22 Sep 2021 in Senate:
Ninaunga mkono lugha ishara iweze kukuzwa katika shule zetu zote katika ngazi zote za serikali hapa Kenya na pia tujumuike na dunia nzima wanapoisherehekea. Hii ni kuwezesha wasiobahatika kuongea na kueleweka katika jamii wapate kipaumbele na wajihisi kama ni wananchi na watu wanaoishi katika dunia.
view
16 Sep 2021 in Senate:
Asante Bi. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Kwa kweli, Taarifa hii imetoka wakati mwafaka kabisa. Wakati huu ni wakati wa kiangazi kikuu ambapo wafugaji wanapata shida na mifugo yao.
view
16 Sep 2021 in Senate:
Hali ilivyo huko Laikipia ni ya kutatanisha zaidi. Maofisa wa polisi ambao wako upande huo wamefanya hali hiyo kuwa ngumu zaidi kuliko kurahisishia watu wa Laikipia kwa sababu wakati ng’ombe 1,000 wanauawa na askari wa Kenya, hiyo ni hali ngumu. Hali ya wafugaji wakati huu ni ngumu.
view
16 Sep 2021 in Senate:
Ng’ombe 5,000 ni kama Kshs200 milioni ambazo zimepotea. Hiyo ni pesa nyingi sana kwa wafugaji hasa wakati huu wa kiangazi. Mimi sijui askari wa Kenya wamefundishwa vipi. Wangesaidia wafugaji wakati huu lakini si kuua ng’ombe.
view
16 Sep 2021 in Senate:
Upande wa Tana River hali ni ngumu zaidi na hali kama ya Laikipia inawakumba wafugaji. Kiangazi ni kikali na malisho ni haba. Hata mahali pa kupata maji hasa upande wa Galana-Kulalu ambapo mradi wa Serikali unafanyika, ng’ombe wanashindwa kuufikia Mto wa Sabaki. Haki haipatikani kwa sababu kuna mradi wa Serikali unaofanyika upande huo.
view
16 Sep 2021 in Senate:
Hali ni kama ile ya Laikipia kwa sababu mifugo hawapati mahali pa malisho. Kupata maji pia ni vigumu kwa sababu kuna mradi wa Serikali kuhusu usalama wa lishe lakini ni ukora mtupu. Hii ni kwa sababu tukisema ni usalama wa lishe na hakuna kitu kinafanyika na watu hawawezi kuufikia mto kunywesha ng’ombe wao maji, basi itakuwa unamaliza watu na kutatanisha hali hiyo zaidi.
view
16 Sep 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Sep 2021 in Senate:
Wakati huu tunataka Waziri hasa afike hapa kwa Seneti. Ninaunga mkono wenzangu waliotangulia. Aje atueleze ni kipi kinachofanyika huko Laikipia. Katika arifa hiyo atueleze watu wa Tana River wanaweza kuufikia Mto Sabaki wapate maji yao na ya mifugo. Hatuwezi kupeleka mradi wa Serikali mahali ili watu wanaolisha upande huo wapate shida.
view
16 Sep 2021 in Senate:
Hivi majuzi Rais wa Kenya alitangaza hicho kiangazi cha Tana River kama janga la Kitaifa. Kama hali hiyo itakuwa hivyo, basi watu waruhusiwe kuingia katika Mbuga ya Tsavo Mashariki, walishe mifugo kwa sababu kuna nyasi upande huo. Ng’ombe wa watu wanaoishi upande huo hawana lishe. Ninaunga mkono.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa nafasi hii ya kuunga mkono Mswada ulioletwa na Sen. Were wa kupeleka nakala za uchapishaji katika sehemu za ugatuzi. Vile unavyojua ofisi ya Government Printer iko na kazi nyingi sana. Uchapishaji umerundika sana na umekuwa mwingi.
view