1 Mar 2023 in Senate:
Sheria yetu inasema uzuri ule unapaswa kuonekana umefanywa. Ni vizuri wenyeji wa Buxton wahusishwe. Sheria zetu za Kenya zinasema watu wapewe nyumba na malezi mazuri. Hii ni jukumu ya Serikali. Kwa hivyo, hawaombi dua kando na maneno ambayo yanasemwa kisheria. Sen. Cherarkey amebobea kwa maswala ya kisheria na namuunga mkono kwa yale amesema. Ni vizuri ile kamati itakayoshughulikia haya mambo iangalie kwa undani. Si suala la Buxton Estate pekee yake kwa sababu kuna watu wengi katika Jamhuri ya Kenya wanaoishi maisha ya kusononeka na uchochole. Itakuwa vyema kama kaamati hiyo itawashughulikia watu wote ambao wanaishi mazingira duni. Sisi sote tuangalie ...
view
28 Feb 2023 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
28 Feb 2023 in Senate:
Bw. Spika, nimemsikia Sen. Tabitha Mutinda akisema mheshimiwa tunayemjadili hapa kuwa komishna ya Tume ya Bunge ni Mkamba. Ningependa kumukumbusha kwamba mheshimiwa ni kiongozi katika nchi ya Kenya. Alikuwa mwenyekiti wa chama kinachoongoza cha UDA. Kwa hivyo, nilitaka tuondoe matamshi hayo katika kumbukumbu zetu ili isionekane kana kwamba yeye ni kiongozi wa Wakamba.
view
28 Feb 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia Hoja iliyoletwa mblele ya Seneti. Kwanza kabisa, naiunga mkono kwa sababu ninamjua mhe. Muthama. Pengine ningepata motisha ya kumjua hata zaidi iwapo ningesikia mahojiano na mawaidha yaliyopeanwa hapa na viongozi. Nimewasikia Sen. Cheruiyot, Sen. (Dr.) Khalwale na Sen. Mungatana, MGH, wakisema kwamba walifanya kazi naye kwa muda mrefu. Bw. Spika, mimi nimemjua kama kiongozi wa chama cha UDA na pia mtu mwenye uzoefu sana katika maswala ya kisiasa. Nilipokuwa katika harakati za uchaguzi, nilienda kwake kumuuliza wosia wake kuhusu mambo ya siasa. Nilimuona kama mtu aliyekomaa na kubobea katika kazi yake. ...
view
28 Feb 2023 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
28 Feb 2023 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, in my understanding of the Standing Orders, it indicates that you have to specify the day.
view
23 Feb 2023 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kumpongeza Sen. Cherarkey kwa taarifa aliyoleta katika Bunge. Wakati huu ambapo bado kuna janga la njaa, kuna ukame kila mahali ilhali Benki Kuu imesema ya kwamba watu wakituma pesa wakitumia simu zao za rununu, watarejesha yale malipo ambayo walikuwa wakilipa. Bw. Naibu Spika, ningependa kuuliza Kamati ambayo imepatiwa fursa hii iangalie mambo hayo kwa kindani wakiwa na Wizara ya Fedha ili waweze kusaidia Wakenya kwa sababu wakati huu bado wako na shida na wangependa kuwa waendelee---
view
23 Feb 2023 in Senate:
Asante Sen. Oketch Gicheru kwa kusema niongezewe muda. Sikutaka kusema tayari alisema nikiwa hapa. Kama ningemwambia aniongezee muda ni kana kwamba ningekuwa nikimuonyesha kwa sababu nimekaa katika kiti kile na mimi naelewa majukumu aliyo nayo. Kwa hivyo, nashukuru Sen. Oketch Gicheru. Bw. Naibu wa Spika, ni vizuri Wizara ya Fedha iangalie hayo mambo kwa kindani na waweze kuambia Benki Kuu ni vizuri haya malipo yasiweze kurejeshwa. Hii ni kwa sababu, bado yale makali ya ugonjwa wa Covid-19 yanaendelea kuadhiri Wakenya kila mahali. Ni vizuri kwanza wangojee. Wapatie Wakenya muda hata kama ni miezi mingine sita ama mwaka mmoja waweze kurejelewa ...
view
23 Feb 2023 in Senate:
Kufanya hivo itakuwa inafanya Wakenya kuendelea kuathiriwa na huu ukame. Ningeomba Kamati inayoshughulikia ifuatilie haya mambo kwa kindani.
view
23 Feb 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view