15 Mar 2023 in Senate:
Huyu Seneta ni mgeni. Hana uzoefu wa Kanuni za Bunge. Bw. Spika wa Muda, chukua fursa hii, upeleke Maseneta wageni ambao hawana uzoefu wapate mafunzo.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, hana uzoefu. Haongei kwa sababu anajua, anafahamu au anazimenya sheria. Debe tupu haliwachi kutiririka, ndiposa sasa unasikia linaendelea kutiririka. Ni vizuri tuseme ukweli. Bw. Spika wa Muda, Sen. M. Kajwang’ ambaye tunamwongelea amenyamaza na kutulia kwa sababu ananielewa. Nikiwa kama Mwanakamati, ninamuomba msamaha kwa sababu hakujulishwa.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, niko kwa hoja ya nidhamu.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, Mwenyekiti wa Kamati amefanya vilivyo, kwa kuleta Ripoti hii, ili iweze kujulikana wazi sababu ya Kamati kutoweza kuenda Mfangano. Hiyo ndiyo sababu. Tumeomba msamaha kwa Seneta.
view
14 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, nina kushukuru kwa kunipa fursa hii. Vile vile, ninamshukuru Sen. Cherarkey kwa kuleta swala hili nyeti ya udhamini wa wanafunzi. Udhamini wa wanafunzi umekuwa ni jambo nzuri sana. Lakini, wale ambao ni wakora wanachukua fursa ile kujinufaisha wenyewe kwa sababu wanajua wanafunzi wengi hawana uwezo. Ukiwatajia udhamini, ni watu ambao wanataka masomo. Lakini, kwa sababu ya ukosefu wa pesa, kunafanywa mchango. Unapata hata wale ambao wanaishi katika maisha ya uchochele wanafanya harambee kusudi waweze kupata ule udhamini na kupeleka watoto wao shuleni waweze kupata masomo. Bw. Spika, Kamati ambayo itashughulikia jambo hili, inapaswa ilete mwangaza zaidi watu wajue ...
view
14 Mar 2023 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise, pursuant to Standing Order No.53(1) to seek a Statement from the Standing Committee on Agriculture, Livestock and Fisheries regarding the distribution of subsidized fertilizer in Laikipia County. In the Statement, the Committee should- (1) State the number of farmers in the county who have benefited from the National Fertilizer Subsidy Programme since the programme began, stating the percentage of eligible farmers these numbers represent. (2) Elaborate how the programme has been implemented stating the areas covered. (3) State measures in place to ensure that smallholder farmers in remote areas of Laikipia County have access to ...
view
9 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nauunga mkono dua lililoletwe na Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge hili. Masuala ya shamba ni nyeti na yamekuwa yakiathiri watu hapa nchini. Wakipsigis walionyang’anywa mashamba yao wanaishi maisha ya kichochole ilhali yale mashamba ni yao. Ukitembea sehemu nyingi katika Kaunti za Nyeri, Kiambu, Murang’a na Laikipia unapata wakaazi ambao walikuwa na shamba zao kitambo, lakini wakoloni walipowasili waliwafukuza na kuwatimua katika vijiji. Watu wale walibaki kufanya kazi katika mashamba waliyonyang’anywa. Hivi leo, watu hao hawajapewa fidia na bado wanaendelea kusononeka na kupata majanga.
view
9 Mar 2023 in Senate:
Kinachoshangaza zaidi ni kuwa miaka 60 baada ya kupata Uhuru, tunaathiriwa na ukoloni mamboleo. Mtu yeyote akimuona mzungu anadhani anafaa zaidi. Ukitembea barabarani na mzungu amevaa nguo zisizo za nidhamu unapata wengine wanafuata mtindo huo. Hatujivunii. Tukiwa katika Bunge hili pia tunavaa suti. Mtu akivalia mavazi ya kiafrika anaonekana kama mtu ambaye yuko nyuma, hajifahamu na hajielewi. Mtu huyo anaonekana amepitwa
view
9 Mar 2023 in Senate:
Ninapoongea, mimi hutumia lugha ya Kiswahili hapa Seneti. Wengi huniona kana kwamba sijastaarabika. Mimi sijafika kwa sababu sineni kwa lugha ambayo wamefunzwa na ambayo imeathiriwa na ukoloni mambo leo. Baadala ya kuyakunua mashamba yetu kwa kufuata Katiba iliyowekwa na kwa njia sawasawa tunawapatia wageni hawa hadhi ambazo hazifai kwao.
view
9 Mar 2023 in Senate:
Ikiwa umepiga foleni pale kwenye benki mzungu atapita na kuhudumiwa na wewe ubaki pale ilhali hii ni nchi yako. Ukienda katika nchi zao wewe utadharauliwa. Watu wengi waliotembea kule wanawezakukueleza Tulienda na Seneta ambaye sitamtaja hapa katika nchi moja ya ughaibuni na tuliokena kama hatufai; yaani tulionekana kama nyani kwa sababu ya rangi ya ngozi zetu. Ni vizuri kamati husika ishugulikie mambo haya kwa undani kabisa na wasiwe na uoga. Hakuna tofauti kati yangu na mzungu.
view