Her story is of hope, hard work and resilience. Her father died before she completed her education but that did not stop her from pursuing her education later on as an adult. Even before joining politics she was passionate in helping and empowering her community.
25 Mar 2015 in National Assembly:
Hon. Deputy Speaker, I beg to move and ask hon. Mwaura to second.
view
12 Feb 2015 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Pia namshukuru Mhe. Okoth kwa kuleta Hoja hii kwa sababu ni jambo ambalo limetutatiza sana. Wakati umefika ambapo elimu yetu ya Kenya iweze kupigiwa msasa kamili kwa sababu kunayo matatizo mengi yameikumba, kuanzia wanafunzi mpaka wale ambao wanawaangalia kama vile wazazi au wale ambao wanawachunga. Kuanzia mambo ya kulipa karo na vilevile kuangazia mambo ya vile uchaguzi unaofanywa watoto wakienda katika kidato cha kwanza, unapata kwamba kuna kuwa na ubaguzi sana wakati wa kuchagua wanafunzi ambao wataenda katika kidato cha kwanza, na hii imeleta kero sana kwa wazazi ambao ...
view
12 Feb 2015 in National Assembly:
ya elimu kuketi ili jambo hili liweze kutatuliwa mara moja ili watoto waweze kusoma. Hii ni kwa sababu tunawanyima watoto haki yao ya kupata elimu. Kwa hivyo, katika mambo ya karo, ni lazima tuketi tuweke vichwa pamoja na tuhakikishe kwamba wanafunzi wanaweza kupata haki yao ya kusoma. Vile vile, naangazia pia wanafunzi ambao hawapati zile alama za kuweza kwenda kidato cha kwanza. Kama mwaka jana, kuna watoto 2,000 ambao hawakuweza kwenda kidato cha kwanza kwa sababu hawakuweza kupata ile alama ya 200. Ni lazima tuketi chini tuangazie jambo hilo hili tusiwanyime watoto haki yao. Watoto wa miaka 13, tunasema waende ...
view
10 Feb 2015 in National Assembly:
Asante sana mhe Spika. Ninataka kuungana na wenzangu kutoka Kaunti ya Taita Taveta kutoa rambirambi zetu. Kwa kweli ni jambo la kuhuzunisha sana. Kama vile Wabunge wametangulia kusema, ni muhimu kwa wanaotulinda, na wanaolinda Kenya kwa ujumla, wapate mafundisho mara kwa mara. Vile vile, ninataka kueleza Bunge hili kwamba Wakenya wamechoka kusikia kwamba uchunguzi utafanywa na hakuna jiwe litaachwa bila kupinduliwa. Tumechoka kusikia kwamba ukweli utapatikana na haupatikani. Jambo hili husemwa kila wakati na hatuambiwi ukweli. Hatuambiwi ni nani ameshikwa na ni nani amefanya kitendo kama hiki. Kama mkenya ametoa ripoti kwamba maisha yake yamo hatarini, mbona uchunguzi usianzie hapo? ...
view
10 Feb 2015 in National Assembly:
Wakenya wanahitaji usalama. Hatuwezi kukuza uchumi bila usalama. Hatuwezi kuenda shule bila usalama. Kwa hivyo, jambo la usalama ni namba moja. Ikiwezekana, fedha za kutosha za kukabiliana na ukosefu wa usalama zitolewe ili tuweze kuboresha Kenya yetu. Asante mhe Spika.
view
19 Nov 2014 in National Assembly:
Ninashukuru sana, Mhe. Spika. Hata mimi nachukua fursa hii kupeana rambirambi zangu kwa familia, jamaa na marafiki wa Senator Kajwang’. Kwa kweli, tumempoteza mtu shupavu, mtu mkakamavu, mtu ambaye alikuwa hana woga wowote; alizungumza kile ambacho alijua ni cha haki. Kwa kweli tumempoteza mtu aliyekuwa anapendwa na watu wengi. Nakumbuka hata katika mikutano yetu ya CORD The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
19 Nov 2014 in National Assembly:
akiwa amefika ulipata kwamba kila mtu alimshangilia na huo mkutano hungeisha kabla hajapewa nafasi ya kuzumgumza maanake wananchi wangelazimisha aongee. Katika wimbo wake wa “bado mapambano”, lazima kuna kitu ambacho alikuwa anahisi kwamba hatujafikia. Kama ni kuhusu ukombozi, alimaanisha hatukuwa tumeupata. Kwa hivyo, wimbo huo, ametuachia sisi ambao ni wachanga kisiasa tuweze kujua kwamba hatujafika na bado tung’ang’ane ili Kenya iweze kuwa mahali pazuri. Kwa hivyo, tunaiombea jamii yake. Tunawaweka katika maombi kwa sababu huu ni wakati mgumu sana na bila nguvu za Mwenyezi Mungu, hawataweza. Sisi sote tuweze kusimama na wao kwa maombi. Ninaamini ya kwamba Mungu ataisimamisha familia ...
view
28 Oct 2014 in National Assembly:
Hon. Chairlady, I beg to move:- The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
28 Oct 2014 in National Assembly:
THAT Clause 13 of the Bill be amended in sub-clause (1) by inserting the words “in consultation with the responsible County Government” immediately after the word “designate”. This is to bring in participation of the county governments. Mining has been more of a curse than a blessing in Africa. Thanks to slots of suspicion and lack of public participation with regard to decisions made around mining. By bringing county governments on board, this will be part of public participation as enshrined in Article 10 of the Constitution.
view
28 Oct 2014 in National Assembly:
Hon. Chairlady, it is the same as at Clause 13 which was meant to include the county governments. The Chairperson has already explained it and I understand. I, therefore, withdraw my amendment.
view