23 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, naomba wenzangu wa upande wa upinzani wakubali kwamba ni vyema Mawaziri wawe wakija hapa ili tuwaulize maswali kwa manufaa ya Wakenya wote. Wakija hapa, tutauliza maswali moja kwa moja kwa sababu watu wengi katika nchi hii huuliza maswali.
view
23 Mar 2023 in Senate:
Sitaki kusema mengi ila kusihi wenzangu kuunga mkono Hoja hii. Sii vyema kumwingiza Spika katika mambo asiyojua. Ni vyema kuzingatia Kanuni za Kudumu na kutambua kwamba yeye ndiye Spika wetu.
view
23 Mar 2023 in Senate:
Sen. Okiya Omtatah amesema atakwenda kortini. Yeye anajua vile mahakama itaamua. Sisi tunafuata sheria ilivyo. Akifika pale, pengine ataambiwa vile amezoea kuambiwa; hiyo ni hewa moto.
view
23 Mar 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika, naunga mkono.
view
22 Mar 2023 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika. Sen. Mandago ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Afya. Kwa hiyo, ingekuwa vizuri awe wa mwisho kuongea baada ya sisi wengine kuchangia ili aweze kusikiliza maoni yetu kuhusu masuala haya. Naomba awe we mwisho na atupe uamuzi huo kulingana na vile anavyosema. Naomba kwa heshima, Bw. Spika.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono dua ambayo imeletwa na Sen. Cheruiyot kwa sababu wauguzi wamekuwa na shida sana. Hili jambo lilianza kitambo nilipokuwa katita hiyo Kamati ya---
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, nimechanganywa kidogo na yule kiongozi wa Chama cha Wiper ambaye amesema---
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, ni Sen. Cherarkey ndiye ananichanganya. Mimi ninaunga mkono dua hii kwamba maslahi ya wauguzi yanapaswa kuangaliwa. Wakati wa homa kali ya COVID-19, wauguzi wengi waliajiriwa na kupewa mkataba. Baada ya COVID-19, hakuna jambo lolote ambalo wanaonekana kufanya kulingana na wale waliowaajiri. Wameleta malalamishi yao hapa ili tuyaangalie. Langu ni kuomba Mwenyekiti wa Kamati ya Afya waangalie haya mambo kwa undani. Tusianze kuyapapasa haya mambo kwa sababu hili ni donda sugu. Ni masuala nyeti ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa kina. Wapo madaktari wengi katika kaunti zetu ambao hawana kazi. Wengine tayari wamepewa nambari ya kuajiriwa na Serikali kwa hiyo hawawezi ...
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, hawa wauguzi wanafanya kazi nyingi sana katika hospitali za kaunti lakini hawalipwi. Kwa hivyo, swala la ugavi wa fedha litakapoletwa katika hili Bunge la Seneti, tuwape mgao wa kutosha ili madaktari wetu waongezwe mshahara. Madaktari wengi katika Kaunti ya Laikipia walikuwa wamefutwa kazi na yule Gavana wa zamani. Ninamshukuru Gavana wetu kwa sababu tulishirikiana na kuwarudisha kazini madaktari hao. Tutaendela kuangalia hilo jambo---
view