25 Apr 2023 in Senate:
Mimi nimeona Sen. Joe Nyutu hayuko na ni Mwenyekiti wangu.
view
25 Apr 2023 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika. Naungana nawe kuwakaribisha wajumbe hawa kutoka Murang’a Kaunti. Ningependa kuwaambia karibuni Seneti. Kwenye Jumba hili mtasoma mengi. Nawatakia kila la heri wakati mko hapa kwa masomo yenu. Vile vile, nataka kuwaambia mlifanya jambo la manufaa zaidi kumchagua Sen. Joe Nyutu. Yeye ni Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Elimu. Yeye huongea Kiswahili sanifu katika Bunge hili. Pia ni mtu aliyebobea. Leo hayupo hapa, ameenda katika
view
25 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 Apr 2023 in Senate:
shughuli za kikazi. Kwa hivyo, yeye ni mchapa kazi na anaendelea kufanya kazi ambayo amechaguliwa kufanya. Bw. Naibu Spika, naungana na wewe kusema asante na kuwaambia karibu sana.
view
25 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Onyonka. Sheria zetu zinasema vijana na walemavu wapewe kazi. Hata hivyo, ni jambo la kuvunja moyo kuona baada ya wao kupewa kazi, hawajalipwa kwa wakati ufao. Siyo Kaunti ya Kisii pekee yake, bali kaunti nchini ambapo unapata watu wengi hawajalipwa. Wawekezaji na wafanyi kazi wengi wanasononeka sababu tayari wamechukua mikopo ya benki. Inakuwa ni vigumu sana kwao kuweza kuendelea na biashara zao ilhali kaunti hizi zaendelea kupokea pesa na kuchagua ni nani watakayelipa. Ikiwa wewe hauwaungi mkono kisiasa, haulipwi. Kamati itakayohusika na jambo hili inafaa ...
view
25 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 Apr 2023 in Senate:
wananchi. Wanabodaboda wanafanya kazi zao vizuri na wanapaswa kulindwa maana wanalipa ushuru. Ukisikia kaunti ambayo wanabodaboda wameanza kushambuliwa, inatutia kiwewe kwa sababu wataanza na wao, waende kwa watu wa magari na hatimaye watatushambulia sisi.
view
25 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Ni vizuri ndege zingine kama vile Qatar na Turkish zipewe mamlaka ya kuzuru Mombasa na sehemu zingine za Kenya. Wataleta ajira kwa vijana---
view
25 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, haiwezi kutua kama haijazuru. Kwa lugha ya Kiswahili inapaswa--- Wacha niendelee. Wanapaswa kuzuru Mombasa na sehemu zingine za Kenya kwa sababu inaongeza ajira kwa vijana wetu.
view
25 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view