John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 611 to 620 of 2259.

  • 21 Feb 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika ulichofanya kizuri ni kutosema chochote. Ulitoa amri ya korti. Seneta wa Kaunti ya Nairobi amesema na kutaja Seneta wa Kaunti ya Nyamira kuwa wao ni watu waliobobea katika mambo ya kufuatilia mahakama. Ni lipi linaolowasumbua kwa sababu kulingana na ujumbe uliotoka katika mahakama umesema kuwa tarehe 28, Machi watu watakusanyika pale na uamuzi dhabiti utatolewa. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Hawa wote ni mawakili waliosema; Sen. Omogeni, Senior Counsel na Kiongozi wa Walio Wachahce wapo pale vile vile. Ni lipi hili ambalo ni zito zaidi linalofanya waende mahakamani na kutoa ushahidi badala ya kuja hapa na kuongea. Kulingana na kanuni zetu za Seneti Spika hana macho wala masikio. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika umeleta ujumbe kutoka kortini na hawa ndugu zangu ambao ni mawakili - naona Seneta wa kutoka Kaunti ya Makueni akitingiza kipaza sauti chake - wanapaswa kwenda mahali panapofaa. Wanafaa waende mahakamani na wayatetee mambo wanayosema. Ujumbe huo utaletewa kama ulivyoletwa hapa na utausoma. Ikiwa huo ujumbe utasema vile wanavyotaka kuwa kiranja wanayetaka aweze kuwepo, wewe hauna budi kufanya hivyo. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Ni Jambo la kuudhi sana katika nchi hii ikiwa tutakuwa hatufuati amri za mahakama. Nimeketi katika Bunge hili kutoka muhula uliopita na nikasikia Sen. Orengo view
  • 21 Feb 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: akisema mahakama ndio suluhisho ukiwa umetendewa jambo. Ikiwa Bw. Naibu Spika hafuati maagizo ya korti zetu zinasema sisi hatuna budi--- view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Sheria tunazotengeneza hapa zinapaswa kupelekwa katika korti zetu ili uamuzi ufanywe. Itakuwa ni jambo la kuvunja moyo sana na lisilo manufaa ikiwa tutatunga sheria halafu korti ambazo tunataka kupatia mamlaka ya kufanya kazi zake tunakosa kuzitambua wala kuziheshimu. Sisi kama wabunge tunafaa tuwe tunasema mambo na kuyaamini. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Nakusihi ikiwa korti limesema--- view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Asante Bw. Spika. Ninaungana na wenzangu kumkaribisha Sen. Kisang na kumpa kongole kwa kazi nzuri aliyoifanya mpaka akaibuka mshindi. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus