2 Mar 2023 in Senate:
Wale ambao waliiandika Katiba hii, na ni sisi Wakenya, hatukumaanisha miungano ya aina hii. Ndiposa Halmashauri ya Usajili wa Mashirika ambayo yalikuwa yamekataa kusajili miungano kama hii yakasimama kidete na yakakataa. Hata hivyo, mambo haya yalipelekwa katika Korti yetu la Upeo na yakaidhinishwa.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Ningependa kuomba, na pengine mawakili kama Sen. Maanzo, watatuambia zaidi kwa sababu wamebobea katika kazi ili, Mwanasheria Mkuu wetu wa Kenya akate rufaa. Sababu ni kuwa majaji wale waliokuwa wamekaa pale ni watano. Ninadhani majaji saba ndio wanapaswa kuwa wamekaa pale waweze kutoa uamuzi wao.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Badala ya Mahakama yetu ya Upeo kutetea na kuilinda sheria yetu, wao wanasikiza mambo kutoka nchi za kigeni. Kazi yao ni kuharibu maadili yetu ambayo tumeyasimamia na tutakufa kwa maadili yetu.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Hata ikiwa watu wote katika hii Seneti watajiunga na hawa wasagaji na mashoga, mimi nitabaki pekee yangu kupambana na hizi sheria ambazo ni mbaya na zinagandamiza. Nitasimama kidete niweze kuhesabika. Hii ni kwa sababu Bibilia inasema hakuna goti halitapigwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Nikiona Mwenyezi Mungu amenisahau, nitamwambia, “Mwenyezi Mungu kumbuka nilisimama kwa Seneti nikatetea sheria zilizo nzuri. Ataniambia “Kinyua simama.” Kwa sababu ninaitwa Yohana, “Kuja upande huu uishi milele na milele.”
view
2 Mar 2023 in Senate:
Nashukuru Bi. Spika Wa Muda.
view
2 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
2 Mar 2023 in Senate:
On a point of order, Madam Temporary Speaker. I would not want to interrupt her, but I find it not appropriate to insinuate about our judgement and visitors from other countries. Does it mean that our courts are not independent? Does it mean that they are influenced by external forces? Especially when she says the First Lady of the USA visited Kenya, then our Judiciary ruled in that favour, I do not find it appropriate.
view
1 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Nimesikiza hii dua kwa makini na nimesikia malalamishi ya wale waliokuwa wakiongea. Lakini nimeshangaa kwa sababu ninavyomjua Kiranja wetu, yeye ni mtetezi wa walala hoi na wanyonge. Najua Serikali yetu ya Kenya Kwanza imekuja kwa kauli mbiu ya kutetea walala hoi na wanyonge. Huu ndio msimamo wetu dhabiti. Wale watu wa Buxton pale Pwani wako pale kihalali. Ikiwa mzazi wa mtu ameishi pale, mtoto akaishi pale na wajukuu na vitukuu wanaishi pale, kama Serikali inataka kuwajengea nyumba zinazofaa, ni vizuri wenyeji waulizwe. Sheria yetu inasema ni vizuri watu wahusishwe kabla mradi wowote haujatekelezwa.
view
1 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view