12 Apr 2023 in Senate:
nilileta Hoja hapa na tukajadili kuhusu suala hilo. Wakati Sen. Sakaja alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, pia suala hilo liliongelewa. Sasa tunaongea kulihusu tena. Nakumbuka lililetwa hapa na Sen. Wambua na sasa limeletwa tena na Sen. Cherarkey. Sasa hivi ninapoongea, limepelekwa kwa Kamati ambapo Mwenyekiti ni Sen. (Dr.) Murgor. Badala ya kukaa hapa kusoma ripoti--- Sijui watu wanatuchukulia vipi kwa sababu suala hili limekuwa likiongelewa hata kabla tuje katika Seneti hii. Mapendekezo yaliletwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Labour and Social Welfare, Sen.
view
12 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Madazyo, lakini hakuna jambo lolote limetendeka. Ni kama kazi yetu hapa ni kuongea tu lakini hakuna mapendekezo yoyote ambayo yanafuatiliwa. Si hilo peke yake. Kuna wafanyikazi ambao wanasononeka kila wakati. Hao ni wale ambao wanaenda katika nchi za Uarabuni. Mambo ambayo tumekuwa tukiongea hapa ni yale yale. Tunapoongea, ni kama mapendekezo tunayotoa yanachukuliwa na Mwenyekiti ambaye hungoja muda wake uishe kisha amkabidhi mwingine anayekuja baada yake bila mapendekezo yoyote kutekelezwa. Wenyeviti huwa wanafanya juhudi na kuzuru sehemu ambazo wanapaswa kutembelea. Hata hivyo, ni kama mapendekezo ya Kamati huwa yanawekwa katika kabati na kuozea au kupata vumbi huko na hakuna lolote ...
view
11 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono dua mbili ambazo zimesomwa katika Bunge hili. Ninamshukuru Bw. Waikwa kwa kuleta dua kuhusu shamba lililoko Kambi Simba katika eneo la Rumuruti. Shamba hilo ni zaidi ya ekari 370. Mzee Kenga wa Mwendia alipatia Idara ya Misitu shamba lake mahali panaitwa Lariak. Baada ya kupatiana Lariak, aliaambiwa atabadilishiwa na shamba lingine huko Rumuruti, Kambi Simba. Baada ya kupeana shamba hilo, Serikali haikubadilisha na kutamka ya kwamba shamba hilo sasa ni la Bw. Kenga wa Mwendia. Kwa hivyo, imekuwa vigumu sana kwa watu walionunua shamba hilo kutoka kwa Kenga wa Mwendia, ...
view
11 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 Apr 2023 in Senate:
Hayo ndio maombi yetu. Ninaomba Kamati itakayoshughulikia jambo hili ifanye halahala ili wakaazi wa Kambi Simba na sehemu zilizoko hapo, waache kusononeka. Bw. Spika, dua la pili la Sen. Cherarkey ni kumhusu Mhe. Seroney. Nimesikiza na kusoma historia kidogo kumhusu Mhe. Seroney. Vile ambavyo ninamjua Sen. Cherarkey na vile nimesoma kumhusu Mhe. Seroney, nimejua ya kwamba tunda halianguki mbali na mti lililotoka. Ushujaa wake na vile anavyoongea bila kuogopa, hilo ndilo jambo. Hata hivi majuzi nilikuwa na woga wakati Sen. Cherarkey alivyonaswa na kutiwa ndani. Nilidhani mambo yameanza kuwa magumu kwake. Kwa sababu Mhe. Seroney alifanya kazi nzuri katika Serikali ...
view
11 Apr 2023 in Senate:
Alishikwa kwa sababu alikuwa akiandamana na ilikuwa kinyume cha sheria na ilijulikana wazi. Ni vizuri yasemwe. Sen. Wambua anafurahi na ninaona akiniambia niendelee kuongea lakini sitaongea mengi. Ijapokuwa nimemsikia Seneta wa Kaunti ya Mombasa akisema Serikali hula wana wake, anajua ya kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha.
view
30 Mar 2023 in Senate:
Asante, Naibu Spika, kwa kuonyesha usawa kwa wote. Ninataka kuungana na wewe kuleta risala za rambirambi za watu wote wa Kaunti ya Laikipia na kuzipeleka kwa watu wa Banisa kwa kupoteza kiongozi Mheshimiwa Kulow Hassan ambaye tunamfahamu. Alijitolea kufanyia wananchi kazi bila kupendelea upande wowote kama ulivyofanya. Ninaleta pia risala kutoka familia yangu. Ndugu zetu wanaopeleka bodaboda wanafaa kuwa waangalifu kwa sababu ajali hizi zinatokea kwa watu wengi. Huyu ni mmoja wetu tunayeletea risala za rambirambi lakini kila siku, watu wetu wanapata ajali hizi na wengi wanakufa. Pia vijana wa bodaboda wanapata maafa. Wagonjwa wengi katika hospitali zetu ni kwa ...
view
30 Mar 2023 in Senate:
Sisi hapa kwetu tuna ile shule ambayo ilitajwa na Kiongozi wa Wengi ambayo inaitwa Centre for Parliamentary Studies and Training (CPST) itakayokuwa ikifanya mafunzo. Tungeomba mkifika hapo mtembelee huko hata muweze kuona masomo yanavyotekelezwa huko. Karibuni na muendelee kucheza golf ambayo ndugu yangu amezungumzia. Mimi pia nimebobea katika mchezo wa golf na ninajua tutapatana viwanjani.
view
30 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view