27 Apr 2023 in Senate:
Asante, Mheshimiwa Spika, kwa fursa hii ambayo umenipatia ili nichangiae Kauli iliyoletwa na Seneta wa Kaunti ya Mombasa, Sen. Faki, kuhusu barabara ya Jomvu kuelekea SGR. Mheshimiwa Spika, naifahamu barabara hiyo. Ni kweli kuwa barabara hiyo iko vibaya sana. Barabara hiyo ni muhimu kwa sababu inasaidia wasafiri kutoka Magongo na Jomvu kuelekea SGR. Barabara hiyo naifahamu vizuri kwa sababu nimekulia maeneo ya Magongo na ni ukweli kuwa inaumiza magari. Kwa hivyo, ningeomba Kamati ya Barabara na Usafiri, itie bidii na ilete Taarifa ya kutosha ambayo itaeleza ni kwa nini ile barabara imesitishwa kutengenezwa. Kando na hilo, Kamati hiyo iko na ...
view
27 Apr 2023 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I have observed today and I want your guidance. Today, we had strangers and students from a particular school in the House and they were neither recognized nor welcomed. Again, I can see strangers in the Public Gallery. Our tradition has it that they need to be recognized. I need your guidance because we are just seeing strangers in the House and that is against the traditions of this House. I thank you, Mr. Speaker, Sir.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ilinichangie Hoja ambayo imeletwa na Seneta wa Kaunti ya Kakamega, Sen. (Dr.) Khalwale. Ninaunga mkono hii Hoja na majina yote ambayo yamepekezwe tukianzia na Sen. Faki, Sen. Mungatana, MGH, Sen. Tabitha Mutinda na Sen. Abdul Haji. Ninafurahia vile
view
27 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
27 Apr 2023 in Senate:
kumechanganywa watu walio na uzoefu mkubwa na watu kutoka dini tofauti, ikiwemo Wakristo na Waislamu. Ninajua hii kazi ambayo wanaenda kufanya si rahisi. Kazi ya kujaribu kung’amua ukweli wa matukio ya maeneo ya Kaunti ya Kilifi, katika maeneo ya Shakahola na matukio ambayo yamepelekea vifo vya watu zaidi ya 95. Nikiangalia hizi hoja ambazo zimeangaziwa hapa, inatakikana tupanue majukumu ama mandate ya hii Kamati. Hii ni kwa sababu, kuna uchunguzi ambao unatakiwa kufanywa ili kuangazia majukumu ya asasi za kiusalama na vyombo vya dola, kuangazia yale mambo ambayo walifanya ama walifaa kufanya na hawakufanya. Tuko na kitengo cha ujasusi, polisi ...
view
27 Apr 2023 in Senate:
Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa fursa hii ambayo umenipa ili kuchangia Mswada huu wa Fedha za Usawazishaji wa Maeneo tofauti tofauti ya
view
27 Apr 2023 in Senate:
ama the Equalization Fund Appropriation Bill. Ningefurahia kuongezea sauti ya watu wa Kaunti ya Taita-Taveta kuandamana na maoni yao juu ya Mswada huu. Kabla sijaendelea, ningependa kusema ya kwamba, ninaungana na Maseneta wachache, akiwemo, Senata wa Kaunti ya Makueni, Sen. Maanzo, kwa kuupinga Mswada huu kwa sababu Mswada huu unaendelea kubagua magatuzi tofauti tofauti nchini Kenya. Watu wa Kaunti ya Taita-Taveta, waliunga mkono Katiba hii kwa sababu ilileta usawa wa ugavi wa raslimali kupitia njia mbili. Njia ya kwanza ilikuwa na ugatuzi na ulihakikisha ya kwamba fedha zinatoka katikati ama Nairobi na zikienda kwa magatuzi.
view
27 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Njia ya pili ambayo ilinuiwa kuhakikisha ya kwamba maendeleo yameenea kila mahali nchini na kuleta usawa katika magatuzi ambayo yaliwachwa kimaendeleo ilikuwa ni Ibara 204 ambayo ilileta fedha ama mgao wa usawazishaji katika magatuzi tofauti tofauti ya Kenya. Wakati tulipata uhuru, kulikuwa na ile sera ambayo iliitwa Sessional Paper No.10 ya mwaka wa 1965 ambayo ililetwa katika Baraza la Mawaziri na Mheshimiwa Waziri wa Mipango wakati huo, aliyekuwa anaitwa Mhe. Tom Mboya. Sera ile, ilisema kuwa tumepata uhuru na tunakusanya ushuru. Je, tutatumia mbinu gani ili tuendeleze Kenya kwa haraka zaidi? Katika Sera ile ambayo ninaangazia ya Sessional Paper No.10 ...
view