11 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 Oct 2022 in Senate:
kwamba haiwezi faulu hata sasa. Kama Waisiraeli walifanya na wakafaulu, basi tuwalete huku watusaidie ili tuweze kufaulu. Katika mpango wa PPP, hii miaka mitano iliyopita tulikuwa tunasukuma mapendekezo tuliyokuwa nayo. Tuliyapeleka kwa PPP department kule Treasury ila hawakupitisha huo mradi wa Njoro Kubwa uliohitaji pesa kiwango cha Kshs6 billion na ulikuwa unalipiwa na sekta ambazo si za Serikali. Najua saa hizi saa hizi utaenda kupita, kwa sababu Raisi amesema watatumia hiyo mbinu ili kupata wafadhili wa kuleta maji kupitia mpango wa PPP, ili tupate maji ya kunyunyizia mashamba yetu. Katika maeneo haya kame, wananchi wanalima lakini hawawezi kuvuna kwa sababu ...
view
11 Oct 2022 in Senate:
Hii imesababishwa na kufungwa kwa viwanja vya ndege na mashirika ya ndege nchini. Kwa mfano, ukienda nchini Zanzibar kuna ndege zaidi ya kumi ambazo zinatoka nchi za kigeni kila siku. Zinaleta watalii katika nchi ile ilhali Mombasa Kaunti haina ndege hata moja na hiki ni kiwanja cha kiwango cha kimataifa. Miaka mitatu nyuma, kiwanja kile kilikarabatiwa na takriban shillingi billioni saba. Hata hivyo, hatujaona ndege zozote za kimatiafa zikishuka na kuleta watalii na kurahisisha usafiri baina ya Mombasa na miji miingine mikubwa ulimwenguni.
view
11 Oct 2022 in Senate:
Usafiri wa ndege; kwa watalii wa humu nchini, umekuwa ghali kwa sababu Kenya Airways ambalo ndilo shirika la ndege linalofanya biashara katika eneo la Mombasa, Kisumu na kwingineko linadai gharama kubwa kuliko wengine wote. Kwa mfano, tikiti ya economy leo kutoka Mombasa kuja Nairobi asubuhi iliikuwa shilling elfu thelathini. Hiyo ni karibu dola mia tatu ambazo zinaweza kukupeleka kutoka Mombasa hadi London ama Frankfurt kwa ndege zinazotoka nje.
view
11 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 Oct 2022 in Senate:
Kufungwa huku kwa biashara na kuwapa nafasi Kenya Airways pekee ni ‘ monopoly’ . Inalemaza uchimi wa Kaunti za pwani. Malindi vile vile ina kiwanja cha ndege ambacho ni cha kiwango cha kimataifa kinacholemaa kwa sababu hiyo. Uwanja wa ndege wa Eldoret kule Uasin-Gishu una ndege nyingi za mizigo. Watu wengi wanapeleka mizigo yao kupitia kule kwa sababu ni rahisi kufanya clearance na kuchukuwa mizigo yao.
view
11 Oct 2022 in Senate:
Hatuoni sababu gani viwanja vya ndege vya kimatiafa vya Moi, Malindi na Kisumu haviwezi kuruhusiwa kupokea ndege za kigeni kulingana na ile tunaita ‘ openskies policy’ . Hatuwezi kuendelea kama Afrika iwapo tumefunga njia, anga na bandari zetu na hatuwezi kupokea. Mhe. Spika wa Muda, bandari ya Mombasa hupokea maelfu ya meli kila mwaka. Meli hizi zinatoka nchi za kigeni zinaleta mizigo na kubebe mingine kutoka Mombasa. Hatuoni sababu ya Uwanja wa Moi Mombasa kutotumika kwa swala hilo.
view
11 Oct 2022 in Senate:
Pili, Uchumi Samawati ni jambo ambalo halikutajwa katika hotuba ya Rais, lakini ni muhimu sana kufufua uchumi wa Kaunti za pwani. Tunao ufuo wa bahari kutoka Lungalunga ama Vanga kusini mpaka Kiunga kaskazini. Sisi kama wenyeji wa eneo lile hatujaweza kupata faida zake kamilifu. Kwa mfano, uvuvi wetu bado ni ule wa kiasili. Unavua kutumia vidau, mshipi moja ama nyavu ndogo ambao hausaidii kupata samaki wa kutosha kukuwezesha kulisha familia na kuuza ili kupata mapato ya kukusaidia na familia yako.
view
11 Oct 2022 in Senate:
Lazima watu wawekeze katika Uchumi Samawati. Unaweza kutuletea utalii na biashara ya samaki, kawi ya upepo wa bahari na vile vile mafuta na vitu vingine ambavyo vinapatikana katika bahari hii.
view
11 Oct 2022 in Senate:
Katika swala la sheria yani ‘ rule of law’, kuna dalili zinazoonyesha kua serikali hii haitaweza kuheshima uhuru wa sheria. Jambo la kwanza ambalo tuemona ni kuwa mahakama imerushiwa vishawishi kadhaa ambavyo vinavyonyesha kwamba serikali hii iko tayari kuhujumu uhuru wa mahakama. Kwa mfano, siku ya pili alipochaguliwa Rais Ruto, tuliona mambo ya kuapishwa harakaharaka kwa majaji sita yalifanywa haraka ambao walikuwa wamezuiliwa siku za awali. Tumeona pia kuna mipango ya kuongeza ruzuku kwa mahakama kwa jumla. Bw. Spika wa Muda, mwisho ni kuwa Rais alipowasili, jambo la kusikitisha ni kuwa Jaji Mkuu na Naibu wake walikuwa wamesimama kwa msitari ...
view