11 Nov 2020 in Senate:
Asante Bi Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kupinga Hoja iliyotolewa ili kuahirisha Bunge na kuweka siku moja kwa wiki. Vile msemaji aliyenitangulia, Seneta wa Kaunti ya Mombasa alivyosema, kwa hakika, hata siku moja tukikaa katika kikao hapa, kama maambukizi yatakuwa yanaendelea, basi hata hiyo siku moja, maambukizi yanaweza kuendelea. Tuko mwezi wa kumi na moja na tuko na kazi nyingi ambazo bado zinasalia katika Bunge. Tukipunguza kwa siku moja, hiyo inamaanisha kwamba, kazi nyingi ambayo ingeweza kufanyika mwaka huu itavuka kuenda mwaka ujao. Bi Spika wa Muda, mambo muhimu kama Building Bridges Initiative (BBI) saa hii inaendelea ...
view
11 Nov 2020 in Senate:
Wakenya wote pamoja. Imani yao ni Bunge hili la Seneti liweze kufanya kazi yake kwa siku tatu. Nilikuwa nikiomba leo yote ili niweze kuongea, lakini sikupata fursa hiyo. Hiyo inamaanisha kwamba, kuna msongamano wa maombi mengi katika Bunge hili. Ndio sababu sisi tunasalia kuendelea kuomba na hatupati nafasi hiyo. Bi. Spika wa Muda, kwa hivyo, tusijinyime hiyo haki ya kuzungumza mambo ya watu wetu katika Bunge hili. Mambo ya maambukizi ya COVID-19 kusema ukweli yako duniani kote. Mimi ninaona huu ugonjwa hautaondoka hapa nchini Kenya. Kama wakati ule tulifunga shule, vyuo vikuu, misikiti na makanisa ilhali huu ugonjwa bado unasambaa. ...
view
11 Nov 2020 in Senate:
Madam Temporary Speaker, equally, when the voting was going on, we had no quorum and I wanted to raise the same.
view
17 Sep 2020 in Senate:
Pole, Bw. Spika. Meza zilikuwa zimekaribiana nikabofia ya Sen. (Prof.) Kindiki. Katika Kaunti ya Tana River tumekuwa katika hali ya hofu kwa sababu kuna vijana walichukuliwa jinsi Sen. Farhiya alisema. Walikuwa wakiendesha gari za aina ya
view
17 Sep 2020 in Senate:
wakibeba abiria kutoka Hola mpaka Bura. Tangu vijana hao kuchukuliwa kutoka magari hayo na kupelekwa mahali ambapo hapajulikani, mpaka leo familia hizo ziko kwa majonzi. Kwa kweli, Sen. Haji ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya National Security,
view
17 Sep 2020 in Senate:
ambao pia mimi ni mwanachama tumekuwa tukimsumbua, Sen. Haji, tukimuuliza mahali ambapo watu wamepelekwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
17 Sep 2020 in Senate:
Ni vizuri kuwa Sen. Haji ameongea kinagaubaga leo na kusema kuwa Waziri wa Wizara ya Interior & Coordination of National Government aweze kuja mbele ya Seneti hii. Pia mimi kule Tana River County nasumbuliwa na watu ambao vijana wao wamekosekana katika hali ya sintofahamu. Bw. Spika, kuna mandugu wawili waliouwawa kinyama katika sehemu ya Mnazini. Waliuwawa usiku na watu waliojitambulisha kama polisi. Mpaka siku ya leo, sisi hatujui kama hao watu walikua polisi au walikua majambazi. Kwa hivyo, ni hali ya kutatanisha sana na tumekua katika hali ya hofu. Nikienda sehemu ya Mombasa kuna watu ambao wamekosekana mpaka leo na ...
view
16 Sep 2020 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Arifa ambayo imetolewa na Seneta wa Bungoma. Kwa kweli, vile rafiki yangu Seneta wa Mombasa alivyosema, kichwa cha kuku hakistahili kilemba. Ndipo unapoona hakika gavana huyu wa Kakamega anachukuwa hatamu za county zote za Kenya akisema ya kwamba, anatishia ya kwamba atapeleka watu katika likizo za lazima. Pia zahanati zote na mahospitali zifungwe. Hana habari ya kwamba Wakenya wengi maskini wanagharamikia pesa zao kwenda kupata matibabu katika hospitali hizi. Yeye akikaa huko Kakamega, akiwa na shida zake tele za Kakamega, anatupa hizo shida katika nchi nzima ya Kenya, ...
view
16 Sep 2020 in Senate:
Wewe kama umechaguliwa na magavana kama mwenyekiti, mkaenda mkakula mandazi na kunywa chai, ukaambiwa wewe ni chairman, wewe ni chairman we kuenda kukunywa chai na kuongea mambo yenyu.
view
16 Sep 2020 in Senate:
Jana wewe uliona Seneti ilikaa mbele ya Rais na kukupatia pesa ambazo hata hujui zimetoka wapi, wakati wewe mwenyewe unatangaza vita kwa Seneti. Wewe ndio unasafiri na ndege kubwa kubwa kuenda kwako huko, wakati Senators wanakupigania na wanakupatia pesa. Kwa hivyo, mtu ambaye akili yake ni timamu hawezi sema ugatuzi uvunjwe, ambapo wewe mwenyewe unafaidika na ugatuzi huo. Kwa hivyo, mimi ninasimama kideti hapa kuunga mkono Arifa ya rafiki yangu Sen. Moses Wetangula. Asante kwa kunipatia nafasi.
view