Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 272.

  • 6 Jul 2021 in Senate: Uchaguzi mkuu wa mwaka ujao hauko mbali. Lakini kwa sababu ya hofu ya COVID-19, Wakenya tayari wameambiwa wakae mbalimbali na wenzao. Mimi sioni kama huu uchaguzi utafanyika vizuri kwa sababu watu wanafaa kukaa mbali, wavae barakoya na hakuna chanjo za kutosha. Hali ikiendela hivi, watu watendelea kukaa mbali na kuwatenga wenzao. Siku ambayo wataambiwa waende kupiga kura, watauliza, “Mmetutahadharisha mwaka wote na sasa tuko na hofu. Tukienda kupiga kura, hali yetu itakuwa namna gani?” Sioni kama huo uchaguzi utafanyika vizuri mwaka ujao. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Ingekua vyema kama Serikali ingetenga pesa za kutosha ili wananchi wetu wapate chanjo. Hii ni kwa sababu kama wananchi hawatapata chanjo na hakuna tiba ya COVID-19, basi hofu tuliyonayo wakati huu itaendelea kutandaa na itafanya uchaguzi usiwe wa maana kwetu. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, siyo wananchi wote wanaovaa barakoya. Seheme ya mashinani ambako nimetoka, sijawahi kuwaona watu wetu wakivaa barakoya. Watu wanendelea na maisha yao ya kama kawaida. Mimi kama Seneta wao ndiye nilishuka gari langu kama nimevaa barakoya na wao waliniangalia na kushangaa sana. Waliniuliza, “Seneta, leo umefunga pua kabisa. Kuna nini limetokea upande wa Kenya ulikotoka?” Niliwauliza kwani bado wanaishi bila kuvaa barakoya na kukaa mbali, walinijibu kuwa hofu ya janga la COVID-19 haiko upande wao. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Afadhali wao wasiovaa barakoya kule mashinani--- view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Asante sana Sen. Pareno. Bi. Spika wa Muda, ninaomba unipe dakika moja tafadhali. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Lugha za Waorma na Wamaasai wakati mwingine zinataja mambo tofauti na vile yalivyo katika maandiko. Ni kweli ni barakoa wala siyo barakoya. Sawa, nimekubali. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, nilikuwa ninasema kuwa barakoa ambazo sisi tumevaa hazivaliwi kule mashinani. Watu wengine wanavaa hizi barakoa kwa sababu ya kuwaogopa polisi na kuwa wanaendelea na biashara zao. Wakiwaona polisi barabarani wanakumbuka kuvaa barakoa zao. Wanaweza kuokota barakoa yeyote barabarani na kuvaa bila kujali kama imetumika au la. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Ningependa kutoa wito kwa Serikali kutenga hela za kutosha ili watu wetu wapate chanjo. Ata tusikae kungojea--- view
  • 6 Jul 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 11 May 2021 in Senate: Madam Deputy Speaker, I vote no. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus