8 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Faki kuhusu ukakatwa kwa umeme katika hospitali ya Mombasa. Bw. Spika, swali langu ni hili: Je, wagonjwa wanalipa wanapoenda kutibiwa katika hospitali hii ya Mombasa? Kama hawalipi, jibu la swali langu litakuwa tofauti. Hospitali hizi zetu tunazojadili hapa, mtu akifariki hupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Watu wanapoenda kuchukua mwili, hulipa kiwango fulani cha pesa. Ikiwa wagonjwa hulipa wanapotibiwa na miili inapochukuliwa kutoka chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hii, pesa hizo huenda wapi?
view
8 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
8 Mar 2023 in Senate:
Nimemsikiliza Sen. Thang’wa akisema kuna hela zinatengwa na Seneti za hospitali za kaunti zote nchini. Kuna pesa za Mombasa, Laikipia na kaunti zingine. Pesa hizi huwa zinaenda wapi? Ninakashifu ule ukataji wa nguvu za umeme na Kampuni ya Nguvu za Umeme Nchini. Bw. Spika, tujiulize maswali ambayo ni mazito. Wale ambao wanaohusika na msimamizi wa hospitali zetu, kwa nini hawalipi deni au bili ya stima? Ningependa Mwenyekiti aulize kama kulikuwa na notisi na ya siku ngapi kabla ya kukata stima katika hospitali hiyo kwa ajili ya wale wagonjwa walio katika vyumba vya wagonjwa mahututi. Je, kuna maadishi kuhusu notisi iliyotolewa? ...
view
8 Mar 2023 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bw. Spika wa Muda.
view
8 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
8 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, mwanasheria, Seneta wa Kaunti ya Nandi, alisema maisha huanza wakati wa uzalishaji. Ni vizuri hilo liondolewe katika rekodi zetu. Ninasema hivyo kwa sababu nakala yetu itaonyesha vile na ninajua yeye ni mwanasheria. Anaweza akanukuliwa katika korti ilihali anajua maisha huanza wakati mwanamke amepata mimba.
view
7 Mar 2023 in Senate:
a: Asante, Bw. Spika. Ni vizuri ukweli usemwe. Kulingana na hiyo taarifa kuhusu karanga, utapata ya kwamba sio karanga peke yake bali ni mazao yote hapa nchini Kenya. Tutilie ukulima manani inavyofaa. Tunaongea kuhusu mazao ya biashara peke yake kwa mfano, pareto mengine. Hatujatilia mkazo mazao ambayo yanaweza kutumika hapa nyumbani. Utasikia tukisema kuhusu mpunga au mahindi lakini si mimea ile mingine kama vile karanga, korosho na viazi kule Nyandarua. Haya hatuyatilii maanani kama Serikali. Tunapaswa kuyatilia maanani kwasababu yatatusaidia. Sisi, kama Serikali ya Kenya Kwanza, tumesema tutaagiza vyakula kutoka nchi za nje ili watu wetu wasikose vyakula. Hii itawezekana ...
view
7 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
7 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, zile Kamati ambazo zitashughulikiwa Taarifa hizi zinapaswa kuangalia haya mambo kwa undani ili tupate suluhu ya kudumu. Tusiwe watu wa kuja Bunge hili kuongea na hakuna chochote tunafanya. Tuwekee mkazo ukulima wote ili tusaidie kizazi tulicho nacho na vizazi vijaavyo. Isiwe tutaongea hili jambo mwaka baada mwaka.
view