John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 661 to 670 of 2259.

  • 24 Nov 2022 in Senate: Lakini ikiwa ule mti atauza katika nchi za ugaibuni na aweze kupata lishe, basi anasema liwalo na liwe. Nilipokuwa nikisikiza, nimesikia miti hii ya mibuyu imekaa zaidi ya miaka 300 pale karibu miaka 200. Yule jamaa akiangalia anasema huu mti umekaa hapa miaka hiyo yote na hajaona manufaa yake na ikiwa mti wenyewe ukiuzwa atapata elfu zake kumi, watoto angalau wapate karo anaona hiyo ni nzuri kushinda mazingira yake. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Kwa hivyo, Bw. Spika, Kamati yetu ambayo najua taarifa hiyo utaelekeza kwao, wanapaswa watafute suluhu za kudumu ndio tuweze kupata manufaa mpaka milele. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Siku ya leo tuseme tu ya kwamba, ndio, hii miti ni mizuri, lakini baadaye wananchi wenyewe hawaelewi faida yake. Hii ni kwa sababu tukiwaelimisha wananchi kuhusu faida yake watakuwa wao wenyewe wakilinda mazingari. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Nimetoka Laikipia, mahali ambapo tuna mashamba makubwa na kuna miti nyingi. Lakini wananchi wanasema ndovu wanatoka katika yale mashamba, wanakuja wanakula katika mashamba yetu na kula mimea yetu na hawapati faida yeyote katika zile sehemu ambako hawa wanyama wamefugwa. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Kwa hivyo, unapata hawa wananchi wataenda kukaa pale, wakate ile miti kwa sababu hawapati faida yeyote. Kwa hivyo, faida ni lazima ionyeshwe kwa wananchi ndio waweze hata wao kufurahia na waweze kuwa wao ndio watakuwa wakilinda mazingira yetu. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Nashukuru Bw. Spika, na naunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Kibwana. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono taarifa iliyotolewa na Sen. Mumma. Kitambulisho ni haki ya Mkenya yeyote aliyefika umri wa miaka 18. Wakenya katika jamii ya Kisomali na Kiturkana hususan ukitembea sehemu za Kaunti ya Laikipia wanaulizwa maswali mengi sana. Wakitaka kusajiliwa ili kupewa vitambulisho wanaambiwa waje na vitambulisho vya nyanya au babu zao. Inaonekana ni kama hawataki kuwapa vile vitambulisho. Wanaulizwa maswali mengi ilhali wamesomea hapa Kenya kwanzia shule ya chekechea, msingi na sekondari. Yule ni Mkenya. Wakitoa vile vyeti vya kuonyesha masomo yao na pia kadi za ubatizo bado hawapewi vitambulisho. Ikiwa huna kitambulisho hata kupata mkopo katika benki, ... view
  • 17 Nov 2022 in Senate: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 17 Nov 2022 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, it was ruled in the morning by the Speaker that one can add information if they are doing so for the purpose of the Committee. I, therefore, believe that what Sen. Cherarkey is doing is in order. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus