John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 571 to 580 of 2259.

  • 2 Mar 2023 in Senate: Madam Temporary Speaker, on a point of order. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Bi. Spika wa muda, Sen. Munyi Mundigi wa Embu anatembea kutoka upande wa Walio Wengi hadi kwa Walio Wachache bila kuzingatia Kanuni za Kudumu za Seneti. Ni kama yuko katika soko la Runyenjes, ambapo anatoka katika duka la muhindi akielekea duka lingine. Mwambie afuate sheria, arejee kwenye kiti chake na kufuata kanuni vizuri ili iwe funzo na aweze kuzoea. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika Wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Siku ya leo ni siku ya hofu zaidi katika nchi yetu ya Kenya. Nina uchungu kutokana na uamuuzi ambao Mahakama yetu ya Upeo ilitoa kwa kukubali kwamba tunapaswa tuwe na miungano ya mashoga, wasagaji, watu walio na jinsia mbili na wale ambao walibadilisha jinsia. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Mimi ninajua kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria sio kutunga sheria. Kazi ya kutunga sheria ni ya Bunge. Ninajua vizuri mamlaka ya mahakama inapatikana kutoka kwa wananchi wa Kenya. Ibara ya 159 ya Katiba yetu inasema mamlaka ya mahakama inatokana na wananchi wa Kenya. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Nikikumbuka vizuri wakati Wananchi wa Kenya walipokuwa wanatengeneza katiba yao, walisema dhahiri shahiri kwamba mwanaume anapaswa kumuoa mwanamke. Kinachonisumbua zaidi ni kuwa Ibara ya 41 inasema kuwa mwanaume amuoe mwanamke ama mtu wa jinsia tofauti, lakini si watu wa jinsia moja. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Sen. Wambua, aliniambia akimaliza mambo haya ya siasa atakuwa muhubiri. Kinachonisumbua ni kwamba, wakati atakapokuwa akiandika ile hati ya ndoa, kulingana na Mahakama ya Upeo, itakuwa ndoa ni ya Mueni na Mwende. Itakuwa ni ya Wambua na King’ola ama Mutua. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Bi. Spika Wa Muda, itakuwa ni jambo la kuvunja moyo. Tutafanya huyu kiongozi ambaye atakuwa tayari amejitolea kuhubiri neno la Bwana kama alivyotangaza hapa aache kuhubiri kwa sababu hataweza kusimama wakati ule. Pengine atakufa tu kwa kupigwa na mshtuko wa roho. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Nikifuatilia mambo yalivyoanza ni ya kwamba Mashirika yasiyo ya Kiserikali yalisimama kidete na kusema ya kwamba hayatasajili hii miungano. Lakini Mahakama yetu ya Upeo, sijui ni kwa kutojua ama kwa kujua zaidi wakaendelea mbele na kusema ya kwamba wanahalalisha miungano hii. view
  • 2 Mar 2023 in Senate: Walituambia ya kwamba, ukiangalia katika Ibara ya 27 ya Katiba, inasema ya kwamba; hupaswi kumzuia mtu yeyote ama huwezi kuwazuia watu kufanya vile wanavyotaka kuungana. Ijapokuwa Ibara ya 36 ya Katiba ya Kenya inasema ya kwamba inakubalisha miungano yoyote. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus