuna wahudumu wengine katika hospitali zetu ambao kwa wiki kadhaa sasa wamekuwa kwenye migomo, zikiwemo kaunti za Kisii na Bungoma. Kaunti za Nairobi na Mombasa zinafanya mazoezi. Itakuwaje kaunti za humu nchini, ikiwemo Bungoma kuwa na mustakabali ama makubaliano ya kurejea kazini na kwamba kutakuwa na marupurupu ya kununua mavazi, kupandishwa vyeo ...
view
-
13 Feb 2025 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
-
13 Feb 2025 in Senate:
madaktari wako kwenye migomo ilhali magavana hawaoni kama kuna shida katika kaunti zao. Nashukuru Maulana kwa kunipa nafasi kuwa mwanakamati wa Kamati ya Afya katika Seneti. Tukiwa na Sen. Olekina pamoja na wengine tutalivalia njuga suala hili. Tunafaa kutembea katika kaunti hizi, kuwataja kwa majina na kuwaeleza kinagaubaga kadamnasi ya umma wale ambao kwa sasa wako katika nchi za ng’ambo kufanya utafiti na kuzuru miradi ya kule ilhali kwao nyumbani ni aibu tele na haitupi sisi moyo kwamba wao ni magavana. Baadhi ya hospitali zetu hazina dawa. Wamejenga hospitali gushi. Kuna majumba yasiokuwa na matabibu na madaktari. La muhimu ni ...
view
-
12 Feb 2025 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika wa Muda kwa nafasi hii ya kuchangia kwenye Kauli za Maseneta. Kauli ambayo Sen. Sifuna ameibua, nimekuwa nikizungumzia mara kwa mara. Kile ambacho nimeona matabibu hawa wa mashinani ni kwamba wako na rununu lakini kwenye mikoba ile hakuna dawa wala hamna pesa. Begi zile hazina ala za matumizi kama vifaa vya kupima damu na mambo kadhaa. Tulikuwa Kaunti ya Naivasha tukijadili kwamba iwapo Serikali itaweza kuongeza mgao wa fedha. Tunafaa tukubaliane kwamba fedha hizi zitatoka kwenye serikali kuu na italipa kwa awamu moja au fedha hizi zitaongezwa na serikali za kaunti zitakazolipa wafanyikazi hawa kwa awamu ...
view
-
12 Feb 2025 in Senate:
Mwisho kabisa nimeona hoja kuhusiana na Shirika la Reli humu nchini. Hio ni mali ya umma. Watu wamebomolewa vyumba na maeneo ya kazi katika kaunti hizi. Tunachotaka kujua ni kuwa wana mipango ipi ya kuhakikisha kwamba shamba zinazomilikiwa na reli ya nchi ya Kenya yanafanya mujibu wa Katiba? Kwa sababu tuna ugatuzi maeneo gatuzi ya humu nchini yanashirikiana vipi na Shirika la Reli kuwapa wanafanyikazi waliotayari kufanya biashara kwenye shamba ambayo hayatumiki kwa muda mrefu zaidi ya miaka 20? Watu wa mkoa wa magharibi na kaunti ya Bungoma wamesikia nikitaja mambo ya madaktari mashinani. Ninamuomba Gavana wa kaunti hii kwamba ...
view
-
11 Feb 2025 in Senate:
Bw. Naibu Spika, ninashukuru sana kwa nafasi hii. Vile vile ninashukuru kuona ndugu zangu ambao wamekuwa wakiukwea mlima sasa hivi wameteremka, wako katika Seneti.
view
-
11 Feb 2025 in Senate:
Waswahili husema “Kipandacho hushuka”. Mimi ninawashukuru Wakenya kwa kutupa nafasi kujumuika nao katika msimu wa Krismasi na mwaka mpya. Tumekuwa na kikao kule Naivasha kutathmini ratiba na mipangilio ya Seneti. Jambo la muhimu ni wale ambao wameteuliwa kuongoza Kamati ya Shughuli za Bunge watie maanani kwa sababu Seneti ni Bunge kuu; Bunge ambalo lina umarufu wa kutunga sheria. Mwaka huu lazima ibainike wazi mbichi na mbivu kuwa majukumu ya Seneti iko wazi kikatiba na kisiasa. Kusiwe na uzembe ambao tuliona mwaka uliyopita lakini tujue kuwa ni sharti tufanye kazi kwa pamoja. Kikundi hiki---
view
-
11 Feb 2025 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
-
11 Feb 2025 in Senate:
Bw. Naibu Spika, ninaomba viongozi wenzangu waweze kutulia. Wamechangamka kana kwamba wamekula aina fulani ya mmea na mmea huo unaweza kuwa sukuma wiki. Bw. Naibu Spika, nashukuru na ninaombea kila la kheri wale ambao wamechaguliwa na kwamba sisi pia tunataraji kwamba baadhi ya kamati za Bunge zitaweza kushughulikiwa ili ratiba zinazotoka ziweze kuuwiana na vikosi vya uchapakazi, ili tuweze kuwatendea Wakenya haki. Ni lazima kuwahakikishia kuwa popote walipo ya kwamba tutalinda ugatuzi na fedha zao. Uwajibikaji ni lazima ndio Wakenya wafurahie matunda ya ugatuzi. Mimi ninaomba Wakenya mahali popote walipo iwapo kuna tetezi na changamoto wasikose kututafuta sisi Maseneta kwa ...
view