19 Jan 2023 in Senate:
Seneta mgeni ambaye ameungana nasi amekuja kutetea Kaunti ya Elgeyo Marakwet pamoja na kaunti zingine zote za Jamhuri ya Kenya. Ni vizuri ajue ya kwamba Seneta aliyemtangulia, sasa ni Waziri Sen. Murkomen. Ni kiongozi aliyebobea sana katika hii Seneti na hata katika Jamhuri ya Kenya kwa kazi yake. Sen. Kisang, ninajua viatu utakavyovivaa ni vikubwa kidogo lakini najua utajisatiti kwa sababu wewe ni mchapa kazi. Ninamjua Seneta vizuri kwa sababu alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya ICT katika Bunge la Taifa, mimi nilikuwa katika Kamati kama hiyo ya Bunge la Seneti. Kwa hivyo tulifanya kazi naye na nina hakika ya kwamba---
view
19 Jan 2023 in Senate:
Asante, Bw. Mwenyekiti wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nikiangalia marekebisho yaliyoletwa na Sen. Mumma, ninapatwa na shida, yeye kusema ya kwamba katika Jopo la Uteuzi angependa kumwondoa mwakilishi wa Tume ya Utumishi wa Umma. Ningemwomba kwa unyenyekevu aweze kuondoa hayo marekebisho kwa sababu mwakilishi wa Tume ya Utumishi wa Umma ni muhimu zaidi wakati hii Tume inapofanya kazi yake. Vile ambavyo mwenyekiti wa kamati ambayo walikuwa wakifanya kazi wakiwa pamoja, Sen. Wakili Sigei, ameweza kuondoa marekebisho aliyoyaleta, bila marekebisho, vile ilivyotoka katika Bunge la Kitaifa hivyo ndivyo inafaa zaidi. Kwa hivyo, ningemwomba Sen. Mumma akubali kuondoa hayo marekebisho ili ...
view
19 Jan 2023 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
19 Jan 2023 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, from where I sit, I think it will be neat if the Members of the Committee that prepared this Report were the last ones to speak on this. You can guide me on that.
view
19 Jan 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninasimama kuunga mkono na kusema ya kwamba ni viziri vile hili Jopo la Uteuzi limeundwa. Nikiangalia naona ya kwamba vile liko ni vizuri kabisa. Ukweli wa mambo ni kwamba wakati wote sheria ambayo inahusu uchaguzi inaposhughulikiwa, kumekuwa na vurugu na mvutano lakini kwa wakati huu nina furaha kwa sababu tutaongea kwa amani bila vurugu ya kuelewana kwa sababu sharia hizi za uchaguzi zinahusu Wakenya wote. Nimesikia Sen. Osotsi akisema ya kwamba kuna wale ambao hawapaswi kuwa wakiangaliwa zaidi, wale wanaopaswa kuangaliwa ni vyama. Ninataka kumwambia ya kwamba watu wote wana sehemu katika ...
view
19 Jan 2023 in Senate:
, wale ndio watakaoshughulikia zaidi. Nimesikiliza ndugu zangu wakisema ya kwamba hii ni sehemu ya serikali. Watumishi wa Umma wale ambao hautawaweka kwa serikali hii ama ile kwa sababu wanafanya na serikali iliyoko na ijapokuwa nilisikia ati wanapoteuliwa na rais ni mpaka waletwe katika Bunge. Bunge lenyewe lina usemi; wanaweza kukataa ama kukubali. Kwa hivyo, Bunge lina usemi katika sehemu ile. Vile ambavyo imetengenezwa kusema ya kwamba kuwe na watu katika Tume ya Bunge; mwanamume na mwanamke mmoja, ninaunga mkono mia kwa mia. Vile vile, watumishi wa umma ni mpaka washughulikiwe. Mahali ambapo nina tashwishi ni hawa wanasheria. Kila mahali ...
view
19 Jan 2023 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir!
view
19 Jan 2023 in Senate:
Bw. Mwenyekiti wa Muda, lile linalotusumbua si vile picha ilivyokua, ila ni ile lugha Seneta wa Nairobi alitumia. Aliita Mwenyekiti anayeongoza Bunge hili mwongo. Haikubaliki! Tutakubali kwanza ikiwa Seneta wa Nairobi akiomba msamaha kwa kutumia lugha isiyokubalika katika Bunge hili. Baadaye, zile picha zinaweza kuletwa. Aliyesema hizo picha si nzuri ni Kiongozi wa Walio Wengi na amevaa miwani. Kwa hivyo, anaweza kosa kuona vizuri.
view
19 Jan 2023 in Senate:
Bw. Mwenyekiti wa Muda, tutaonekana kama tunafanya mzaha ikiwa tutanukuu ukiitwa mwongo, na baada ya wewe kusema vile, anarudia kuwaita wale wanaokushauri hapo waongo. Hilo si jambo nzuri. Ni vizuri aombe msamaha ndio tuonekana tunaheshimu Kanuni tulizozitunga sisi wenyewe.
view
30 Dec 2022 in Senate:
Point of order of order, Mr. Deputy Speaker, Sir.
view