27 Apr 2023 in Senate:
ambayo imekuja sasa hivi na tunataka kupitisha, inaendelea kunyima Kaunti yangu ya Taita-Taveta fedha. Wakati wa mfumo wa kuangalia maeneo ambayo yatafaidika kwa pesa ya kusawazisha magatuzi, Kaunti ya Taita-Taveta ilikuwa inafaidika. Wakati wa kupitisha mfumo wa kugawanya hizi pesa kwa mara pili, yaani second generation, tulipata kwamba Kaunti ya Taita-Taveta imepewa Wadi mbili peke yake. Hizo Wadi mbili ni Kasighau na Chala. Wadi mbili kati ya Wadi 20 za Kaunti ya Taita-Taveta.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Huu mgao wa kusawazisha magatuzi, ulikuwa tayari umewekwa ua ya kwamba hizo pesa zingeangazia huduma za barabara. Leo ninauliza, je, Tume ya ugavi wa pesa ama Commission on Revenue Allocation (CRA ) ilifanya utafiti namna gani na kugundua ni wadi mbili peke yake Kaunti ya Taita-Taveta, ambazo zinafaa kupata mgao wa kusawazisha magatuzi?
view
27 Apr 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, asante. Tumekuwa na rafiki yangu, Sen. Cherarkey, kwa hili Bunge na tumefanya mambo mengi pamoja. Bi. Spika wa Muda, nafikiri kulikuwa na Ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti ambayo ilikubaliana na Commission on Revenue Allocation (CRA), ya kwamba magatuzi yanafaa kupata Kshs407 bilioni. Kamati hiyo ya Fedha na Bajeti inayongozwa na mstahiki gavana party leader Sen. Ali Roba, ilileta mabadiliko katika Mswada uliotoka katika Bunge la Kitaifa. Ilikuwa inasema ya kwamba tupatie magatuzi Kshs385 bilioni. Kamati yetu ikasema tufanye mabadiliko na tupee magatuzi Kshs 407 billioni, kulingana na mapendekezo ya CRA. Bi. Spika wa Muda, ...
view
27 Apr 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, muda wangu utaumia na nafikiria leo ndio siku ya mwisho.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Ni ukweli wa mambo kwamba Kamati ya Fedha na Bajeti ilifanya kazi nzuri. Walituletea Ripoti nzuri ambayo ilikuwa inapendekeza tusikubaliane na Bunge la Taifa, kuipa counties Kshs385 bilioni, wakongeza hadi Kshs407 bilioni. Lakini, Bunge la Seneti lilikataa na likapea counties Kshs385 bilioni.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Yes, Madam Temporary Speaker.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Nashukuru sana, Bi. Spika wa Muda. Ninaongea kuhusu uhitaji wa wananchi ama eneo la Taita-Taveta wa hizi pesa za usawazishaji wa magatuzi. Bi. Spika wa Muda, kuna maeneo yalioachwa nyuma kimaendeleo na Taita- Taveta ilikuwa ni kati ya hayo maeneo. Hiyo pesa ilioekewa uwa ama kwa kimombo ilikuwa ring-fenced, ni ya kupeleka madawa hospitali, kupelekea wananchi maji, stima na kujenga barabara. Je, leo hii, wakati wa mfumo wa kugawanya hizi pesa kwa awamu ya pili, kuwacha Taita-Taveta inamaanisha ya kwamba Taita-Taveta imepata barabara?
view
27 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, nimeona taa lakini ukweli ni kwamba nimeongea tu kwa dakika tano. Huo ndio ukweli wa mambo kwa sababu kumekuwa na points of order na
view