22 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninatumai muda wangu ulikuwa umesimamishwa. Katika eneo la Nanyuki, madaktari huko wanaendelea kufanya kazi katika hali duni sana. Mshahara wanaolipwa hautoshi. Pia wauguzi wanaishi maisha ya uchochole. Sio Nanyuki peke yake bali pia Nyahururu, Kinamba na Rumuruti. Kuna madaktari wengi lakini zahanati zetu zilionekana kuwa nzuri wakati wa homa kali ya COVID-19. Baada ya ugonjwa huo kupungua, inaonekana ni kama wameachwa na hawaangaliwi tena. Ninaiomba Kamati inayoongozwa na Sen. Mandado kuvalia njuga suala hili na kuliangalia kwa kina kirefu. Wewe umekuwa katika hizo kaunti na unajua shida ambazo madaktari wanapitia---
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, ninashukuru kwa kunipa fursa. Ni vizuri Hoja hii imeletwa leo ndio watu waeze kuongea. Kulingana na Katiba ya Kenya, Kipengele 37, kinasema vizuri sana, maandamano yanapaswa yafanywe lakini kwa amani. Kwa hivyo, watu kubeba mawe ni jambo ambalo linaudhi sana. Kuwashambulia Wakenya wengine na kuwaibia ni jambo ambalo halikubaliki. Mimi niliona maandamano hayo watu walkuwa wanatembea hapa mjini na wakafanya maduka ya watu yafungwe.
view
22 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, watu wliashambuliwa na hata wengine wako mortuary . Ukweli ujulikane, kile kilichoniudhi zaidi, nikuona Kiongozi wa Waliowachache na wengine wameshikwa.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, ni vizuri historia ya anayeongoza maandamano ijulikane. Tunajua ya kwamba alifanya maandamano akasumbua Rais Moi hadi akamfanya kuwa waziri, alafu akafurahi. Kutoka hapo, akafanya maandano tena wakati wa Rais Mwai Kibaki, akafanywa kuwa Waziri Mkuu. Akafanya maandamano wakati wa Rais Uhuru Kenyatta, akasalimiwa. Ukiona jina Orange Democratic Movement (ODM), inamaanisha One Dangerous Man na anajulikana ni nani. Anajulikana. Kwa hivyo, inapaswa ijulikane vizuri ya kwamba hata sasa---
view
21 Mar 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika. Nasimama kuunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Joe Nyutu wa kutoka Kaunti ya Murang’a. Mambo ya nguvu za umeme yamekumwa ni hali ya sintofahamu katika nchi yetu. Sio Murang’a peke yake. Ukitembea sehemu nyingi hasa katika Kaunti ya Laikipia unapata transformers ambazo tumepewa zinasambaza nguvu za umeme kwa mtu mmoja tu ilhali sehemu hiyo ina watu wengi ambao hawana stima. Mradi ule unaitwa Last Mile kwa lugha ya kiingereza. Hata hivyo, sisi watu wa Kaunti ya Laikipia hatuna tabasamu yoyote kwa sababu stima yenyewe hakuna. Tunaishi kwa giza. Taarifa hii isiangazie Kaunti ya Murang’a pekee yake. Waangazie ...
view
21 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
21 Mar 2023 in Senate:
Hivyo basi, Shirika la nguvu za umeme linapaswa liangazie haya mambo. Wanapoulizwa haya maswali, waseme ni transformer ngapi ambazo wamepeana huko Laikipia, watu wangapi wamepewa stima. Sio hayo tu, bei ya nguvu za umeme imepanda sana. Tumeambiwa kwamba hii ni kwa sababu hakunyeshi. Lakini pia kukinyesha mara moja tu, stima zinapotea. Unashindwa ni shida gani iliyoko. Wakati wa kiangazi, unaambiwa hakuna maji. Kukinyesha, unambiiwa maji yamekuwa mengi hivyo basi stima hatupati. Tungetaka tuambiwe ni watu wangapi wamepewa umeme kwetu Laikipia na ni watu wangapi wamepangiwa kupewa umeme wakati huu wanasema ni tabasamu na isiwe ni tabasamu ya mwisho. Hivyo basi, ...
view
21 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika nilitaka kusema kwa sababu imeandikwa katika daftari zetu. Badala ya sisi kuwapongeza wanafunzi, itakuwaje sisi tutakuja kuwakosoa kwa kuwaambia yale wanayosoma hayana manufaa na kuwaambia wavuvi, wafugaji ni wa manufaa zaidi kushinda wanafunzi. Badala ya kuwapa wanafunzi motisha, anawadharau na kuwaonyesha masomo sio ya manufaa. Sisi tulioko hapa ni wasomi na weledi wa masomo. Asante.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, ninasumbuka kwa sababu tayari wewe ulikuwa umefanya uamuzi kwa jambo hili. Karatasi iliyoletwa hapa na ndugu yangu mwana sharia, Sen. Omogeni, hayo ndio mambo anakuambia ufanye uamuzi. Wewe mwenyewe unajua ni wakati gani utafanya uamuzi, ni mambo gani utaangalia uweze kufanya uamuzi. Hakuna mtu yeyote katika Bunge hili anaweza kukushurutisha, kukuamrisha ama kukuambia chochote kwa sababu wewe ndio mwenye uwezo na ujuzi wa kufanya hiyo kazi. Na kwa sababu ulikuwa umefanya uamuzi, na umeletewa barua ambayo wewe haujui imetoka wapi. Imesemekana imeletwa siku ya leo. Bw. Spika, wewe unapaswa kufanya uamuzi bila kuamrishwa na mtu yoyote. Lakini mimi ...
view