16 Nov 2022 in Senate:
Asante Bw. Spika. Ninaunga mkono Taarifa hiyo. Ni vizuri hao wanariadha waliobobea watwikwe majukumu mengine. Wanaweza kuwa mabalozi ambao watapeperusha bendera yetu ughaibuni. Ni jambo la kuvunja moyo kwamba huwa tunawapongeza wakati huu lakini baadaye, utapata wanaishi maisha ya uchochole. Ni vizuri kwamba hata baada ya wao kufanya vizuri, wapewe mafunzo ya utumizi na uwekezaji wa hela zao. Wakiwekeza hela vizuri, watazitumia katika siku zao za usoni wakati ambapo hawataweza kukimbia tena ama kufanya biashara zingine.
view
16 Nov 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Nov 2022 in Senate:
Ni vizuri tumeweza kuwapongeza wakati huu, wala sio kuwakumbuka tu wakati wamekumbwa na shida. Ninaunga mkono alivyosema, Seneta wa Kaunti ya Nandi, Sen. Cherarkey. Amesema ya kwamba Serikali ichukue jukumu la kutumia hawa wanariadha kama mabalozi ili wawakilishe Kenya yetu katika sehemu wanazotembelea.
view
15 Nov 2022 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I Second.
view
10 Nov 2022 in Senate:
Bw. Spika, nimemsikiza ndugu yangu, Sen. Faki. Kitu chochote duniani kikizidishwa huwa na tahadhari yake. Ni vizuri Sen. Faki awafunze vijana kutoka Pwani. Hayo maneno ya kusema kuwa vijana wameshindwa kushika nyumba si kwa sababu ya mmea ule. Mtu mzima akiamua kutafuta Miraa au muguka---
view
10 Nov 2022 in Senate:
Ukipitisha kile kiwango ambacho kimekubalika kwa kitu chochote hata maziwa, chakula ama kingine, kinaleta madhara. Vijana wetu wa pale Pwani waambiwe ya kwamba ule mmea si mbaya lakini wasipitishe kiwango kinachohitajika. Ni mmea mzuri na unaletea nchi yetu ya Kenya mapato mengi. Kwa hivyo---
view
10 Nov 2022 in Senate:
Amesema vijana wa Pwani wameshindwa kushika nyumba. Wanapaswa wajipange vizuri ama tuwatumie vijana waweze kuwasaidia kushika nyumba.
view
9 Nov 2022 in Senate:
Asante, Bw. Naibu wa Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ninaunga mkono ripoti ya kuidhinishwa kwa atakayekuwa Mkuu wa Polisi, Bw. Koome. Ninaunga mkono kwa sababu yeye ni mtu aliye na uzoefu wa kazi hiyo. Nimemsikiza rafiki yangu, Sen. Wambua, akizungumza juu ya Bw. Koome. Ninakumbuka pia aliyekuwa Mkuu wa Polisi, Bw. Mutyambai, alipokuwa akiteuliwa, nilimsikia Sen. Wambua akituambia vile ako na uzoefu. Ni vizuri na alifanya kazi nzuri. Bw. Koome amekuwa na uzoefu zaidi na nina uhakika atafanya kazi nzuri na ndiposa ninaunga mkono. Bw. Naibu wa Spika, Bw. Koome anapaswa ashughulikie shida zilizoko katika sehemu zetu za ...
view
9 Nov 2022 in Senate:
Ahsante, Bw. Spika. Nasimama kuunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na Kiongozi wa Wengi. Ni wazi dhahiri shahiri kwamba mimi ni mmoja wa wale wameteuliwa katika Tume ile. Kwanza kabisa, nataka kupongeza wale wengine walioteuliwa; Mhe. Mohamed Ali, Mhe. Faith Gitau, Mhe. Patrick Makau, Mhe. Joyce Korir na wale wengine wote. Hawa ni watu ambao wamemakinika kwa kazi yao. Mimi na wale wengine watakoingia kwa Tume hii tutaenda kuwakilisha Wabunge wala sio sisi binafsi. Bw. Spika, imekua ya kwamba mtu akichaguliwa katika Tume ile, yeye huenda kwa mapendekezo yake mwenyewe na kujipendelea. Tutafanya kazi na Wabunge wale wengine kwa sababu ...
view
9 Nov 2022 in Senate:
limeshambulia PSC midhiri ya nyuki. Tume hili linafaa lijitolee ili tuweze kupambana na SRC kwa sababu Wabunge wana haki kulipwa mishahara. Tumekuja leo katika Jumba hili na tunapaswa kupewa sitting allowance . Lakini, tukisema hivyo, Wakenya wanasema tunajipenda na hakuna kitu kama hicho.
view