17 Mar 2020 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii na hasa mabadiliko yaliyopachikwa na Seneta wa Migori. Bi. Spika, kwa kweli, tangu ugonjwa wa (COVID-19) utangazwe kote duniani, hapa Kenya watu wamepata wasiwasi mwingi sana. Kuna uvumi mwingi unaendelea hapa na pale. Mimi naonelea kwamba ni bora Seneti isiairishe vikao vyake kwa sababu wananchi wa Kenya wako na imani sana na Bunge la Seneti. Wanapoona Bunge la Seneti liinahairisha vikao vyake, hofu yao itaongezeka maradufu. Kwa wakati huu ambao tunaenda nyumbani, hata wale ambao wako katika kaunti ambazo sisi tunarudi wanajuwa hii ugonjwa bado haijafika huko ...
view
17 Mar 2020 in Senate:
Kwa kweli, kama leo hatungeairisha kikao chetu, tungekuwa tunafuatilia wenzetu ambao tayari wameambukizwa, na kama idadi hii itaongezeka au kupungua kwa wale walio hospitalini. Kwa walio hospitalini, tunawaombea Mungu, wapate afueni ya haraka na watoke hospitalini. Wakati huu ambao tutaenda nyumbani, tutaenda kuangalia mikakati iliyowekwa katika kaunti ambayo itasaidia kupunguza maambukizi zaidi kwa wakati huu.
view
4 Mar 2020 in Senate:
Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono Rais wa Bureau of Women Parliamentarians of the Inter-Parliamentary Union(IPU), Sen. Kihika, kwa kuleta Taarifa hii kwenye Seneti. Nawaunga mkono akina mama hapa Seneti. Wanawake wanapaswa kuinuliwa katika nyanja zote za maendeleo. Wasichana na wavulana ni watoto katika familia. Tunapoinua wavulana, ni vyema tuwainue wasichana pia kwa sababu katika kujenga taifa dhabiti, lazima nguvu zote zitumike. Akina mama wakiwa na hafla yao, Maseneta wanaume wanafaa kuwaunga mkono. Wanawake hutulia zaidi wanaume wakiwa karibu nao. Wanaume wamekuwa wakiwaunga wanawake mkono katika mambo mengi. The electronic version of the Senate ...
view
4 Mar 2020 in Senate:
Seneta mwenzangu alisema kwamba wanawake ni viumbe waliotulia sana lakini kwa wanawake kutiuia zaidi, lazima baba awe karibu. Kwa hivyo nawaomba Maseneta wanaume wasikose hafla itakayoandaliwa kusherehekea siku ya akina mama. Katika hafla hiyo, ukiona mama ameketi peke yake, tafadhali nenda ukae karibu naye ili atulie kama maji ya mtungi.
view
4 Mar 2020 in Senate:
Nawapenda Maseneta wanawake na nimeona wamefurahishwa na jambo hilo. Nitahudhuria hafla hiyo ya akina mama. Naunga mkono Rais wa akina mama katika IPU ambaye aikuwa Spika wa Kaunti ya Nakuru na Seneta anayewakilisha Kaunti ya Nakuru sasa hivi.
view
3 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Taarifa fupi iliyosomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo ambako ninahudumu kama Mwanachama. Nzige wanaopatikana katika sehemu nyingi za nchi ya Kenya wameleta maafa mengi, hasa sehemu ninakotoka ya Tana River. Nzige wako kwa wingi. Tulipata baraka ya mvua nyingi hivi karibuni na sehemu zote zimekuwa na nyasi tele. Hasa mazingara yote yamekuwa ya kuvutia na maisha yetu pia imeanza kubadilika. Lakini tangu nzige watuvamie, mazingara hayo yameanza kuharibika. Nzige wamekuwa wengi na wanakula miche yote ambayo inakua wakati wa mvua. Nzige hawa wamesababisha ukosefu wa nyasi na kuathiri wakulima ...
view
3 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwa hakika, usalama wa nchi hii ni kitu muhimu sana. Ili kupunguza utatanishi na mazungumzo ya hofu nyingi mitaani, ni vyema kabisa tuelezwe kinaga ubaga hali ya usalama ilivyo hapa nchini. Tukiangazia sehemu za kaunti za Wajir na Mandera, tuliona vile mambo yalivyofanyika jana na juzi. Hali ilikuwa ni kulumbana, na watu walikuwa wakifyatuliana risasi hapa na pale. Kunao majangili walioingia sehemu hiyo, ambao sisi tunanona katika runinga na vyombo vingine vya habari, kwamba kuna hali ya kutatanisha katika upande huo. Bi. Spika wa Muda, hali ya usalama sio tu kuhusu ...
view
3 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Nimewasikiza vizuri marafiki zangu, Sen. Sakaja na Sen. Kinyua, ambaye ni Mwenyekiti wangu katika Kamati ya Ugatuzi. Kwa kweli, hali ya kutatanisha ni kwamba ukishuka kutoka kwa ndege, kuna kifaa kinachowekwa karibu na kichwa chako. Sio mimi peke yangu, bali najua kwamba pia hao wamewahi kupimwa hivyo. Wakati unapimwa hivyo, lazima utafikiria, “Alaa, leo unapimwa sehemu yako ya kichwa.” Hii ni kwa sababu mtu anakugusa kichwa hivi. Sasa, anajua haraka vipi iwapo umeambukiwa au la? Katika hali hiyo sasa, lazima kutakuwa na taharuki, mtafaruku na hasa kutatanika hapa na pale. Na jambo hilo sio kwangu ...
view
3 Mar 2020 in Senate:
Nikiendelea, Bi. Spika wa Muda, ugonjwa wa COVID-19 ilipatikana Uzunguni, hasa sehemu ya bara Asia kule kwa Wachina. Kule ndiko maafa mengi sana yametokea. Sisi hapa tunatakiwa kuangalia watu waliotoka bara hizo, na hasa kuangalia usafiri wa watu kutoka huko ambao wanakuja upande huu. Katika sehemu ya Kaunti ya Mombasa, mimi sijapata kusikia kwamba kuna COVID-19 Kenya. Iwapo kuna ugonjwa wa COVID-19 Kenya, hatutaki kutatanika wala kuwa na wasiwasi. Bali tunataka Serikali itoe taarifa, iseme iwapo kuna wagonjwa ambao wamepatikana, na kuna hospitali iliyotengwa kwa watu wa ugonjwa wa COVID-19, ili tusitatizike wali kuwa na wasiwasi. Serikali ikifanya hivyo, wale ...
view