John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 651 to 660 of 2259.

  • 24 Nov 2022 in Senate: Nilipokuwa nikitazama runinga, niliona wakulima wanaotoka Kilifi wakisema kwamba sasa wamepata afueni. Angalau sasa wanaweza kupanda mboga, mahindi na chakula kingine ndio waweze kupata lishe. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Kwa hivyo, jambo la kwanza tunapaswa kuzingatia na kuangalia kwa undani ni Wakenya wanaoishi Kilifi na sio hao pekee yao ambao wanaoishi penye miti hii ya mibuyu view
  • 24 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: iko. Ukiangalia hata sehemu ambayo Sen. Kathuri ametoka, utapata inafika wakati hawa wakulima wanang’oa miti ya majani chai na kahawa ili waweze kupanda mimea ambayo itawapatia faida. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Kwa hivyo, ni jukumu letu na la Serikali kuwaonesha wananchi manufaa ya ile miti na manufaa itapatikana tu, ikiwa itampatia mtu kuweza kupata lishe yake. Kwa mfano; ukitembelea sehemu nyingi ambako kuna hii misitu, wananchi wanauliza faida ya hii misitu ni nini? Hii ni kwa sababu mwananchi asipopata faida ya misitu, hatapata manufaa yoyote kwa ile misitu. Hii ni kwa sababu yeye anataka lishe na manufaa kwa kiti kilichoko katika sehemu ile. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Bw. Spika, hata ijapokuwa naunga mkono ni jukumu ya Serikali kuambia mwananchi ndio. Hii ni kwa sababu nilipokuwa nikiangalia katika runinga kama nilivyosema, niliona wananchi wakiwa na furuha. Wanasema wakingoa ule mti wa mubuyu, wanapata sehemu ya kupata chakula chake. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Mswahili anasema kuwa “mtoto akikosa maziwa ya mama, hata ya mbwa ni maziwa.” Kwa hivyo, ni vizuri, hata ijapokuwa tunaunga mkono kwa sababu ya mazingira haya mazuri, lakini mazingira yakiwa hata mazuri namna gani na mtu ana njaa haitakuwa na faida yeyote kwake. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Kwa hivyo, ni kama yale mazingira na zile hela zinapatikana wakati tuna hii maneno ya control of carbon emmisions, wananchi wenyewe waweze kupatiwa zile hela ndio waweze kuwa na motisha ya kuweza kuchunga mazingira. Kwa mfano: kama ni ile miti mtu anajua ndio huu mti utanisaidia. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Nimesikia, kwa mfano, ukitembea huko Mau, unapata kunakuwa na vurugu ya yule ambaye anafaidika. Hii ni kwa sababu akichunga ng’ombe wake katika ule msitu, yeye anapata lishe na yule ambaye angelitaka kulima pale ndio apate lishe--- Kwa hivyo, ni lazima kama Serikali tujue ya kwamba kila mtu anapata manufaa ya mazingira ambako anaishi. Hiyo nadhani ingelikuwa ni nzuri Zaidi. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Vile ambavyo ningependa kuihamasisha hii Kamati ni waangalia na watafute jambo la kudumu kwa mti wowote. Tunaweza kusema ndio miti iling’olewa na ikabebwa. Lakini, kama mwananchi angejua umuhimu wa ile mti kung’olewa na iondolewe, angekataa na angepigana ule mti usingolewa, kwa sababu anajua manufaa yake. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus