Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 895.

  • 23 May 2024 in Senate: Bw. Naibu Spika, yule anayeomba nafasi ni kiongozi wa walala hoi. Nashukuru kwa nafasi hii na naomba kwamba, katika msimu huu wa mvua nyingi--- view
  • 23 May 2024 in Senate: Bw. Naibu Spika, sihitaji mwelekeo wake view
  • 23 May 2024 in Senate: Bw. Naibu wa Spika, inaashiria kuwa Seneta alikuwa anasinzia nilipokuwa natoa hoja zangu. Ndio mkoko unaalika maua. Mafuriko nchini humu yameathiri familia nyingi. Jana jioni kwenye Wadi ya Chesikaki katika Eneo Bunge la Mlima Elgon, kulikuwa na maporomoko ya ardhi ambayo yalifunika watu wanne wa jamii moja. Mmoja alipata majeruhi makubwa sana. Tunaeleza athari za mafuriko. Lazima serikali za kaunti ziwajibike katika matumizi ya fedha ambazo tunapeleka mashinani. Tunataka zionekane kuwa zinafanya kazi. Isiwe kwamba ni fedha ambazo zinatumika kufurahisha na kufanya viongozi kuishi maisha ya starehe. Kuanzia sasa, naomba sisi kama Seneti tuweze--- view
  • 23 May 2024 in Senate: Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir. I rise pursuant to Standing Order No.53 (1) to seek a statement from the Standing Committee on Labour and Social Welfare regarding staff at the management level at Kenya Seed Company. In the statement, the committee should: (1) Provide a detailed report of personnel at management level, including the current heads of departments at the Kenya Seed Company, their academic and professional qualifications, employment dates, the employment terms and disaggregated into contracts, permanent and pensionable as well as casual staff. Further, highlighting the ethnic composition within each category. (2) State the criteria used for ... view
  • 22 May 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa nafasi hii. Ningependa kuchangia taarifa ya bwawa la maji ambalo Seneta wa Kitui ameelezea. Ni muhimu Serikali inaporatibu na kuweka mipangilio ya kuwekeza katika sekta ya maji kuwahusisha washikadau wote kwa sababu wao ndio wamiliki wa rasilimali ambayo tunajadili sasa. Mwafrika ni mtu ambaye ana itikadi na historia yake. Ikiwa historia na itikadi zake haziwezi kuheshimika, ni dhahiri shahiri kwamba mtu huyo hana thamani yoyote. Hii ndio sababu naunga Seneta wa Kitui mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained ... view
  • 22 May 2024 in Senate: Kuna sehemu ambazo mababu waliotutangulia walizikwa na mahali walikuwa wanafanyia sherehe za kitamaduni. Maeneo hayo lazima yapewe kipaumbele katika kufidia serikali za kaunti na jamii husika. Pia kuna sehemu za ibada na mbuga za wanyama ambazo vile vile lazima zishughulikiwe. Serikali inapotaka kuwekeza katika kaunti hizo, ni lazima iwape watu hao kipaumbele. Bw. Naibu wa Spika, naomba upeane mwelekeo kwa Waziri husika katika sekta ya maji. Kando na bwawa ambalo tunajadili litanufaisha watu wa Tharaka Nithi na Kitui, kuna mabwawa mengine katika nchi ya Kenya ambayo Serikali ya Kenya Kwanza itaanzisha. Lazima wawajibike na kueleza nchi mikakati ambayo wataweka ili ... view
  • 22 May 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Namkaribisha Waziri wa Kilimo baada ya mchakato mgumu kuhusu pembejeo. Langu ni kuuliza Mhe. Waziri swali moja au mawili. Eneo la Magharibi, hasa Kaunti ya Bungoma, kuna upanzi wa kahawa. Juzi kumekuwa na madai na ishara kwamba kuna ulanguzi wa kahawa kutoka viwanda vya usagaji kahawa katika Kaunti ya Bungoma kuelekea nchi jirani. Pia, gharama ya ukuzaji wa kahawa katika nchi jirani ya Uganda ni bora zaidi kuliko nchi ya Kenya. Vile vile, wakulima wanadai kwamba mfumo wa malipo wa fedha za kahawa hauwapi motisha na nishati ya kufanya ukulima. Hivi kwamba, karibu ... view
  • 22 May 2024 in Senate: kwamba halmashauri na viwanda hazivunji pesa za wakulima. Pia fedha zilizopitishwa za view
  • 22 May 2024 in Senate: zinawafikia wakulima vitongojini kwa wakati unaostahili. Asante, Bw. Naibu Spika. view
  • 22 May 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Nitafanya jinsi umeelekeza ili nipate majibu kamili. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus